Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amewataka
wawekezaji katika sekta za nishati na madini kufanya utafiti wa kutosha
katika maeneo husika kabla ya kuendelea na miradi yao.Profesa Muhongo
aliyasema hayo katika mkutano baina yake na wawakilishi kutoka Kampuni
ya Lake Holdings ukiwa ni moja kati ya mikutano kadhaa inayoendelea wiki
nzima baina ya Wizara na wawekezaji wa sekta hizo.
Kampuni hiyo
iliyosajiliwa mwaka 2012 ina mpango ya kujenga kituo cha kuzalisha umeme
chenye uwezo wa megawati 300 hadi megawati 450 wilayani Songea mkoani
Ruvuma.
Huo ni mradi mkubwa zaidi ukilinganishwa na mradi wao wa
awali katika Kata ya Kiwira wilayani Rungwe, Mbeya uliolenga megawati
200 za umeme.
No comments:
Post a Comment