Na Beatrice Lyimo- Maelezo
Watumishi wa umma wametakiwa kutumia muda wa kazi kuhudumia wananchi na sio kufanya kazi zao binafsi kwa kutumia ofisi na vifaa vya serikali.
Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alipofanya ziara katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa lengo la kuangalia maendeleo ya Hospitali kwa kukagua vifaa tiba na kuongea na watendaji wakuu wa hospitali hiyo.
Balozi Sefue ameongeza kuwa watumishi wa umma wanapaswa kufanya kazi kwa kutoa huduma bora na kwa upendo kwa wananchi kwani moja ya kanuni na taratibu za mtumishi wa umma ni kumhudumia mteja pasipo upendeleo.
“kwa upande wa madaktari na watoa huduma za afya mnatakiwa kutoa huduma bora na zenye upendo kwa wananchi ili nao wajione wanahaki ya kupatiwa huduma hiyo”.
“kwa watumishi wote wa umma tukijitambua kuwa sisi ni watumishi wa umma tutafanya kazi kwa bidii na kwa kujituma” alifafanua Balozi Sefue.
Pia muda wa kuingia na wa kutoka ofisini na pia kujipima ni nini amefanya ndani ya masaa nane katika kuhudumia wananchi.
“Hizi si nguvu za soda ni lazima kubadilika pindi tunapowahudumia wateja kwa wakati na kwa ufanisi” alisema Balozi Sefue.
adhalika katika kuhakikisha serikali inatoa huduma bora kwa wananchi Balozi sefue ameagiza katika kila ofisi itoayo huduma kuwe na dawati la msaada kwa wananchi waweze kupata huduma kwa haraka.
No comments:
Post a Comment