Saturday, March 12

MRADI WA PARTOMA WATOA MATOKEO YA UTAFITI WA WODI ZA WAZAZI

pat1

Mwenyekiti wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Kanga Meternity Trust (KMT) Dkt. Mohd Hafidh akitoa maelezo ya taasisi hiyo inavyofanya kazi zake kuhakikisha Mama wajawazito wanapata huduma bora wanapokwenda kujifungua hospitali Kuu ya Mnazimmoja katika hafla ya  kuwasilishwa  Utafiti wa Mradi wa PartoMa iliyofanyika Hoteli ya Tembo, Forodhani Mjini Zanzibar.
pat2
Madaktari bingwa wa Hospitali ya Mnazimmoja Dkt. Naufal Kassim (kushoto), Dkt. Zaki (kati) na Mwenyekiti wa KMT Dkt. Mohd Hafidh wakijadiliana jambo wakati wa hafla ya kuwasilishwa utafiti uliofanywa na Dkt. Anna Maaloe (hayupo pichani) kuhusu wadi za wazazi za Hospitali ya Mnazimmoja.
pat3
Mtafiti kutoka Mradi wa PartoMa Dkt. Anna Maaloe akiwasilisha utafiti wake juu ya huduma za wodi za wazazi za Hospitali kuu ya Mnazimmoja katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Tembo Forodhani Mjini Zanzibar.
pat4
Mwenyekiti wa Baraza la wauguzi na wakunga Dkt. Amina Abdulkadir akitoa mchango wake wakati wa kuwasilishwa utafiti wa huduma za wodi za wazazi za Hospitali kuu ya Mnazimmoja. Picha na Makam Mshenga-Maelezo Zanzibar.
pat5
Dkt. Ali Salum kwa niaba ya  Mkurugenzi wa Hospitali kuu ya Mnazimmoja akimkabidhi cheti na zawadi Metroni Mkuu  wa Hospitali hiyo kwa kushiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na Mradi wa PartoMa katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Tembo.
pat6
Wauguzi wa wodi ya wazazi katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja wakimpa zawadi ya mlango na kasha Dkt. Anna  Maaloe kwa kazi nzuri aliyosimamia ya utafiti wa wodi za wazazi katika Hospitali ya Mnazimmoja. Picha na Makam Mshenga-Maelezo Zanzibar.
………………………………………………………………………………………………………………………
Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar   
Mradi wa PartoMa unaoshirikisha  Chuo Kikuu cha Copenhagen nchini  Denmark na Hospitali Kuu ya Mnazimmoja   wenye lengo la kuongeza ufanisi na kuwajengea uwezo   wafanyakazi  wa  wodi  za wazazi katika hospitali ya Mnazimmoja umeanza kuleta  mafanikio makubwa.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mradi wa PartoMa kwa kushirikiana na Taasisi isiyo ya kiserikali Kanga Martenity Trust (KMT) iliyopo Hospitali ya  Mnazimmoja umeonyesha vifo vinavyotokana na  uzazi  na vifo vya watoto wanaozaliwa vimepungua tokea kuanza kwa mradi huo mwaka mmoja uliopita.

Akiwasilisha utafiti uliofanywa  na mradi wa PartoMa ambao uliwashirikisha madaktari, wakunga na wasaidizi wakunga katika wodi za wazazi, Dkt. Anna Maaloe amesema bado ni mapema kuthibitisha kuwa mafanikio hayo yanatokana moja kwa moja na kuwepo  mradi huo lakini ufanisi na utaalamu wa wafanyakazi  kwenye wodi za wazazi  Hospitali ya Mnazimmoja umeongezeka.

Amesema Hospitali za rufaa, kama ya Mnazimmoja zinawajibu mkubwa wa kuwa na mafunzo ya mara kwa mara kwa wafanyakazi waliopo na wanaotegemewa siku za mbele na kuweka miongozo bora ili kuokoa maisha ya mzazi na mtoto pamoja na wagonjwa wa kawaida.

“Kwa kuliona hilo mradi wa PartoMa umekuwa ukiandaa mafunzo  ya kuwajengea uwezo   madaktari na watendaji wa wodi za wazazi   Hospitali  Mnazimmoja siku moja kwa  miezi mitatu baada ya saa za kazi  na kuweka miongozo  ambapo  wafanyakazi wengi wamekuwa wakishiriki,” aliongeza Dkt. Anna.

Katika utafiti huo  Dkt.  Anna amesema imebainika kuwa wafanyakazi wengi wa Hospitali  ya Mnazimmoja wamehamasika kuongeza elimu na ufanisi na hiyo inasaidia katika kuokoa maisha ya  wananchi.

Hata hivyo amesema bado kunachangamoto katika kutoa huduma bora zaidi katika Hospitali ya Mnazimmoja ikiwemo  uhaba wa wafanyakazi katika wodi za wazazi ukilinganisha  na ongezeko kubwa la wazazi wanaotumia Hospitali hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Hoteli ya Tembo Forodhani, Mwenyekiti wa KMT Dkt. Mohammed Hafidh amesema utafiti huo ambao ni wa kwanza kufanywa na kuwashirikisha watafiti wa wazalendo  Hospitali ya Mnazimmoja utasaidia kuwa na taarifa sahihi na za uhakika kwa maendeleo ya Hospitali hiyo.

Amesema lengo la utafiti huo ni kuwasaidia mama wajawazito  kujifungua salama na kwa heshma na kuzuia vifo vya mama na mtoto ambavyo vinaweza kuzuilika.

Nae Dkt. Naufal Kassim amekiri kuwepo mtafartoMa  na ameshauri madaktari kujipanga kufanya tafiti zaidi za afya na kuyatumia  matokeo ya tafiti zilizopo kwa ukamilifu.

Katika hafla hiyo  Dkt. Ali Salum kwa niaba ya Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja aliwakabidhi  vyeti madaktari, wakunga na wasaidizi wakunga walioshiriki    mafunzo ya kuwajngea uwezo   baada ya saa za kazi  bila malipo katika hospitali hiyo.

WAKANDARASI WA MRADI WA MAJI MKOANI KIGOMA WABANWA .

 

 Naibu waziri wa maji na umwagiliaji mhandisi Izack Kamwele akikagua chanzo kikuu cha maji safi na salama cha mradi wa kuongeza upatikanaji wa maji katika mji wa kigoma kilichopo eneo la katonga.

Friday, March 11

MARCO ROBIO AMSHAMBULIA TRUMP

Muwania urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican, Marco Rubio amemshambulia mwenzake Donald Trump kwa kusema kuwa Uislam unaichukia Marekani, katika mdahalo uliorushwa kwenye televisheni huko Miami.

TAMISEMI YAKANUSHA AJIRA MPYA ZA WALIMU

 TAARIFA KWA UMMA
Kumekuwa na taarifa za upotoshaji zinasombazwa kwenye mitandao ya kijamii juu ya kutolewa kwa ajira mpya ya walimu kwa shule za sekondari na msingi kwa mwaka 2015/2016. 

Thursday, March 10

RAIS WA ZANZIBAR NA VIETNAM WAFANYA MAZUNGUMZO DAR


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, jana Ikulu Jijini Dar es Salaam akipofika kwa mazungumzo na ujumbe aliofuatana nao,Picha na Ikulu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Ujumbe wake (kushoto) wakiwa katika mazungumzo na Ujumbe wa Rais wa Vietnam Truong Tan Sang jana Ikulu Jijini Dar es Salaam akiwa nchini kwa ziara ya Kikazi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akifuatana na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang(katikati) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jana Ikulu Jijini Dar es Salaam(kulia) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Augustin Mahiga.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akiagana na mgeni wake Rais wa Vietnam Truong Tan Sang(kushoto) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jana Ikulu Jijini Dar es Salaam(katikati) mawair mbali mbali wa Vietnum walioungana na Rais Truong

AINGIA JELA MIAKA 7 KWA KUMKATA NYETI MKEWE ILI AMILIKI MALI


Mkazi wa Kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora, Mashaka Maziku (60) amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa kosa la kumkata sehemu za siri mkewe kwa imani za kishirikina ili apate mali.

Hakimu Joctan Rushwela alisema jana kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora imeridhishwa na ushahidi uliotolewa upande wa mashtaka.

Hakimu Rushwela alisema anamhukumu mshtakiwa huyo kwenda jela ili iwe fundisho kwa wengine wanaokuwa na tamaa ya kujipatia mali kwa njia za kishirikina.

Awali wakili wa Serikali, Idd Mgeni alidai kuwa mshtakiwa huyo na mganga wa jadi, walitenda kosa hilo kati ya Oktoba 29 na Novemba 2, 2014 katika eneo la Kazaroho Kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora.

Wakati wa tukio hilo, ilidaiwa kuwa Maziku aliambiwa na mganga huyo ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Kahele Paul kwamba akipeleka sehemu za siri za mkewe atapata Sh5milioni.

Alidai baada ya kupewa ushauri huo, alimchukua mkewe na kwenda kumnywesha pombe ili aweze kutimiza ukatili huo.

Alidai baada ya kunywa pombe nyingi, alichukua kisu na kumkata sehemu za siri mkewe na kuzihifadhi kwenye mfuko wa suruali yake na kutoweka. 
Alidai kwa mujibu wa mashahidi wanne, mwanamke huyo alikuwa akipiga kelele kutokana na maumivu makali aliyopata huku akivuja damu nyingi.

NDALICHAKO: VYETI FORM 6 VYENYE MFUMO WA GPA HAVIBADILISHWI.



Serikali imesema haina mpango wa kubadili vyeti vya wanafunzi waliomaliza kidato cha sita mwaka jana kutoka kwenye mfumo wa alama za GPA kwenda Divisheni.

Msimamo huo wa serikali, umetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako.
 
Amesema serikali haina mpango wa kubadili mfumo huo wa vyeti kwani tangu awali wanafunzi walisoma kwa mfumo wa GPA na vyeti vilitoka kwa mfumo huo.

“Hatuwezi kubadili vyeti hivyo, isipokuwa vimehitajika kwa ajili ya marekebisho madogo ambayo Katibu Mkuu wa Wizara, aliyasema lakini siyo kubadili kwenda mfumo wa divisheni,” alisema.

Februari mwaka huu, Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), lilitangaza kusitishwa kwa ugawaji wa vyeti vya kidato cha sita kwa wanafunzi waliohitimu mwaka 2015, huku likiagiza kuwa vile vilivyokwisha gawanywa kwa wahitimu hao vinatakiwa kurejeshwa kwenye chombo hicho.

Hata hivyo, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk, Charles Msonde, hakubainisha marekebisho ambayo wanatakiwa kuyafanya kwenye vyeti hivyo na badala yake kudai baraza linataka kujiridhisha na baadhi ya vitu.

Hatua hiyo ya kubadili vyeti hivyo iliibua utata mkubwa, huku baadhi ya wadau wakiwamo maofisa elimu, wakihisi Necta huenda inalenga kuvibadili vyeti hivyo kutoka kwenye mfumo wa wastani wa alama (GPA), kwenda kwenye ule wa jumla (division).

KUBENEA AKAMATWA NA JESHI LA POLIS AJUMUISHWA KESI YA UCHAGUZI WA MEYA DAR


MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea amekamatwa na Jeshi la Polisi leo asubuhi wakati akiwa katika Mahakama ya Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Kubenea amekamatwa na polisi akituhumiwa kushiriki kumpiga Terresia Mmbando, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mmbando alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliofanyika wiki mbili zilizopita na baadaye kuahirishwa hatua ambayo iliibua malumbano.

Kubenea  alikwenda leo mahakamani kuendelea na kesi yake inayohusu kumtukana Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Kesi hiyo ilifunguliwa tarehe 15 Desemba mwaka jana baada ya wawili hao kukutana kwenye Kiwanda cha Nguo cha TOOKU kilichopo Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Katika tuhuma za kumpiga Mmbando, waliokamatwa katika hatua ya kwanza ni Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Mwita Waitara, Mbunge wa Ukonga na madiwani wawili ambao kwa sasa wapo nje kwa dhamana.

Baada ya kupata dhamana Mdee alisema “Watake wasitake wataachia, hapa ni Ukawa tu. Yote haya yana mwisho lakini wajue kuwa namba ‘zinatufeva’ na si vinginevyo.”

Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar s Salaam ndio chanzo cha kukamatwa kwa Kubenea na wengine waliotangulia ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimekuwa vikisigana.

Ukawa wanalalamika kuminywa na Halmashauri ya Jiji kwa madai ya kushirikiana na CCM. Ukawa wameeleza kuwa zinafanyika hujuma ili CCM ishinde Umeya wa Jiji.

Jumla ya wajumbe wa mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji ni 161. Kwa upande wa Kinondoni kuna wajumbe 58 ambapo CCM wapo 20 na ukawa 38.

Temeke jumla ya wajumbe 49, CCM wapo 31 na ukawa 18 na Ilala jumla ya wajumbe 54 huku CCM wakiwa 23 ukawa 31.

Wednesday, March 9

Monday, March 7

Mtazame Rais Magufuli akimtangaza katibu mkuu mpya

SEKONDARY YA IYUNGA MBEYA TENA YATEKETEA MABWENI MAWILI


Mabweni mengine  mawili  ya  shule  ya  Sekondari  Iyunga  iliyoko  jijini  Mbeya  yameteketea  kwa  moto  mchana  huu.

Hii  ni mara ya pili sasa moto kuzuka katika shule hiyo .Wiki kadhaa zilizopita moto ulizuka na kuteketeza bweni moja la Mkwawa(‪Pichani‬) huku sababu zikielezwa ni hitilafu  ya  umeme  kutokana  na  uchakavu  wa  miundo  mbinu  shuleni  hapo.