Friday, October 7

DR.MAGUFULI ATISHIA KUMFUTA KAZI MTOTO WA DADA YAKE KWA KISA HIKI.................


Rais Dkt John Pombe Magufuli ametishia kufukuza kazi mtoto wa dada yake kutokana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutopeleka umeme katika kiwanda kipya cha kusindika matunda cha Bakhresa.

Rais Magufuli alisema jana alipokuwa akifungua rasmi kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa kilichopo Mwandege, Mkuranga mkoani Pwani.

Wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi, kiongozi mmoja wa kiwanda hicho akieleza changamoto wanazokumbana nazo alisema kuwa tatizo linalowakabili ni la umeme ambapo wameongea na TANESCO lakini hadi leo umeme haijafikishwa kiwandani hapo hivyo kuwalazimu kutumia jenereta kuendesha mitambo kitu kinachopelekea kuongezeka kwa gharama za uzalishaji.

Aliposimama kuhutubia Rais Magufuli aliuliza kama kuna kiongozi yeyote wa TANESCO mkoa wa Pwani ndipo akasimama mtoto wa dada yake. Rais Magufuli akamwambia anafahamu kuwa amefanya kazi nzuri alipokuwa Kagera na Tanga na kuwa anataka ahakikishe umeme unafika katika kiwanda hicho la si hivyo ataanza kumtumbua yeye ambaye ni mtoto wa dada yake.

Rais Magufuli alielekeza maswali mawili kwa TANESCO wakati wa hotuba yake, kwanza, kama TANESCO wanania ya kufanya biashara, kwanini hawapeleki umeme kiwandani hapo kwa sababu ni fursa ya kibiashara, pili aliuliza kama TANESCO wanania ya kuona Tanzania inakuwa ya viwanda, kama wanania, kwanini hawapeleki umeme kiwandani hapo.

Rais Magufuli ametoa miezi miwili kwa TANESCO kuhakikisha kuwa wanafikisha umeme kiwandani hapo kama wanataka kuendelea na kazi zao.

Kuhusu ombi la uongozi wa kiwanda hicho kutumia  gesi asilia inayopita jirani na kiwanda hicho, Rais Magufuli alisema kuwa watakaa na Wizara ni Nishati na Madini na Wizara ya Viwanda na Biashara kuona namna wanaweza kulishughulikia hilo.

No comments: