Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu
Hassan amevuna wanachama 272 Mkoani Tanga kutoka vyama mbalimbali vya upinzani
baada ya wanachama wa vyama hivyo kujiunga rasmi na CCM.
Bi. Samia Suluhu ambaye ni mgombea
mwenza wa Dk. John Pombe Magufuli amefanikiwa kuvunja ngome za wapinzani katika
mikutano yake ya kampeni mjini Tanga baada ya wagombea udiwani watano wa ACT
Wazalendo kujiunga na CCM pamoja na wanachama wengine 235 toka Tanga mjini
kujiunga na CCM kwenye mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa
Usagara mkoani Tanga.
Akihutubia katika mkutano huo wa
kampeni kunadi ilani ya CCM Tanga mjini uwanja wa Usagara, Bi. Samia Suluhu amewapokea
wagombea udiwani watano kutoka ACT Wazalendo, wakiwemo Wilson Elia (wa Kata ya
Duga), Gasper Maboko (Kata ya Nguvumali), Charles Luanda (Maweni) na Marry
Scoty (Kata ya Tanga Sisi) pamoja na Sada Mbwambo (viti maalum).
Mbali na madiwani hao kukihama chama
cha ACT, wanachama 235 kutoka ACT, CUF na Chadema wamejiunga na CCM kwenye
mkutano huo wa Tanga mjini huku wengine 37 wakijiunga na CCM katika mkutano
mwingine ulofanyika Jimbo la Muheza hivyo kutimiza wanachama 272 wapya kujiunga
katika mikutano ya siku hiyo.
Akizungumza na wanaCCM na wananchi
waliojitokeza mkutano wa Tanga Mjini, Bi. Suluhu amewaomba kuichagua CCM kurudi
madarakani ili kuendeleza maendeleo iliyofikia katika maeneo mbalimbali,
ikiwemo huduma za kijamii na miundombinu hasa ya barabara.
Bi. Samia amefanya mikutano minne
mikubwa katika majimbo ya Mkinga, Pangani, Mheza na Tanga Mjini na mikutano
midogo midongo sita alioifanya njiani akisimamishwa na wananchi wakitaka
kumsikia alipokuwa akipita.
********************************************************************
MWANZA
Msajili wa vyama vya siasa nchini
Mh.Jaji Francis Mutungi amewataka viongozi wa mathehebu ya dini,wamiliki wa
vyombo vya habari na asasi za kiraia wasikubali kutumiwa na wanasiasa kuvuruga
amani iliyodumu miaka 54 ya uhuru wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu 2015.
Wito huo umetolewa jijini Mwanza
katika maadhimisho ya siku ya amani duniani ambapo kitaifa yamefanyika jijini humo
na kuwahusisha, viongozi wa madhehebu ya dini, asasi za kiiraia, wasomi,
walemavu, wamiliki wa vyombo vya habari na wandishi wa habari Mh.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la
umoja wa mataifa linalojihusisha na utoaji elimu, sayansi na utamaduni kwa
jamii UNESCO hapa nchini Bi.Zurmila Rodriguez amewataka watanzania kudumisha
amani iliyopo miaka 54 ya uhuru hasa kwa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu
2015 kwa kumuenzi baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere ambaye
alipigania ukombzi wa nchi za Afrika na kuitangaza Tanzania kuwa kisiwa cha
amani duniani.
Kwa upande wake kaimu mkuu wa mkoa
wa Mwanza mchungaji Baraka Konisaga amesikitishwa na vurugu za wananchi
kuchukua sheria mikononi kwa kuvunja gari la jeshi la polisi vioo ambapo naibu
kamishina wa polisi ambaye ni kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Charles Mkubo
ameuhakikishia umoja wa mataifa kuwa jeshi la polisi Tanzania limejipanga
kikamilifu kuimalisha ulinzi wakati wa kampeni, siku ya kupiga kura na siku ya
kutangaza matokeo.
Ajenda kuu ya mkutano huo ni namna nchi zote tano za Afrika Mashariki zinavyoweza kuwa na matumizi sawa na viwango vinavyofanana vya dawa pamoja na kuhamasisha uwekezaji zaidi kwenye uzalishaji wa dawa.
Asilimia 80 ya dawa zinazotumika nchini huagizwa kutoka nje ya nchi, tena zikiwa na viwango tofauti, nyingine zikiwa chini ya viwango na nyingine zinazokubalika kwa kiwango cha kimataifa, kutokana na nchi zinapozalishwa dawa hizo na namna zinavyoingizwa.
Pamoja na tofauti za viwango, mkutano huo umejadili matumizi sahihi ya dawa ambayo yamekuwa na athari kubwa kwa watumiaji hususan kusababisha usugu wa dawa.
