Tuesday, November 24

USINDI SURA MBAYA...SHINDANO LA SURA MBAYA ZIMBABWE LAMALIZIKA KWA GHASIA.....

Ghasia zimeibuka baada ya mwanaume mwenye umri wa miaka 42 kutangazwa kuwa mshindi katika shindano la mtu mwenye sura mbaya Jijini Harare nchini Zimbabwe, huku mashabiki wakiwatuhumu majaji kwa upendeleo.

Majaji hao walimchagua, Mison Sere, kuwa mshindi kutokana na kutokuwa na meno mengi na kuwa na uwezo wa kuibadilisha sura yake kwa kuikunja kunja, na kumshinda bingwa mtetezi William Masvinu, ambaye amekuwa bingwa tangu mwaka 2012.

Mshindi wa shindano la mwanaume mwenye sura mbaya nchini Zimbabwe, huibuka na zawadi ya dola 500, ambayo ni fedha nyingi ukizingatia wengi wa washiriki wa shindano hilo huwa hawana ajira maalum.
                                      Washiriki wa sura mbaya wakiwa katika mapozi tofauti 
                    Mshindi wa shindano la sura mbaya Mison Sere akiwa amebebwa juu

ZIARA YA HAPA KAZI TU...KATIBU MKUU KIONGOZI OMBENI SEFUE AFANYA ZIARA MUHIMBILI...

SEF1
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari ambao umefanyika leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli kwamba wagonjwa hawapaswi kulala chini. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru. Picha zote kwa hisani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
SEF2
Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue akisaini kitabu cha wageni mara baada baada yakwasili hospitalini hapo.
SEF3
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ambako amefanya ziara kuangalia utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuhusu huduma bora kwa wagonjwa na kutekeleza wagonjwa kutolala chini. Wagonjwa hivi sasa wanalala kwenye vitanda na siyo chini. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi na Jamii, Dk Donan Mmbando na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa ya Moi, Othuman Wanin Kiloloma.
SEF4
Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue akihoji kutokamilika kwa mashine ya MRI kwa wakati baada ya kutembelea chumba ambako mashine hiyo imehifadhiwa. Ofisa anayesimamia utengenezaji wa mashine hiyo, Monica ameahidi kwamba mashine hiyo itakamilika Alhamisi ijayo.
SEF5
Mmoja wa mafundi wa mshine ya ST-Scan akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue kuhusu utengenezaji wa mashine hizo. Fundi huyo ameahidi kwamba mashine hiyo itakamilika Jumatano.
Picha zote kwa hisani Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue leo amefanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na mambo mengine amesema serikali itaendelea kuboresha sekta ya afya nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati.
 
Akizungumza baada ya kutembelea MNH, Balozi Sefue amesema amekagua mashine za MRI na CT-SCAN na kueleza kuwa spea zimeshafika na kazi ya kutengeneza mashine hizo inaendelea. 
 
Pia amesema kwamba Serikali ya Tanzania imesaini mkataba mpya na Serikali ya Uholanzi wa kununua vifaa vipya na Hospitali ya Muhimbili itapata CT-SCAN moja wakati Hospitali ya Bugando itapata mashine moja ya MRI.
 
Pia, amewataka wahudumu wa afya kuwahudumia vizuri wagonjwa wanaotumia Bima ya Afya ili kuongeza mapato katika hospitali za serikali.
Akizungumzia kuhusu kudhibiti wizi wa dawa za serikali, Balozi Sefue amesema ni vema ukaimarishwa mfumo wa MSD kwa kutumia mifumo ya 
 Tehama na kuwa na maduka yao ya ndani.
 
Katika ziara hiyo, Balozi Sefue amepata fursa ya kufanya kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk Donan Mmbando na watendaji wa MNH ili kupata sura ya matatizo yote katika hospitali hiyo.

HATIMA YA MWILI WA MAREHEMU MAWAZO KUAGWA JIJINI MWANZA KUAMULIWA LEO NA MAHAKAMA.....


                                          

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema leo kimefungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, ili kuiomba Mahakama hiyo kutengua zuio la kuuaga mwili wa aliekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Geita Marehemu Alphonce Mawazo, lililotolewa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kutokana na hofu ya kiusalama pamoja na uwepo wa ugonjwa wa Kipindupindu.

