Ikulu imeahidi kufanyia kazi madai ya Chama cha Wasanii Wachoraji
Tanzania (Chawata), ambayo waliyawasilisha jana, kikilalamikia ofisi
hiyo katika awamu ya nne iliyokuwa chini ya Rais Jakaya Kikwete,
kuwachelewa malipo yao ya Sh. milioni 53.6.
Kwa mujibu wa taarifa ya
Chawata kwa vyombo vya habari jana, fedha hizo zimetokana na kazi za
sanaa ambazo zilichukuliwa na serikali ya awamu ya nne kutoka kwa
wafanyabiashara wa eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam na kupelekwa
Ikulu.
Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa,
alithibitisha kuwapo na madai hayo na kuwa yatafanyiwa kazi ndani ya
wiki moja kuanzia jana.
“Ni kweli Ikulu inadaiwa, lakini ni deni la
awamu ya nne, kwa hiyo tumewaomba kuwakamilishia madai yao ndani ya wiki
moja, baada ya kufanya uhakiki ili kujiridhisha,” alisema Msigwa.
No comments:
Post a Comment