Nimekutana na jarida la New African Magazine toleo ya December 2015 na ndani ya jarida hilo nikakutana na list ya watu waliotajwa kama watu wenye ushawishi mkubwa zaidi Africa kwa mwaka huu wa 2015… kwa upande wa burudani nimekutana na mastaa watano huku Mtanzania akiwemo mmoja tu!
Hawa ndio Africa Most Influencial Africans in Media, Arts & Culture waliotajwa na jarida la New African Magazine:
Lupita Nyong’o – Kenya.
Baada ya kushinda tuzo yake ya kwanza ya Oscars ya Best Supporting Role kwenye filamu yake ya kwanza kubwa, Two Years A Slave, staa wa movie Lupita Nyong’o kutoka Kenya amezidi kuonyesha uwezo wake kwenye industry ya filamu Marekani kwa
kuzidi kupokea nafasi nyingi kubwa za kuigiza pamoja na kushinda tuzo
kadhaa kwenye majukwa mbalimbali Marekani. Licha ya hayo Lupita pia ni Balozi wa Wild Elephants na Mwanaharakati wa haki za Wanyama.
Trevor Noah – South Africa.
Mchekeshaji kutoka South Africa, Trevor Noah aliiteka dunia baada ya Marekani kumtangaza kuwa mtangazaji mpya atakayerithi kiti cha show ya comedy, The Daily Show nchini Marekani. Toka ujio wa Trevor Noah kwenye
kipindi hicho watazamaji wa show hiyo kutoka Marekani wametokea
kuvutiwa na mchekeshaji huyo ambaye material yake kubwa ya comedy
inaongelea sehemu kubwa ya maisha ya Kiafrika. Kwa mujibu wa ripoti
kadhaa zilizotolewa na mitandao tofauti Marekani, ujio wa Trevor Noah kwenye kipindi hicho kumeongeza watazamaji milion 1.5 kwenye show hiyo.
Diamond Platnumz – Tanzania.
Staa wa muziki wa Bongo Fleva na mshindi wa tuzo ya MTV Africa Music Awards 2015: Best Live Act pamoja na MTV EMA 2015: Best African Act, Diamond Platnumz kwa mwaka huu ametajwa kama mmoja wa wasanii wa kubwa wa Africa
kwa mwaka 2015 akiwa na ushawishi mkubwa ndani na nje ya Africa, akiwa
pia na mashabiki wakubwa na wanaomuongelea zaidi kwenye mitandao ya
kijamii kitendo kinachomfanya Diamond kuwa msanii kijana mwenye ushawishi mkubwa kwa mwaka huu wa 2015.
Yemi Alade – Nigeria
Baada ya hit song yake ya ‘Johnny’ kuweka headlines sehemu mbalimbali Africa staa wa muziki kutoka Nigeria, Yemi Alade alijipatia umaarufu mkubwa sana kupitia video hiyo ambayo ushawishi wake umegusa watazamaji zaidi ya milion 30 kweye mtandao wa YouTUBE. Ukiachia hayo style yake ya muziki pamoja na mavazi yake imetokea kuvutia wasichana wengi wanaofuatilia muziki wake.
Koffi Olomide – DRC Congo.
Mkongwe wa muziki kutoka Congo, Koffi Olomide amekuwa akijulikana kwenye industry ya muziki kuanzia miaka ya 1970 na bado umaarufu wake unagusa watu wengi wa rika zote duniani. Mwezi October mwaka huu 2015, Koffi aliachia album yake ya 13 na ya mwisho ikiwa na nyimbo 39. Licha ya kuachia Album yake ya mwisho Koffi anahesabika kama miongoni ya watu waliobadilisha sura ya muziki nchini Congo.