Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts

Thursday, November 17

JK AWATUNUKU DIGRII WAHITIMU 1,179 CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU DUCE

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (wa pili kulia) akimkabidhi zawadi mwanafunzi bora wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (Duce), Haji Mohamed wakati wa Mahafali ya Tisa ya chuo hicho leo. Jumla ya wanafunzi 1,179 walihitimu na kutunukiwa digrii za awali. 

SERIKALI YABARIKI UZINDUZI WA TELEVISHENI YA KIDIGITALI KUTOKA STARTIMES


Serikali kupitia Wizara ya Ujezi Uchukuzi na Mawasilano imebariki uzinduzi wa televisheni mpya ya kidigitali kutoka kampuni ya Startimes Tanzania. 

Wednesday, November 16

KIWANDA CHA KUTENGEZA VIROBA FEKI CHAKAMATWA.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla, akiwa ameongzana na timu ya Serikali yenye wataalamu na wanausalama wameendesha operesheni kali ya kusaka viroba feki na pombe nyingine haramu katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam  na kufanikiwa kukama shehena kubwa ya bidhaa hizo feki na haramu kwenye maeneo  hayo.

Saturday, October 8

ZSSF TENDER : PROVISION OF CLEANING SERVICES AT ZSSF PREMISES, ZANZIBAR

ZANZIBAR SOCIAL SECURITY FUND
                                                                P.OBOX 2716,
                                                KILIMANI MNARA WA MBAO,
                                                                  ZANZIBAR

Tender No. ZSSF/2016/2017/NC/01
For
Provision of Cleaning Services at ZSSF Premises, Zanzibar

 

Friday, October 7

WAFANYABIASHARA WA DRC WAIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA.

k1
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Congo (DRC) nchini Tanzania Bw. Sumail Edward (kulia) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa wafanyabiashara wa Congo kutumia Bandari ya Dar es Salaam baada ya Serikali kuondoa vikwazo, kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari  Bw. Tiganya Vincent.
k2
Baadhi ya waandishi wa habari wakimfuatilia kwa makini Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Congo (DRC) nchini Tanzania Bw. Sumail Edward (mwenye suti) wakati alipokuwa akielezea kuridhika na uamuzi wa Serikali ya Tanzania kuondoa vikwazo katika Bandari ya Dar es Salaam na kupelekea wafanyabiashara wa Congo (DRC) kuendelea kuitumia bandari hiyo.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MADUDU MAMLAKA YA USTAWISHAJI MAKAO MAKUU DODOMA (CDA)


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge), Bw. Uledi Mussa afuatilie malipo ya kiwanja kilichouzwa na CDA kwa sh. milioni 240 lakini fedha iliyoingia ofisini ni sh. milioni 6 tu.

Saturday, April 30

MKURUGENZI WA IDARA YA MAAFA NCHINI ATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIKA KWA MAFURIKO.

Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akizungumza jambo na Mkurugenzi wa idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali Mbazi Msuya wakati wakitembelea kijiji cha Mandaka Mnono kujionea athari ya mafuriko,katikati ni Mbunge wa viti Maalum (Chadema) mkoa wa Kilimanjaro Lucy Owenya.

Wednesday, April 27

PANYA ROAD 18 WADAKWA DAR

Jeshi la Polisi linawashikilia vijana zaidi ya 18 wenye umri kati ya miaka 14 na 20 kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uhalifu katika maeneo ya Wilaya ya Temeke.

Thursday, April 14

POLIS WATATU WATIMULIWA KATI KISHA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUPOKEA RUSHWA TABORA


Polisi watatu wa wilayani Urambo, Mkoa wa Tabora wamefikishwa mahakamani kwa mashitaka ya kuomba na kupokea rushwa. 

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Tabora, iliwafikisha askari hao jana katika Mahakama ya Wilaya ya Urambo huku mwingine akidaiwa kukimbia.

Askari hao waliofukuzwa kazi kabla ya kufikishwa mahakamani ni John Okinda, Kabila Pius na Patrick Robart. 

Anayedaiwa kukimbia ni Elisha ambaye polisi inaendelea kumtafuta. 

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Urambo, Hassan Momba, Wakili wa Takukuru, Edsoni Mapalala alidai washitakiwa walitenda makosa hayo Machi 7 mwaka huu.

Mapalala alidai siku hiyo katika kijiji cha Mkirigi, Kata ya Ilege, Wilaya ya Kaliua, washitakiwa hao wakiwa waajiriwa wa jeshi la polisi, waliomba rushwa ya Sh milioni tatu kutoka kwa Dotto Gandulanye ili wasimchukulie hatua za kisheria baada ya kumkuta akiwa na bangi.

Wednesday, April 13

KAMANDA WA POLIS MWANZA AWATAKA POLIS KUWAKABILI MAJAMBAZI KWA NGUVU ZOTE....


Kamanda mpya wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amewataka polisi kukabiliana na majambazi kwa nguvu zote na ikibidi kuwaua kabla hawajasababisha madhara makubwa kwa raia.

NEC YAPONGEZWA KWA UCHAGUZI WA 2015 KUMALIZIKA KWA AMANI


Kamati ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala imeipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kufanikisha kuendesha Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015 vizuri na kuiacha nchi ikiwa na Amani, utulivu na Usalama.

WANANCHI WATAKIWA KUWAOMBEA VIONGOZI

 

MKE wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa amewaomba wananchi wa wilaya ya Ruangwa kuwaombea dua viongozi wa taifa, Rais Dk. John Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ili waweze kufanya kazi zao kikamilifu. 

PICHA !! RAIS MAGUFULI AKIPOKEA HATI ZA UTAMBULISHO WA MABALOZI KUTOKA NCHI MBALIMBALI IKULU

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa nchi ya Jamhuri ya Czech hapa nchini Pavel Rezac, tukio hilo lilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.