Saturday, September 19

MPYA KUMHUSU LUKE SHAW

2C78A77900000578-0-image-a-2_1442589564680

Mchezaji wa Machester united Luke Shaw alipata injury kwenye mechi UEFA dhidi ya PSV na kukimbizwa hospitali ya karibu na uwanja uliokua unafanyika mechi ile. Baada ya kupata matibabu kwenye hospital ya St Anna huko Eindhoven, Luke Shaw anategemea kurudi Manchester kwa ajili ya kuendelea na matibabu zaidi.

HAYA HAPA MATOKEO YA EPL LEO MECHI ZA JIONI, ARSENAL ACHEZEA VIWILI KWA MTUNGI



Gabriel is blocked by Chelsea players as he tries to  confront Diego Costa


Premier League
 
Chelsea 2 - 0 Arsenal

TAMBWE AIBUKA SHUJAA YANGA IKIWATUNGUA JKT RUVU 4-1


Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe akishangilia moja ya goli lake alilofunga kwenye mchezo dhidi ya JKT Ruvu
Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe akishangilia moja ya goli lake alilofunga kwenye mchezo dhidi ya JKT Ruvu
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga, imeendelea kufanya kweli kwenye uwanja wa Taifa baada ya jioni ya leo kuibugiza JKT Ruvu jumla ya goli 4-1 kwenye mchezo wa raundi ya tatu ya ligi hiyo iliyoendelea leo.

Goli la kwanza la Yanga lilifungwa na mshambuliaji Donald Ngoma katiaka kipindi cha kwanza dakika ya 33 huku goli hilo lililodumu mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.
Yanga vs JKT Ruvu 
Kipindi cha pili Yanga walirudi wakiwa wamecharuka kwani dakika ya 48 kipindi cha pili Amis Tambwe aliifungia Yanga bao la pili,  dakikambili baadae Naftali Nashon akaifungia JKT Ruvu goli ambalo liliipa nguvu timu hiyo na kuanza kutafuta goli la kusawazisha.
Wakati JKT Ruvu wakiwa kwenye harakati za kutafuta goli la pili la kusawazisha, Amis Tambwe akapachika goli la tatu dakika ya 60 kwa upande wa Yanga ambalo ni goli lake la pili kwenye mechi ya leo huku Thabani Kamusoko akihitimisha kalamu ya magoli kwa upande wa Yanga kwa kufunga goli la nne dakika ya 87 ya mchezo.

HILI NDIO KUBWA KWA LEO KUTOKA KWA DK MAGUFULI WILAYANI CHATO

Dk Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa mwalimu wake wa darasa la kwanza marehemu, Cornel Pastory


Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijinadi kwa wananchi huku akishangiliwa aliposimama kusalimia katika Mji wa Nyakanazi, wilayani Biharamulo, Mkoa wa Kagera leo.

MANENO ALIYOYAANDIKA ANNIE MKE WA 2 FACE KWENYE CAKE KATIKA BIRTHDAY YA MUMEWE NDIYO YALIYOKUWA KIVUTIO KIKUBWA.........



Huenda katika Sherehe ambazo staa wa Nigeria 2 Face Idibia amewahi kuzifanya hii ambayo ilifanyika jana September 18 2015 ilikuwa imekaa poa zaidi !!

JUMAMOSI YAKO ITAKUWA NJEMA KINOMA NOMA KAM UTAANZA NA VITUKO HIVI VYA KUKUTOA MBAVU AHAHAHAHAHAHA MI NIMEANZA!!!!








HAYA HAPA NDIO MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPT 19,2015

 



Friday, September 18

MWAMERIKA ALIYEENDA KUTOA MSAADA KWA WAHANGA WA TETEMEKO ASIKITISHA WATU KWA KILICHOMKUTA!! FUATILIA KISA KIZIMA HAPA {VIDEO}

Dahlia Yehia alikuwa ni msichana mwenye furaha, amani na moyo wa kuwasaidia watu wenye shida lakini ndoto zake zilifupishwa baada ya safari yake ya kwenda Nepal kwenda vibaya!

NIMEONA NIKULETEE MIJENGO YA HOTEL ZA AJABU ZINAZOPATIKANA HUMU DUNIANI........


