Tuesday, February 16

JPM...UTEUZI MPYA.....

Rais John Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi, makamishna wanne wa Jeshi la Polisi na pia amemteua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imewataja mabalozi walioteuliwa ni Dk Asha-Rose Migiro, Mathias Chikawe na Dk Ramadhan Dau.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, vituo vya uwakilishi kwa mabalozi hawa vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia kukamilika.Dk Migiro ambaye alikuwa miongoni mwa wana CCM waliojitokeza kuwania kuteuliwa kuwa wagombea urais, amewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Vile vile amewahi kuongoza wizara mbalimbali, ikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje; Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto pamoja na Wizara ya Katiba na Sheria aliyomaliza nayo kwenye Serikali ya Awamu ya Nne.

No comments: