habari
Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam Troung Tang Sang amewasili nchini leo hii kwa ajili ya ziara ya siku tatu yenye lengo la kuimarisha Ushiorikiano wa Kiuchumi na Kibiashara kati ya Tanzania na Vietnam.
Rais Trough Tang Sang akiambatana na ujumbe wa watu 51 ambao ni wafanyabishara pamoja na baadhi ya mawaziri kutoka Vietnam amepokelewa Ikulu jijini Dar es salaam na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikalini
Mara baada ya mapokezi hayo Rais Troung alifanya mazungumzo maalum na Rais Magufuli Ikulu maz\ungumzo yaliyojikita katika kuimarisha uhusiano wa kudumu kati ya nchi hizo mbili ikiwemo kupanua wigo wa uwekezaji utakaochochea biashara kati ya Tanzania na Vietnam pamoja na kukubaliana kuwekeana mikataba ya kutowatoza kodi mara mbili wawekezaji na wafanyabishara wanaowekeza katika nchi hizo.
Mara baada ya Mazungumzo hayo na Ugeni huo Rais Magufuli akizungumza na waandishi wa habari amsema kuwa ujio wa ujumbe huo utaleta chachu ya maendeleo nchini na itafungua uhusiano mpya wa kibiashara kati ya Tanzania na Vietnam sambamba na kuiongeza chachu ya uzalishaji katika sekta ya kilimo na viwanda kutokana na nchi hiyo kuimarika vizuri katika sekta hizo.
Kwa Upande wake Rais Troung Tang Sang amesema anajisikia fahari kuona Uhusiano kati ya Tanzania na Vietnam unaimarika na kuongeza kuwa Uhusiano na Ushirikiano huo utaleta maendeleo ya dhati nchini huku akisifu juhudi zinazofanywa na Serikali katika katika mapambano dhidi ya umasikini nchini.
Channelten tz
No comments:
Post a Comment