Monday, February 1

ALIYESABABISHA GUZMAN KUNASWA AHOJIWA

Mwigizaji filamu wa Mexico Kate del Castillo anahojiwa kuhusiana na sakata inayomhusu mmoja wapo wa walanguzi wakuu wa dawa za kulevya Joaquin "El Chapo" Guzman ambaye sasa anatumikia kifungo gerezani.

Sunday, January 31

Marais wapinga kutuma jeshi la AU Burundi


Image copyright

Muungano wa Afrika AU hautatuma kikosi cha walinda amani hadi pale serikali ya rais Pierre Nkurunziza itakapotoa mwaliko.

Hatariiiii!!!! Mji wafurahia mtoto wa kwanza baada ya miaka 28

Ostina


Image copyright

Mji mmoja kaskazini mwa Italia unasherehekea kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza tangu mapema miaka ya 1980.

Matangazo ya bunduki yapigwa marufuku Facebook

Bunduki


Image copyright

Watu binafsi hawataruhusiwa tena kuweka matangazo ya kuuza bunduki katika Facebook na Instagram, kampuni ya Facebook ambayo pia inamiliki Instagram imetangaza.

Tai wa Israel aliyedhaniwa kuwa jasusi sasa huru

Tai


Image copyright

Tai huyo alitoka Uhispania
Tai mkubwa aliyezuiliwa nchini Lebanon akituhumiwa kuwa jasusi wa Israel ameachiliwa huru baada ya walinda usalama wa Umoja wa Mataifa kuingilia kati, maafisa wa Israel wamesema.

Wawindaji haramu wamuua rubani nchini Tz


Shirika moja la wakfu wa utunzaji wa mazingira, linasema kuwa rubani mmoja raia wa Uingereza, amepigwa risasi na kuuawa nchini Tanzania.
Rubani huyo anasemekana kuwa alikuwa akipepeleza mzoga wa ndovu porini alipodunguliwa na mwindaji haramu aliyekuwa amejificha .
Operesheni hiyo ilikuwa katika mbuga ya wanyama pori ya Maswa Kaskazini mwa Tanzania.

Ugiriki:Wasusia mechi kupinga vifo vya wahamiaji



Image copyright

Wachezaji wa timu mbili hasimu nchini Ugiriki wamesusia mechi wakipinga ongezeko la vifo vya wahamiaji wanaozama wakijaribu kuingia nchioni humo kukwepa vita Syria na Iraq.

BARCA WAINGIA NUSU FAINALI KOMBE LA MFALME



Mabingwa watetezi wa kombe la Mfalme Barcelona wamesonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Barcelona waliwachapa Athletic Bilbao kwa mabao 3-1 kwa mabao ya Luis Suarez, Gerrard Pique na Neymer na hiyo barca kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-2.

Nao Celta de vigo wakawaondoa katika michuano hiyo vijana wa Diego Simione Atletico Madrid kwa kuwachapa kwa mabao 3-2.

Robo fainali ya pili itapigwa leo usiku kwa Las Palmas kushuka dimbani kuwakabili Valencia, huku Mirandés wakiwa na kibarua pevu dhidi ya Sevilla.

JAMA ATOA MPYA KWA KUSAFIRI PEKE YAKE KWENYE NDEGE KWA LENGO LA KUTALII


Inaweza kutokea unasafiri kwenye gari hivi labda toka Dar mpaka Morogoro kwenye basi la abiria peke yako, unaweza kujifariji kwa kuchekicheki nje mazingira, ukachezea simu yako au ukaendelea zako na safari kwa kusikiliza muziki au kuangalia TV kwenye basi, lakini vipi kwenye ndege  inakuwaje?

Jamaa mmoja Alex Simon mtalii kutoka Austria, alijikuta kwenye level za kistaa hivi au mtu fulani VIP kwenye ubora wake baada ya kujikuta akiwa ndio abiria pekeake ndani ya ndege ya abiria zaidi ya 100… alitoka zake  Manila kwenda Boracay ndani ya Ufilipino kwa ajili ya kutalii tu !!

Baada ya Simon kuingia kwenye ndege alianza kupiga stori na marubani baadae akaungana na wahudumu wawili wa ndege wakiendelea na stori mpaka alipotua

Cheki Video ya jamaa mwenyewe hii hapa mwanzo mpaka mwisho wa safari.

MKAKATI WA MITI MIL. 10 KUPANDWA DODOMA WAWEKWA

Dodoma
 
MKOA wa Dodoma umejiwekea mkakati wa kupanda miti milioni 10 kwa ajili ya utunzaji mazingira.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa alisema hayo juzi mjini hapa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti kimkoa uliofanyika katika Chuo cha Serikali za mitaa cha Hombolo.

