Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu amemwagiza Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari Kuu ya Dawa
(MSD), kuwasimamisha kazi mara moja wakurugenzi wanne wa taasisi hiyo
kutokana na tuhuma za kuwepo matumizi mabaya ya Sh bilioni 1.5.
Wakurugenzi hao ni Mkurugenzi wa Kanda wa MSD, Cosmas Mwaifwani,
Mkurugenzi wa Fedha, Joseph Tesha, Mkurugenzi wa Ugavi, Misanga Muja na
Mkurugenzi wa Manunuzi, Heri Mchunga.“Naomba uwaandikie barua za
kuwasimamisha wakurugenzi hawa wanne ili wapishe uchunguzi wa matumizi
mabaya ya Sh bilioni 1.5 za MSD,” alisema Ummy alipozungumza na
waandishi wa habari jana Dar es Salaam.
Ummy alisema taarifa
alizonazo ni kwamba kiasi hicho cha fedha, kilitumika kununulia dawa
kinyume cha utaratibu na Sheria ya Manunuzi ya Umma, hivyo kuna haja ya
kufanyika kwa uchunguzi huo.
No comments:
Post a Comment