Teknolojia ya sasa inazidi kukua siku hadi siku, wataalamu wamekuwa wakibuni vitu mbalimbali duniani kwa lengo la kuleta ushindani.

WIZARA YA AFYA YAMTAKA MKEMIA MKUU ATAFUATILIA MATUMIZI YA SIGARA YA KIKO YA MAJI (SHISHA)

index 
 
………………………………….
WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imeiagiza Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufuatilia matumizi ya sigara ya kiko ya maji (Shisha) katika kumbi za starehe  za hapa nchini kwa kuwa sigara hizo zinahusishwa na  matumizi ya madawa ya kulevya.

USHAWAHI KUSIKIA NDOA YA FASTA FASTA? SASA HII IMEFUNGIWA BEACH MBELE YA WATU NANE......SOMA NA TAZAMA PICHA HAPA


Ronke na Lawson wamependana? Love yao hawakutaka masuala ya kusumbuana na ndugu masuala ya michango, vikao vya Harusi, kujaza watu Ukumbini.. wao kila kitu kimefanywa simple tu yani.

SERIKALI YAUJIBU UKAWA KUHUSU SAFARI YA RAIS NA GHARAMA,YADAI KUTOTUMIA HATA NUSU YA KIWANGO WALICHOKITAJA WAPINZANI

TAARIFA KWA UMMA - ZIARA ZA RAIS NJE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

Safari za Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete Nje ya Nchi.
 

Wizara imesikitishwa na taarifa za uongo zilitolewa katika vyombo vya habari kuwa Mhe. Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uongozi wake wa miaka 10 ametumia Shilingi trilioni 4 kwa ajili ya safari za kikazi nje ya nchi, ambazo ni wastani wa bajeti nzima ya wizara kwa miaka mitano (5).

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kutoa ufafanuzi kuwa tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aingie madarakani mwaka 2005, kiasi kikubwa kabisa cha bajeti kuwahi kutengwa kwa ajili ya safari za Viongozi Wakuu yaani Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu ni shilingi bilioni 50 ambazo zilitengwa kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015 kwa ajili ya Idara ya Itifaki. 


Kwa miaka mingine yote wastani umekuwa ni kati ya shilingi bilioni tano hadi 25 kulingana na mahitaji ya idara hiyo.
 

Ifahamike kuwa kiasi hicho cha shilingi bilioni 50 ni bajeti nzima ya Idara ya Itifaki, ambapo kuna fungu maalum kwa ajili ya ziara za viongozi. Fungu hilo linagharamia makundi makuu matano kama ifuatavyo:
 

1. Kundi la Rais wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
 

2. Kundi la Makamu wa Rais wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
 

3. Kundi la Waziri Mkuu wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
 

4. Kundi la Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka nje ya nchi wanapotembelea Tanzania; na
 

5. Kundi la Wajumbe Maalum wanaokuja nchini kuleta taarifa muhimu kwa Rais.
 

Makundi yote haya hugaramiwa na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ndani ya bajeti ya Idara ya Itifaki kifungu cha Ziara za Viongozi.

Aidha uandaaji wa bajeti ya Wizara chini ya Idara ya Sera na Mipango unahusisha wadau wengine nje ya Wizara kama vile Kamati ya Bunge ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na hupitishwa kila mwaka na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tunapenda kuwaatahadharisha wananchi juu ya watu wanaotoa taarifa za uongo kwa madhumuni ya kujenga chuki dhidi ya Serikali. Ikumbukwe kuwa ziara za viongozi zinazoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje zina mafanikio makubwa kwa nchi na Watanzania kwa ujumla.

Wizara inaandaa taarifa ya ndefu ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara, changamoto na mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka kumi ya uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambayo itatolewa kwa umma kwa lengo la kutoa elimu zaidi.
 

                                                                                        Imetolewa na:
                                                    Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
                                             Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
                                                                                  17 Septemba 2015

Queen Darleen: Muziki Umenikosanisha Na Boyfriends Zangu

Queen Darleen ambaye pia ni dada yake na Diamond amesema ameachana na wanaume wengi kutokana familia za wanaume kutomkubali kwa kudai ni mhuni.
11264967_899675290067888_1156573801_n 
Darleen alisema ndugu wa upande wa wanaume wamekuwa wakichochotea maneno kwa watoto wao hali iliyosabisha kuachana.