Alisema mkoa wa Dodoma unatarajiwa kupanda miti milioni 10, ambapo kila Wilaya itapanda miti milioni 1.5.

“Tunahitaji miti kwa ajili yetu sisi na kwa ujumla wetu, miti inauzwa kwa bei nafuu ambayo kila moja anaiumudu” alisema

Alisema uharibifu wa mazingira katika mkoa wa Dodoma ni mkubwa hasa kwenye maeneo ya vilima.

Alisema mwaka huu mkoa wa Dodoma umepata mvua nyingi ni vizuri kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kupanda miti.

Aliagiza kila shule ya msingi na sekondari kuwa na vitalu vya kupanda miti 400. “Hata kwenye mashamba binafsi miti ipandwe mashamba mengi ya Dodoma hayana miti tofauti na mikoa mingine ambapo mashamba yanakuwa na miti”
alisema

Akisoma taarifa ya hali ya upandaji miti kwenye chuo cha Serikali za mitaa cha Hombolo, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dk Mpamila Madale alisema chuo hicho kipo katika mpango mkakati wa kupamda miti kila mwaka jumla
ya miti isiyopungua 1,500 ili kuweza kuwa na miti mipya 7,500. Alisema kwa miaka mitano iliyopita  2010-2015, Chuo kilipanda miti jumla ya miti 6,000 sawa na asilimia 80 ya makadirio na kati ya hiyo miti 5,100 iliota

Alisema katika kipindi hicho lengo halikufikiwa kutokana na sababu ya ukame uliokuwepo mwaka 2015 ambapo chuo kilipanda miti katika maeneo machache.

“Upandaji miti siku ya leo kwa mashimo yaliyoandaliwa ambayo ni zaidi ya 1,600 Chuo kitahakikisha miti yote iliyopandwa inatunza na kuota yote kwa asilimia 100” alisema

Ofisa Misitu wa Manispaa ya Dodoma, Eline Kizigha alisema zoezi la upandaji miti katika mkoa wa Dodoma ytangu msimu wa mvua uanze mwaka huu limekuwa likitekelezwa na wadau mbalimbali wanaojihusisha na
hifadhi ya mazingira kutokana na kuwepo kwa mvua ambazo zinaendelea kunyesha hadi sasa.

Alisema tangu mwaka 2010 hadi 2015 jumla ya miti milioni 2.4 ilipandwa kwenye maeneo ya shule ya msingi, sekondari, watu binafsi na taasisi mbalimbali kama makanisa na vyuo kama Chuo cha Serikali za Mitaa na
Chuo Kikuu cha Dodoma.

Alisema  licha ya ukame mifugo pia huaribu ukuaji wa miti inayopandwa.
 

Mwandishi: John Banda Mhariri:Denice J. Kazenzele january 31/2016 {jumapili

HUU NDIO UNYAMA ALIOFANYIWA MSAGA NAFAKA WA MKOANI GEITA..ACHINJWA KISHA........!!

Zoezi la usafi wa mazingira katika kijiji cha Muungano nje kidogo ya mji wa Chato mkoani Geita limeingiwa dosari baada ya tukio la mtu mmoja kuuawa kwa kuchinjwa na kufungiwa ndani ya mashine ya kusaga nafaka hali iliyosababisha mamia ya watu kufurika kushuhudia tukio la kusikitisha na kuacha kufanya usafi kwenye maeneo yao.
 


ITV imeshuhudia mamia ya watu wakiwa wamefurika katika mashine ya kusaga nafaka inayomilikiwa na Bi.Jamira Abdu Mkazi wa Chato ambaye amemtaja marehemu kuwa anafahamika kwa jina la Juma Saidi alikuwa akifanya kazi ya kusaga nafaka katika mashine hiyo zaidi ya miaka saba na kusema kwamba hivi karibuni marehemu alikuwa na ugomvi na mkewake ambapo alihama nyumbani kwake na kuanza kulala mashineni hapo.

Baadhi ya wananchi wanaomfahamu marehemu Juma wamesikitishwa na tukio la mauaji ya kinyama na kuiomba serikali kuimalisha ulinzi na wengine wakuiomba kurejeshwa kwa jeshi la jadi Sungusungu kwa lengo la kukomesha matukio ya kihalifu.

Alipotakiwa kuthibitisha tukio hilo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Chato Bw. Shabani Ntalambe hakuwa tayali kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa anasimamia usafi wa mazingira ambapo ITV imelazimika kuzungumza na afisa mtendaji wa kijiji cha Muungano na diwani wa kata ya Muungano ambao wamethibitisha kutokea kwa mauaji ya kinyama.
Chanzo-ITV