Leo December 9 2015 nimekuwekea
tena stori zote kubwa za Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye Udaku,
michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea nchini kwakoo.....
Wednesday, December 9
Tuesday, December 8
Tinga Tinga...Baada ya TRA kuifungia account ya shirikisho la soka Tanzania (TFF), imenifikia kauli ya TFF hapa …
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema tayari limeshaanza kufanya mazunguzo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kufikia hatma ya akaunti yake kufungiwa. Kupitia kwa Afisa Habari wa Shirikisho hilo, Baraka Kizuguto, amesema wao kama TFF hawahusiki na kufungiwa kwa akaunti yao, bali serikali ndio chombo pekee kinachopaswa kuhojiwa kwanini TFF haijalipa kodi.
Kizuguto ameweka wazi kuwa kodi ambayo TFF wanadaiwa imetokana na mishahara waliyokuwa wanalipwa Makocha wa kigeni, tokea ujio wa Marcio Maximo pamoja na deni la kodi ya mchezo wa Brazil na Tanzania, uliofanyika mwaka 2010. Mishahara hiyo ilikuwa ikilipwa na serikali pia Kamati maalum ya serikali ndiyo ilihusika na mechi ya Taifa Stars na Brazil maana mapato yake hayakuingia kwenye akaunti ya TFF.
“ TRA
wamezuia akaunti kwa madai kwamba kuna malimbikizo ya kodi ambayo
yanafakia zaidi ya Bilioni 1.6 na deni hilo limetokana na malipo ya
mishahara kwa makocha walioondoka, mapato yaliyopatikana kwenye mechi
kati ya Taifa Stars na Brazil, kwa maana hiyo mapato na mishahara ya
makocha hao ilikuwa haipitii TFF” >>>Kizuguto.
Shirikisho limesema kufungwa kwa akaunti
hiyo kumesababisha timu ya Taifa ya Vijana Chini ya umri wa miaka 15
(U15) kushindwa kuendelea na ziara yake ya kutembelea Kigoma, Burundi, Rwanda, Uganda na mwisho Nairobi Kenya kutokana shirikisho kushindwa kugharamia.
TRA inaidai TFF
zaidi ya bilioni 1.6 za kitanzania, ikiwa ni malimbikizo ya kodi kwa
kipindi cha mwaka 2010 – 2013 huku akaunti iliyofungiwa ina jumla ya
kiasi cha Shilingi milioni 300.
AHADI NI DENI......Duu!! mwanamitindo katimiza ahadi yake ya kuvua nguo baada ya Palmeiras kutwaa Ubingwa …
Stori za Brazil
kufanya vizuri katika soka zimekuwa kawaida sana ila siku hizi hii ni
mpya kutoka kwa mashabiki wao, inashangaza kidogo, tumewahi kusikia Mrisho Ngassa akiahidi kama atashindwa kufunga goli katika mechi Yanga dhidi ya Simba atachoma moto nyumba zake tano ahadi ambayo alifanikiwa kuitimiza kwa kufunga goli.
Ila kwa mashabiki wa kike wa Brazil wameingia katika headlines hii mtu wangu, wiki iliyopita mwigizaji wa Brazil Maite Proenca mwenye miaka 57 aliahidi kama timu yake ya Botafogo itashinda na kufuzu kucheza Ligi daraja la kwanza Brazil atavua nguo, December 8 ni headlines za mwanamitindo wa kibrazil Cintia Vallentim mbaye nae aliahidi ahadi kama hiyo kama timu yake ya Palmeiras itatwaa Ubingwa wa Brazil.
Cintia Vallentim ametimiza ahadi hiyo ya kupiga picha akiwa mtupu baada ya timu yake ya Palmeiras kuifunga Santos kwa mikwaju ya penati na kushinda Kombe la Brazil. Tukio hili linakuja ikiwa ni wiki moja imepita toka muigizaji Maite Proenca kufanya kama hivyo ila yeye ni baada ya Botafogo kushinda na kupanda daraja la kwanza.
Sunday, December 6
Fagio la JPM.... hawa ni maofisa waliosimamishwa kazi TANESCO...
Nitahakikisha nakupatia kila stori
inayonifikia….sasa hivi nakusogezea hii stori kutoka shirika la Umeme
Tanzania (Tanesco) kuhusu kuwasimamisha kazi maofisa 7 waandamizi
kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo wizi na ubadhirifu.
Akizungumza leo Dec 6, 2015 mbele ya waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba alisema…’Ukiacha
kero zinazosababisha na Miundombinu TANESCO inachukua hatua madhubuti
za kuwaadhibisha wafanyakazi wake wanaotoa huduma mbaya na kuwa kero kwa
wateja baadhi ya kero ambazo zimekuwa zikilalamikiwa pamoja na lugha
mbaya, wateja kudaiwa rushwa kabla ya kupewa huduma kucheleweshewa
huduma, ubadhirifu‘ – Mramba
‘Shirika linapenda kuwahakikishia
wateja wake kuwa tayari limeanza kuchukua hatua kali kwa wafanyakazi
wanaobainika kujihusisha na mambo hayo’ – Mramba
Kwa mfano
katika kipindi cha miezi miwili Shirika limewaachisha kazi maofisa 7
waandamizi kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo wizi na
ubadhirifu.Miongoni mwao ni wale waliofikishwa mahakamani kule Kagera
na kuripotiwa na vyombo vya habari jana.Walioachishwa kazi ni pamoja na
wafanyakazi wa ngazi za Mameneja, wahandisi na wahasibu’ – Mramba
‘Shirika
litaimarisha hatua hizo ambapo mfanyakazi yeyote atakayebainika
analaghai wateja, anadai rushwa anatoa lugha chafu au huduma mbovu
atawajibishwa mara moja na pale atakapobainika kuachishwa kazi‘Mramba
KIDUME NDANI.... Kim Kardashian na Kanye West waongeza furaha ndani ya familia yao…
Baada ya safari ndefu ya ujauzito wa staa huyo wa kipindi cha televisheni cha ‘Keeping Up with the Kardashians’ ambayo ilichukua headlines katika vyombo mbalimbali vya habari duniani hatimaye familia ya mastaa hao imejaliwa mtoto wa pili wa kiume jana Desemba 5.
Mtoto huyo ambaye mpaka sasa hajapewa jina anakuwa ni mdogo wa mtoto wao wa kwanza aitwaye North West.
Subscribe to:
Posts (Atom)