Katika kesi hiyo, Chadema inawakilishwa na Mawakili watatu ambao ni James Millya, John Mallya pamoja na Paul Kipeja ambapo mlalamikaji ni Charles Lugiko ambae ni baba mdogo wa Marehemu Mawazo.

Mahamaka hiyo chini ya Jaji Lameck Mlacha, imesikiliza malalamiko ya upande wa washtaki na kuahirisha kesi hiyo hadi kesho ambapo imeamuru mlalamikiwa ambae ni Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mwanza pamoja na mwanasheria Mkuu wa Serikali kupelekewa nyaraka za kesi hiyo kabla ya kusikiliza utetezi wao hapo kesho.

Mapema kabla ya kesi hiyo kusikilizwa, wafuasi wa Chadema waliokuwa wamekusanyika nje ya viunga vya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, walilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia kuingia Mahakamani hapo ili kujua hatima ya kesi hiyo, ambapo wamesema kitendo hicho kinaondoa dhana ya Rais John Pombe Magufuli, kuwa yeye ni rais wa wananchi wote wakati wao kama Chadema wananyimwa haki zao.

Licha ya Malalamiko hayo pamoja na ulinzi mkali wa polisi uliokuwa umetanda Mahakamani hapo, bado wafuasi wa Chadema hawakuondoka katika viunga vya Mahakama hiyo hadi pale Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Freeman Mbowe alipowasihi kurejea majumbani mwao hadi kesho kesi hiyo itakaposikilizwa tena.

Ni zaidi ya siku nane sasa tangu marehemu Alphonce Mawazo auawe kikatili Mkoani Geita na watu wasiojulikana kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni chuki za kisiasa ambapo mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando.
SOMA ZAIDI »

BALOZI SEFUE AWAASA WATUMISHI WA UMMA KUWAJIBIKA.....

OM1 
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Bw Silasi David mmoja ya wagonjwa waliolazwa katika kitengo cha mifupa cha MOI.
OM2
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na mmoja ya wagomjwa waliolazwa katika kitengo cha mifupa cha MOI Bw. Muhusin Hamiri. 

                                                                                 Na Beatrice Lyimo- Maelezo
Watumishi wa umma wametakiwa kutumia muda wa kazi kuhudumia wananchi na sio kufanya kazi zao binafsi kwa kutumia ofisi na vifaa vya serikali.
Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alipofanya ziara katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa lengo la kuangalia maendeleo ya Hospitali kwa kukagua vifaa tiba na kuongea na watendaji wakuu wa hospitali hiyo.
Balozi Sefue ameongeza kuwa watumishi wa umma wanapaswa kufanya kazi kwa kutoa huduma bora na kwa upendo kwa wananchi kwani moja ya kanuni na taratibu za mtumishi wa umma ni kumhudumia mteja pasipo upendeleo.
 

“kwa upande wa madaktari na watoa huduma za afya mnatakiwa kutoa huduma bora na  zenye upendo kwa wananchi ili nao wajione wanahaki ya kupatiwa huduma hiyo”.
 

“kwa watumishi wote wa umma tukijitambua kuwa sisi ni watumishi wa umma tutafanya kazi kwa bidii na kwa kujituma” alifafanua Balozi Sefue.
Pia muda wa kuingia na wa kutoka ofisini na pia kujipima ni nini amefanya ndani ya masaa nane katika kuhudumia wananchi.
 

“Hizi si nguvu za soda ni lazima kubadilika pindi tunapowahudumia wateja kwa wakati na kwa ufanisi” alisema Balozi Sefue.
adhalika katika kuhakikisha serikali inatoa huduma bora kwa wananchi Balozi sefue ameagiza katika kila ofisi itoayo huduma kuwe na dawati la msaada kwa wananchi waweze kupata huduma kwa haraka.

MAADHIMISHO YA SIKU YA TAKWIMU AFRIKA YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM......

T1
Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Prof. Adolf Mkenda akihutubia wadau mbalimbali wa takwimu katika maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya “Takwimu Bora kwa Maisha Bora”.
T2
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo ya utangulizi katika katika maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya “Takwimu Bora kwa Maisha Bora”
T3
Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano Dkt. Carina Wangwe kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) akielezea umuhimu wa kujiunga katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii wakati wa maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya “Takwimu Bora kwa Maisha Bora”.
T4
Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof. Innocent Ngalinda akielezea umuhimu wa takwimu rasmi katika kupanga na kutathmini programu mbalimbali za maendeleo nchini wakati wa maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya “Takwimu Bora kwa Maisha Bora”.
SOMA ZAIDI »

KUHUSU RAIS WA ZANZIBAR....MGOGORO WA ZANZIBAR WATUA IKULU YA MAREKANI......

                                                                       Na Mwandishi Maalum, Washington

Wakati vikao vya siri vya kutafuta suluhu ya mzozo wa kisiasa visiwani Zanzibar vikiwa vimeripotiwa, juhudi za kuupatia ufumbuzi mzozo huo zimehamia kutoka Ikulu ya Zanzibar na kufika Ikulu ya Marekani (White House).
Wanachama wa ZADIA kutoka majimbo tafauti Nchini Marekani wakionyesha mabango yao.

Mnamo tarehe 21 mwezi huu, Wazanzibari waishio nchini Marekani waliandamana hadi kwenye Ikulu ya nchi hiyo katika juhudi za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa ili kuupatia suluhisho mzozo huo.

Akizungumza na waandishi wa habari mbele ya Ikulu hiyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) iliyoandaa maandamano hayo Bwana Omar Haji Ali, alisema kuwa maandamano hayo yanakuja katika juhudi za Jumuiya hiyo za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa katika kuukwamua mgando wa kisisas visiwani Zanzibar.

Aliendelea kusema kwamba maandamno hayo pia yana lengo la kumkumbusha rais Barack Obama wa Marekani kutekeleza ahadi yake ya kuilinda demokrasia Barani Afrika.
"Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika mapema mwaka huu, rais Obama alisema '.. pale ambapo raia hawawezi kutekeleza haki zao, basi ulimwengu una jukumu la kukemea. Na Marekani itafanya hivyo, hata kama wakati mwengine itakuwa inauma'..", alikumbusha Bwana Ali.

Aliongeza kuwa "Wananchi wa Zanzibar wameshindwa kutekeleza haki yao kwa zaidi ya nusu karne sasa. Wakati umefika sasa kwa ulimwengu kuchukua jukumu lake. Wakati umefika sasa kwa Marekani siyo tu kukemea, lakini pia kuchukua hatua za kivitendo ili kuhakikisha kuwa sauti za Wazanzibari zinasikilizwa na kuheshimiwa"

Alipoulizwa ni hatua gani watakazochukuwa iwapo Serikali ya Marekani haikuchukua hatua yoyote kusaidia kumaliza mgando wa kisiasa Zanzibar, Bwana Ali alisema "Tuna imani na rais Obama, na tumemfikishia barua ya malalamiko yetu, na tunasubiri jibu lake, na imani yetu ni kuwa atachukua hatua madhubuti khususan ikizingatiwa kuwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulikuwa wa mwanzo kutoa taarifa kuelezea kuwa uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa wa haki na huru" Alidokeza kuwa, iwapo hali itaendelea kubakia kama ilivyo, basi ZADIA itaelekea kwnye Umoja wa Mataifa.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) Bwana Omar Haji, akiongea na moja waandishi wa habari.

Katika maandamano hayo yaliyowashirikisha pia wapenda amani na demokrasia kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni, waandamanaji walibeba mabango yaliyokuwa na maneno kama vile "Mshindi wa uchaguzi atangazwe", "maamuzi ya Wazanzibari yaheshimiwe", "bila haki hakuna amani' na mengineyo.

Aidha, waandamanaji hao walipiga makelele wakidai "tunataka matokeo yetu ya uchaguzi.."

Akizungumza na Swahilivilla, raia mmoja wa Marekani aliyeshiriki kwenye maandamano hayo alisema "Nilimpeleka mwanangu kwenda kusoma kule, bado ana mapenzi na Zanzibar, na amenisimulia habari nzuri za amani, utulivu na ukarimu wa watu wake. Amekuwa akifuatilia hali ilivyo, na kwa hamasa kubwa alipopata habari za maandamano haya, akaniomba tuje kuwaunga mkono Wazanzibari katika kudai haki yao"

Itakumbukwa kuwa, wananchi wa Zanzibar walipiga kura mnamo tarehe 25 Oktoba mwaka huu, lakini Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Bwana Jecha Salum Jecha akatangaza kufutwa kwa uchaguzi huo Mkuu visiwani humo, kitendo ambacho wataalamu wa Sheria wamesema kuwa kinakwenda kinyume na Katiba ya Zanzibar.

Wachambuzi wanaona kuwa hatua hiyo ya Bwana Jecha ilikuja wakati asilimia kubwa ya matokeo yaliyokuwa yametangazwa yalikuwa yanampa ushindi mgombea wa urais wa Zanzibar kutoka chama cha upinzani cha Wananchi (CUF) Maliim Seif Shariff Hamad.

Kitendo cha kufutwa kwa uchaguzi huo ambao wachunguzi wa nje na ndani waliulezea kuwa ulikuwa wa haki na huru, kimezua mtafaruku wa kisiasa visiwani Zanzibar, na juhudi za ndani na nje zimekuwa zikifanyika ili kumaliza mgogoro wa kisiasa visiwani humo.

Maandamano ya ZADIA ni katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kimataifa za kusaka suluhu za mgogoro huo kwa njia za amani.
Mpenda amani na Demokrasia Lodi Mohamed akiongea na muandishi wa habari Njee ya Ikulu ya Marekani (White House)

UNDP YAKABIDHI MRADI WA DOLA ZA MAREKANI 150,000 WA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI KIJIJI CHA CHAMWINO....

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo akikata utepe kuzindua Kisima cha maji safi na salama katika kijiji cha Machali A wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma mwishoni mwa juma lililopita.                                                              
IMG_9772
Kisima kilichozinduliwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo.
UZINDUZI-MRADI
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja waMataifa la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), kijijini humo.
IMG_9802
                                      Bango la mradi uliozinduliwa na Bw. Alvaro Rodriguez.

Mfaham Huyu Hapa...Msanii wa bongofleva aliethibitisha kupata Zero kwenye mtihani wa Form IV...


MziwandaNATIONHuwa ni mara chache sana utasikia staa au mtu maarufu kajitokeza au kakubali kuweka wazi kuhusu sehemu aliyowahi kuharibu au kufeli kwenye maisha.
Kwenye muziki wa bongofleva tunae Nuh Mziwanda ambaye pia ni boyfriend wa msanii Shilole…… Nuh ameongea ukweli wa moyoni kwenye exclusive interview na millardayo.com na kusema >>> ‘Kwenye maisha yangu ninachojutia ni nilivyofeli mtihani wangu wa form IV nilipata Zero kabisa na sikufanya mitihani kama mitatu, yote hiyo ilitokea sababu ya muziki’
Nilikua mtoto mwenye akili sana na Mama yangu alikua anategemea nitakuja kuwa mtu flani mwenye elimu yake kwenye familia yetu na sio Mwanamuziki, nyumbani kwetu tuko watano na mimi ndio wa mwisho na nilikua nina akili sana kuliko wote na kuanzia la kwanza mpaka la saba nilikua sishuki kwenye Wanafunzi kumi bora‘ – Nuh
mziwandanation4Kwenye sentensi nyingine Nuh anamalizia >>> ‘Kupata Zero Form IV ni jambo ambalo linanifanya nijute sana mpaka sasa, ningekaza ningekua nafanya muziki huku nikisoma lakini nilivyojua maswala ya muziki tu nikaachana na Masomo, najutia…. nilikuja nikarudia tena mitihani na nikafeli, inaniuma sana… kama ninavyokosea kiingereza sio kwamba napenda, ni shule hamna’
Nuh amesema kuna uwezekano wa kurudi shule >>> ‘shule ni kitu muhimu haikataliwi, ni kitu poa unakuwa Mwanamuziki alafu una elimu yako… na muziki naudai sana ndio maana naukazania sababu ulinifanya nifeli shule’

Soma Vichwa Vya Habari kubwa za Magazeti 14 ya Tanzania leo... November 24 2015 kwenye Udaku, michezo na hardnews.....

 
Leo November 24 2015 nimekuwekea tena stori zote kubwa za Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye Udaku, michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea Duniani...
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.