Friday, February 26

IJUEEEE.....ORODHA YA MIJI 10 YENYE FOLENI YA MAGARI DUNIANI DAR SIJUI NI YA NGAPI VILEEE...


Huenda ukawa umezoea na kuboreka na foleni ya jiji la Dar Es Salaam ambalo wakati mwingine inaweza kukugharimu kwa zaidi ya saa moja kukaa katika foleni kutoka Tegeta hadi Posta, hususani mvua ikiwa inanyesha  Dar Es Salaam sehemu huwa zinakuwa na foleni kubwa. Mtu wangu wa nguvu nimekutana na list ya mpya kutoka www.telegraph.co.uk ya miji 10 inayoongoza kwa foleni Duniani, imeandikwa 04/02/2016.

SOMA YA LEOOO.....Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo February 26 2016 kwenye udaku, hardnews na michezo....


February 26 2016 naanza kwa kukusogezea post ya stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye , Michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea....

Thursday, February 25

PATA HII.....TOKA IKULU YA TANZANIA.....

Ikulu imeahidi kufanyia kazi madai ya Chama cha Wasanii Wachoraji Tanzania (Chawata), ambayo waliyawasilisha jana, kikilalamikia ofisi hiyo katika awamu ya nne iliyokuwa chini ya Rais Jakaya Kikwete, kuwachelewa malipo yao ya Sh. milioni 53.6.

SOMA HII......TANZANIA na "Cash Budget"......

Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, imeamua kutumia mfumo wa ‘Cash Budget (kutumia kilichokusanywa), huku baadhi ya wachumi wakisema utaleta nidhamu ya matumizi ya serikali na kubana watumishi ambao walizoea kutumia vibaya fedha za umma kwa kuzipangia matumizi yasiyo na tija.
Wizara ya Fedha na Mipango imeeleza kuwa, mfumo wa kupanga na kutumia kinachokusanywa na Mamlaka ya Mapato (TRA), ndiyo ulioamuliwa kutumiwa na serikali ya awamu ya tano.Itakumbukwa kuwa, tangu Novemba mwaka jana, mapato ya TRA yalipanda kutoka wastani wa Sh. bilioni 800 na Sh. bilioni 900 kwa mwezi mpaka Sh. trilioni 1.3, Desemba, mwaka jana Sh. trilioni 1.4, Januari, mwaka huu Sh. trilioni 1.06 na malengo ya Februari ni kukusanya Sh. 1.03.
Jana Ofisa Habari wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ingiaheddi Mduma, alisema utaratibu wa kutumia kilichokusanywa utaendelea kutumika kila mwezi.
Alisema kila makusanyo yatakayopatikana kwa mwezi husika, yatatumika kulingana na mahitaji husika ya mwezi huo.
“ Mahitaji yakiwa mengi katika mwezi husika, basi hata fedha itakayokusanywa kwa mwezi huo itatumika kulingana na mahitaji hayo, tutakuwa tunafanya hivyo kila mwezi,” alisema Mduma.

UTAJIRI WA TANZANIA...

Tanzania imedhihirisha kuwa ni tajiri mkubwa wa rasilimali ya gesi asilia baada ya kugundulika kwa gesi nyingine katika bonde la mto Ruvu yenye ukubwa wa ujazo wa futi trilioni 2.17.
Ugunduzi huo wa gesi asilia umefanywa na Kampuni ya Dodsal Hydrocarbons and Power Tanzania Limited ambayo imekuwa inafanya shughuli za utafutaji wa gesi na mafuta katika Mkoa wa Pwani.Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Pilavullathil Surendran alisema jana katika mkutano wa wawekezaji wa gesi na mafuta ulioandaliwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuwa, thamani ya gesi iliyoko katika eneo hilo inafikia Dola za Marekani bilioni sita sawa na Sh trilioni 12.
Ugunduzi huo mpya unafanya hadi sasa Tanzania kuwa na amana ya gesi yenye ukubwa wa futi za ujazo trilioni 57.27.

PITIA HAPA.....Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo February 25 2016 kwenye udaku, hardnews na michezo.....


February 24 2016 naanza kwa kukusogezea post ya stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye , Michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea....DSC01243 DSC01244 DSC01245 DSC01246 DSC01247 DSC01248 DSC01249 DSC01251 DSC01252 DSC01253 DSC01254 DSC01255DSC01256 DSC01257 DSC01258 DSC01259 DSC01260 DSC01261 DSC01262 DSC01263 DSC01264 DSC01265 DSC01266DSC01267 DSC01268 DSC01270 DSC01271 DSC01278 DSC01279 DSC01280 DSC01281 DSC01282 DSC01284DSC01286 DSC01287 DSC01289 DSC01291

Sunday, February 21

SOMA HAPAAAA.....Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo February 21 2016 kwenye, Hardnews na michezo....


February 21 2016 naanza kwa kukusogezea post ya stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye , Michezo na haerdnews ili uju kinachoendelea...... DSCN0647 DSCN0648DSCN0671 DSCN0672 DSCN0673 DSCN0674 DSCN0681DSCN0676 DSCN0677 DSCN0678DSCN0649 DSCN0650 DSCN0651 DSCN0652 DSCN0653 DSCN0654 DSCN0655 DSCN0656 DSCN0657 DSCN0658 DSCN0659 DSCN0660 DSCN0661 DSCN0662DSCN0663 DSCN0664 DSCN0665 DSCN0666 DSCN0667 DSCN0668 DSCN0669 DSCN0670