Sunday, January 31

Matangazo ya bunduki yapigwa marufuku Facebook

Bunduki


Image copyright

Watu binafsi hawataruhusiwa tena kuweka matangazo ya kuuza bunduki katika Facebook na Instagram, kampuni ya Facebook ambayo pia inamiliki Instagram imetangaza.
Facebook tayari ilikuwa imepiga marufuku uuzaji wa bunduki bila mtu kuchunguzwa historia yake, lakini sheria mpya sasa zinalenga kuzuia uuzaji na ununuzi wa bunduki kati ya watu binafsi katika mitandao hiyo ya kijamii.
Watu wanaomiliki biashara hata hivyo bado wanaweza kutangaza bunduki zao wakitumia kampuni au mashirika yao kwenye Facebook na Instagram. 
Mabadiliko hayo yamejiri wiki tatu baada ya Rais wa Marekani Barack Obama kufanyia mabadiliko sheria za uuzaji wa silaha.
Miongoni mwa mengine, Bw Obama ameifanya lazima kwa wauzaji wote wa silaha kuchunguza watu wanaotaka kununua silaha.

Image copyrightTHINKSTOCK

Majimbo pia yatatakiwa kutoa habari kuhusu watu ambao hawaruhusiwi kununua silaha kutokana na kutokuwa na akili timamu au kuhusika katika visa vya ghasia.
Mabadiliko hayo ya Facebook yanaweka vikwazo sawa na vilivyowekewa wauzaji wa mihadarati na dawa kwenye Facebook ambao kwa sasa inatumiwa na watu 1.59 bilioni duniani.

No comments: