Thursday, February 18

MATOKEO KIDATO CHA NNE 2015, YATANGAZWA......

Baraza la mitihani la taifa limetangaza matokeo ya kidato cha nne ambapo Watahiniwa 113,489 wamefeli mtihani wa kidato cha 4 mwaka 2015 na watahiniwa 272,947 wamefaulu.

NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YALIYOPANGWA KWA MFUMO WA DIVISION.
-Ufaulu umeshuka kwa asilimia 1.85 mwaka 2014 kwa mfumo wa GPA ambapo ufaulu ulikuwa ni asilimia 69.76 Mwaka 2015 ufaulu kwa mfumo wa division ni asilimia 67.91
- Wasichana wachukua nafasi tatu za mwanzo katika kumi bora.

SOMAAA....Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo February 18 2016 kwenye udaku, Hardnews na michezo..


February 18 2016 naanza kwa kukusogezea post ya stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye Udaku, Michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea..DSCN0452 DSCN0453 DSCN0416 DSCN0417DSCN0463DSCN0475 DSCN0454 DSCN0455 DSCN0456 DSCN0457 DSCN0458 DSCN0459 DSCN0460 DSCN0461 DSCN0462 DSCN0424 DSCN0425 DSCN0432 DSCN0433DSCN0465 DSCN0466 DSCN0467 DSCN0470 DSCN0436 DSCN0437 DSCN0438 DSCN0439 DSCN0471 DSCN0472 DSCN0442 DSCN0443

Tuesday, February 16

John Walker Feat Ras Lion - HODI MGANGA

KAMA KUNA MTU WA TUZO KUKUZA VIPAJI KWANINI ASIWE MKUBWA NA WANAWE? {SALAMU TMK ITAZAME HAPA NAFSI} YAMOTO BAND WAPYA

TUMBUA MAJIPU.......

Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesitisha mkataba wa Mkurugenzi wa bodi ya mikopo na wakurugenzi wengine wa nne kutokana na utendaji mbovu katika kuendesha bodi hiyo..

MSAADA...BONDIA MANNY PACQUIAO AKABIDHI NYUMBA KWA FAMILIA MASIKINI..


 Mwana masumbwi maarufu Duniani toka nchini Phillipines Emmanuel Dapidran Pacquiao (37) maarufu kama "Manny Pacquiao" amekabidhi nyumba kwa wananchi wa jimbo lake kwa ajlili ya makazi ya familia masikini zipatazo 1,000...

Akieleza wakati wa makabidhiano ya nyumba hizo kwa wananchi hao Pacquiao alisema, amejenga nyumba hizo kwa fedha ambazo amekuwa akizipata kutokana na malipo ya Ubunge na mchezo ya ngumi ambao unamuingizia pesa kibao.

Nyumba zenyewe ni hizo kama zinavyoonekana kwenye picha..

Kutoka kwa...WAZIRI MUHONGO.....

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amewataka wawekezaji katika sekta za nishati na madini kufanya utafiti wa kutosha katika maeneo husika kabla ya kuendelea na miradi yao.Profesa Muhongo aliyasema hayo katika mkutano baina yake na wawakilishi kutoka Kampuni ya Lake Holdings ukiwa ni moja kati ya mikutano kadhaa inayoendelea wiki nzima baina ya Wizara na wawekezaji wa sekta hizo.
Kampuni hiyo iliyosajiliwa mwaka 2012 ina mpango ya kujenga kituo cha kuzalisha umeme chenye uwezo wa megawati 300 hadi megawati 450 wilayani Songea mkoani Ruvuma.
Huo ni mradi mkubwa zaidi ukilinganishwa na mradi wao wa awali katika Kata ya Kiwira wilayani Rungwe, Mbeya uliolenga megawati 200 za umeme.

JPM...UTEUZI MPYA.....

Rais John Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi, makamishna wanne wa Jeshi la Polisi na pia amemteua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imewataja mabalozi walioteuliwa ni Dk Asha-Rose Migiro, Mathias Chikawe na Dk Ramadhan Dau.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, vituo vya uwakilishi kwa mabalozi hawa vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia kukamilika.Dk Migiro ambaye alikuwa miongoni mwa wana CCM waliojitokeza kuwania kuteuliwa kuwa wagombea urais, amewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Vile vile amewahi kuongoza wizara mbalimbali, ikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje; Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto pamoja na Wizara ya Katiba na Sheria aliyomaliza nayo kwenye Serikali ya Awamu ya Nne.

JIPU LA....MSD..

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amemwagiza Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD), kuwasimamisha kazi mara moja wakurugenzi wanne wa taasisi hiyo kutokana na tuhuma za kuwepo matumizi mabaya ya Sh bilioni 1.5.
Wakurugenzi hao ni Mkurugenzi wa Kanda wa MSD, Cosmas Mwaifwani, Mkurugenzi wa Fedha, Joseph Tesha, Mkurugenzi wa Ugavi, Misanga Muja na Mkurugenzi wa Manunuzi, Heri Mchunga.“Naomba uwaandikie barua za kuwasimamisha wakurugenzi hawa wanne ili wapishe uchunguzi wa matumizi mabaya ya Sh bilioni 1.5 za MSD,” alisema Ummy alipozungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam.
Ummy alisema taarifa alizonazo ni kwamba kiasi hicho cha fedha, kilitumika kununulia dawa kinyume cha utaratibu na Sheria ya Manunuzi ya Umma, hivyo kuna haja ya kufanyika kwa uchunguzi huo.

JIPU..TBC..

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amewasimamisha kazi watumishi wawili wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kutokana na utendaji usioridhisha.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TBC Dar es Salaam jana, Nape aliwataja watumishi waliosimamishwa kazi kuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Matukio, Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi, Edna Rajab ambao wamesimamishwa kazi na uamuzi huo utafikishwa kwa Bodi ya TBC kwa hatua zaidi.“Tunachukua uamuzi wa kuwasimamisha kazi watendaji hawa ili kujenga upya Idara hii muhimu katika ustawi wa TBC na habari kwa ujumla,” alisema Nape.
Aidha, Waziri huyo amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TBC kuwachukulia hatua watumishi wengine walio chini ya Idara hiyo kwa kuwa wako chini ya mamlaka yake na kutoa mrejesho wa hatua alizochukua dhidi ya wale wote wilioonesha utendaji mbovu.

SOMA HAPA...Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo February 16 2016 kwenye udaku, Hardnews na michezo.......

February 16 2016 naanza kwa kukusogezea post ya stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye Udaku, Michezo na hardnews ili ujue kinachoendeleaDSCN0322 DSCN0323 DSCN0324 DSCN0325 DSCN0326 DSCN0327 DSCN0328 DSCN0329 DSCN0330 DSCN0331 DSCN0332 DSCN0333 DSCN0334 DSCN0335 DSCN0336 DSCN0337DSCN0338 DSCN0339 DSCN0340 DSCN0341 DSCN0342 DSCN0343DSCN0344 DSCN0345 DSCN0346 DSCN0347 DSCN0348 DSCN0349DSCN0350 DSCN0351 DSCN0352 DSCN0353 DSCN0354 DSCN0355