Katika kuadhimisha sikukuu ya Iddi el haji mkoa wa Morogoro viongozi wa dini ya kislamu wamesema misikiti sio mahala pa kampeni za kisiasa na hawapo tayari kuona nyumba za ibada zinatumika kama madaraja ya kuwavusha wanasiasa.
Wakihutubia waumini wa dini ya kislamu kwenye ibada ya sala ya Iddi el haji mkoa wa Morogoro viogozi hao wamewataka waumini kusherekea sikukuu ya Iddi el haji kwa kuzingatia misingi ya dini yao huku wakiendelea kuliombea taifa hasa wakati huu tunaoelekea uchaguzi mkuu ili uchaguzi ufanyike kwa haki na amani.
Naye mkuu wa mkoa wa Morogoro Dokta Rajabu Rutengwe amewataka wananchi kushiriki katika zoezi la uchaguzi kwa amani na utulivu ikiwa ni kutekeleza haki yao ya kideokrasia ya kuchagua viongozi watakao leta mabadiliko ya kweli kwa wananchi.
Via>>ITV
No comments:
Post a Comment