Hii stori imegusa kwenye vichwa vya habari za Magazeti ya Tanzania November 11 2015, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, na kasimulia stori
ilivyokuwa mwanzo mwisho mpaka wakapata taarifa kuhusu mpango wa ndoa
kufungwa kati ya msichana mwenye umri wa miaka 14 na mvulana mwenye umri
wa miaka 17.
“Tulipata
taarifa kutoka Kijijini kwao kutoka kwa wananchi ambao hawakufurahia
hicho kitendo, tukaweka mtego wa kufuatilia.. tulifanikiwa kupata
watuhumiwa ambao ni kijana anayeoa, baba na mama mzazi wa muoaji, na
mwalimu ambaye alihusika na alijua mkakati unaoendelea kwa mwanafunzi
wake“-Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, RPC Dhahiri Kidavashari.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi akaendelea na sentensi nyingine >>> “Wamekamatwa na sasahivi wako kituoni, taratibu za kuwafikisha Mahakamani zinaendelea“- Dhahiri Kidavashari.
Kisheria hii ishu ya ndoa ikoje? Majibu ya RPC haya hapa >>> “Kisheria
ilitakiwa iridhiwe na wazazi, kuna Sheria tatu, Sheria ya ndoa, Sheria
ya dini na Sheria za kimila… kisheria mtu yoyote chini ya miaka 18 hana
ridhaa ya kuamua ndoa, halafu huyo ni mwanafunzi aliyesajiliwa kufanya
mtihani.. Tuheshimu haki za Kikatiba za kila mtu, kusoma ni haki ya kila
mtu na wazazi wana wajibu wa kusomesha watoto… ni ng’ombe 11 tu
zilizotelewa ili aolewe“- Dhahiri Kidavashari.