Miongoni mwa wadau wakuu kwenye eneo hilo, ni Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini (TFDA) ambayo imezungumzia mfumo huo mpya wa wazalishaji wa dawa unaoanza kutekelezwa kikanda na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kudai utakuwa na tija kwa watumiaji na kuondoa usugu ambao ulijitokeza wakati wa matumizi ya dawa ambazo azina viwango.
Imeelezwa
kuwa lishe bora ni muhimu kwa ustawi wa
watoto kiafya na kielimu hivyo ni vyema kwa serikali kuingiza katika katiba ya
nchi inayotambua moja kwa moja haki za watoto.
Kauli hiyo imetolewa na mgombea udiwani kata ya kisarawe kwa tiketi ya
chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA katika mdahalo uliofanyika katika
ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na kuwahusisha wagombea wa ngazi
hiyo katika kata hiyo ili kuzungumzia ajenda za watoto kuzungumzwa katika jamii.
Akiinadi Ilani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo, Baraka Musa
anayegombea udiwani kata ya Kisarawe, amesema chama chake kinaamini kuwa lishe
bora ni muhimu kwa ustawi wa watoto kiafya na kielimu na endapo kitaingia
madarakani kitahakikisha kinawekeza kwenye kupata Katiba inayotambua na kuzitaja
moja kwa moja haki za watoto.
Naye mgombea wa udiwani wa kata hiyo kupitia tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi Abel Mudo amesema endapo chama chake kitapata ridhaa ya kuendelea
kuongoza nchi kitawekeza zaidi katika shule na kuhakikisha zina walimu wa
kutosha na kwamba serikali yake imetengeneza mazingira rafiki na kutoa zana kwa
watoto wenye ulemavu.
Mgombea huyo ameahidi kufanya kazi pamoja na wadau mbalimbali ili
kuhakikisha wanapunguza ukatili kwa watoto na kukabiliana na matatizo ya
mimba za utotoni sambamba na kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa hadi kidato cha
nne.
Diendere ambaye alipindua serikali hiyo siku ya alhamisi wiki iliyopita amesema kuwa alifikia uamuzi huo kwa lengo la kile anachokiita kuepusha umwagaji mkubwa wa damu.
Kauli yake kukiri kukabidhi madaraka inakuja huku majeshi ya serikali yaki ukaribia mji mkuu wa Ouagadougou
Jeshi la Burkina Faso limeahidi kuwepo kwa hali ya Usalama kutokana na mapinduzi hayo,japo kuwa wameahidi kuto waangamiza waliofanya mapinduzi hayo iwapo tu watasalimisha silaha zao.
Hata hivyo kwa sasa Jeneral Diendere anadaiwa kujificha nyumbani kwa kiongozi wa kijadi Mogho Naaba.
bbcswahili/Re-Edited by Denice Kazenzele
Scott Walker,
ambaye ni miongoni mwa wagombea waliokuwa wakiwania kuteuliwa kugombea urais wa
Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican amejiondoa katika kinyang'anyiro
hicho.
Bwana Walker ambaye alikuwa gavana wa jimbo
la Winscosin amesema amejitoa kwenye kampeni hizo ili kutoa nafasi kwa uteuzi
wa mgombea muafaka atakayekabiliana na Donald Trump.Mgombea huyo, ambaye alikuwa akiungwa mkono kwa wingi na wafuasi wa mrengo wa kulia, lakini hata hivyo katika kura ya maoni kiwango chake kilishuka baada ya kufanya vibaya katika midahalo.
Bbcswahili/Re-Edited by Denice Kazenzele
************************************************************
MOGHADISHU SAA 06:00 MCHANA 22.09.2015
picha hii haina uhusiano wa moja kwa moja na habari husika |
Shambulizi lililotokea jana dhidi ya Ikulu ya Somalia mjini Mogadishu limesababisha vifo vya watu zaidi 9 na wengine 14 kujeruhiwa.
Mabomu yaliyotegwa ndani ya gari yalilipuka usiku wa siku hiyo nje ya lango la Ikulu ya Somalia, na watu 9 wakiwemo askari wawili wa jeshi la serikali na wageni 3 waliuawa kwenye shambulizi hilo.
Siku hiyo maofisa wa serikali ya Somalia na baadhi ya wajumbe wa nchi nyingine walikuwa wakikutana kwenye Ikulu hiyo kujadili uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.
Wakati mlipuko huo unapotokea, washiriki wengi wa mkutano huo walikuwa wameondoka, lakini walikuwepo maofisa wachache waliobaki ambao ni kati ya waliouawa na kujeruhiwa.
Kundi la Al-Shabaab limetangaza kufanya shambulizi hilo dhidi ya maofisa wa serikali ya Somalia.
Cri/Re-Edited by Denice Kazenzele
No comments:
Post a Comment