Monday, February 1

ALIYESABABISHA GUZMAN KUNASWA AHOJIWA

Mwigizaji filamu wa Mexico Kate del Castillo anahojiwa kuhusiana na sakata inayomhusu mmoja wapo wa walanguzi wakuu wa dawa za kulevya Joaquin "El Chapo" Guzman ambaye sasa anatumikia kifungo gerezani.

Imebainika kuwa ndiye alipanga mkutano baina ya mlanguzi huyo El Chapo na mwigizaji mwengine wa Hollywood Sean Penn hapo Octoba wakati El Chapo alikuwa angali anasakwa baada ya kutoroka jela. .
Del Castillo na Guzman waliwasiliana kwa ujumbe wa maandishi mara kadhaa kabla alipokutana na Sean Penn huko kaskazini mwa Mexico.
Guzman alikamatwa tarehe 8 January, miezi 6 baada ya kutoroka jela lililokuwa lenye ulinzi mkali.
Image copyright
El Cchapo na Sean Penn
Baada ya kukamatwa na wanajeshi wa Mexico huko mjini Los Mochis kaskazini mwa Mexico alipelekwa jela ya Altiplano ambako yuko katika ulinzi wa saa 24.
Wakuu wa Mexico wangali wanatathmini pendekezo la kumkabidhi kwa Marekani ili kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria.
Sean Penn alifanya mahojiano na El Chapo kwa ajili ya makala iliyochapishwa na jarida la Marekani The Rolling Stone.
Polisi wa Mexico walikuwa wamehangaika sana kumsaka alipotorokea El Chapo , na wakapata mwamya pale alipokutana na Kate del Castillo.
Image copyright
Image captionEl Chapo alikamatwa baada ya kutoroka jela miezi sita iliyopita
Mkuu wa sheria wa Mexico Arely Gomez amesema maafisa salama walimfuatilia wakili wa Guzman hadi wakagundua mahali walipokuwa Sean Penn na Kate del Castillo.
Mawasiliano ya simu ya mkononi baina ya Kate del Castillo na Guzman yalibainisha kuwa awali Guzman hakuwa anamjua Sean Penn .
Huenda Guzman alivutiwa na Kate ambae ni mwigizaji mashuhuri huko Mexico.
Kate del Castillo alijulikana pia kwa uigizaji wake kama mlanguzi mkuu Bi Teresa Mendoza katika mfululizo wa vipindi vya Reina del Sur yaani Malkia wa Kaskazini.

No comments: