Sunday, September 20

HATA KATIKA MECHI NA SIMBA NITAFUNGA TU

 
Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma amesema mechi dhidi ya Simba, itakuwa kama mechi nyingine na ana uhakikaa atafunga.


Ngoma raia wa Zimbabwe, amefikisha mabao matatu katika mechi zake tatu za Ligi Kuu Bara. Mechi ya nne ni dhidi ya Simba, wikiendi ijayo.

"Nimeanza kuona ugumu wa ligi, lakini ninaona pia napata uzoefu na kujua cha kufanya. Simba ni watani wa Yanga lakini ni timu kama nyingine.

"Kufunga hakuwezi kuwa asilimia mia, lakini ninaamini uwezo wangu, ninawaamini wenzangu na ninaiamini timu kwa ujumla na ushirikiano wetu.

"Litakalotokea kama ni kufunga au kutoa pasi, lakini kikubwa Yanga ishinde ili twende na mwendo huu," alisema Ngoma.

No comments: