Tuesday, April 19

ALICHOKISEMA KITILA MKUMBO JUU YA MWENGE WA UHURU




Inahitaji bidii ya ziada katika kuelewa nia na malengo ya serikali ya CCM ya kusitisha maadhimisho muhimu ya siku muhimu za Uhuru na Muungano, lakini hapohapo inaendelea na mahangaiko ya mbio za Mwenge nchi nzima.

Maadhimisho ya siku za Uhuru na Muungano hutumika kutukumbusha tulikotoka kama nchi na kutoa ahadi ya kuendelea kupigania na kulinda uhuru na muungano wetu.

Aidha, maadhimisho haya hutumika kuvielimisha vizazi vipya kuhusu mapambano yenu ya kutafuta, kulinda na kuendeleza uhuru na muungano na kuwakumbusha wajibu wao wa kuendeleza mapambano haya.

Ni makosa ya kimantiki na kifalsafa kujaribu kukokotoa gharama za maadhimisho haya katika minajili ya pesa. Umuhimu wa kujitambua na kujipambanua kinchi na kitaifa huwa havipimwi kipesa!

Sasa hili la kuendelea na mbio za mwenge inakanganya mno madai ya Rais Magufuli kwamba anabana matumizi ya serikali.

Ni vigumu kueleweka katika ulimwengu na kimantiki na kifikra. Malengo ya mbio za mwenge yalishaisha na kimsingi mbio hizi hazina tena msingi wa kifalsafa.

Jambo la maana ni kwa Rais Magufuli kuwarudishia CCM mwenge wao ili waumiliki na kutunza kama sehemu ya historia ya chama chao.

Waliweza kutunyanganya viwanja na majengo mbalimbali tulivyovijenga sote kama nchi, kwa nini wanapata ugumu kujitwalia huu mwenge? Oops nilitaka kusahau kwamba Rais Magufuli ni zao la chama hikihiki. Basi sawa, tuendelee tu kuisoma namba!

No comments: