Thursday, September 24

WAJUE MARAIS WALIOONGOZA KWA MUDA MREFU BARANI AFRIKA, YUPO MSEVEN NA DOS SANTOS



Suala la iwapo marais wanafaa kuruhusiwa kuwania kwa muhula wa tatu katika nchi ambazo katiba inasema kiongozi anafaa kuwa mamlakani kwa mihula miwili pekee limechipuka tena huko Congo-Brazzaville.

Rais wa taifa hilo Denis Sassou Nguesso ametangaza kuwa taifa hilo litaanda kura ya maamuzi kuamua iwapo ataruhusiwa kuwania kwa muhula wa tatu.

Mjadala sawa unaendelea nchini Rwanda.

Lakini je, wajua ni viongozi gani wa sasa wameongoza mataifa yao kwa muda mrefu zaidi Afrika?

Hawa hapa:

•Miaka 36: Teodoro Obiang Nguema Mbasogo - Equatorial Guinea, alichukua madaraka kupitia mapinduzi ya serikali mwaka Agosti 1979

• Miaka 36: Jose Eduardo dos Santos - Angola, alichukua uongozi baada ya kifo cha rais wa kwanza wa taifa hilo Agostinho Neto Septemba 1979

Miaka 35: Robert Mugabe - Zimbabwe, alishinda uchaguzi wakati wa kujinyakulia uhuru kwa taifa hilo Aprili 1980

• Miaka 32: Paul Biya - Cameroon, alichukua uongozi baada ya kujiuzulu kwa rais wa kwanza wa nchi hiyo Ahmadou Ahidjo, Novemba 1982

• Miaka 30: Denis Sassou Nguesso - Congo, aliwekwa uongozini na jeshi mwezi Oktoba 1979 na akaongoza hadi mwezi Agosti 1992. Alirejea tena Oktoba 1997 na kuendelea hadi sasa.

Miaka 29: Yoweri Museveni - Uganda, alichukua uongozi rais baada ya kundi lake la waasi kuchukua madaraka mwezi Januari 1986
BOFYA HAPA CHINI UONE MAFURIKO YA HATARI YA MGOMBEA

No comments: