Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

Monday, November 14

AZAM FC YASAKA NA KUANDAA VIPAJI VIPYA


TanzaniaImage copyrightGOOGLE
Image captionVijana wakipepetana kuwania nafasi ya malezi ya vipaji maalum

Vijana saba wenye umri chini ya miaka 17, wamepenya kwenye majaribio ya wazi ya mwisho katika mkoa wa Dar es Salaam, yaliyoendeshwa na Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC mwishoni mwa juma.

Friday, October 7

LIGI YA WANAWAKE KUANZA KUTIMUA VUMBI NOVEMBA MOSI, TIMU 12 KUSHIRIKI


Timu 12 zinatarajiwa kushiriki Ligi ya Taifa ya Wanawake inayotarajiwa kuanza Novemba mosi, mwaka huu kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Maendeleo ya Soka la Wanawake na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), zilizoridhia tarehe hiyo.

Saturday, April 2

WAZIRI NAPE AFANYA MKUTANO NA WASAMBAZAJI WA FILAMU NA MUZIKI NCHINI LEO

ep1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiongea na wasambazaji wa filamu na muziki nchini wakati wa mkutano kati yake na wasambazaji hao uliojadili namna gani ya kuboresha tasnia hiyo kwa manufaa ya wasanii, wasambazaji na uchumi wa Taifa.(Picha Na Benjamin Sawe- WHUSM)

Sunday, January 31

Wawindaji haramu wamuua rubani nchini Tz


Shirika moja la wakfu wa utunzaji wa mazingira, linasema kuwa rubani mmoja raia wa Uingereza, amepigwa risasi na kuuawa nchini Tanzania.
Rubani huyo anasemekana kuwa alikuwa akipepeleza mzoga wa ndovu porini alipodunguliwa na mwindaji haramu aliyekuwa amejificha .
Operesheni hiyo ilikuwa katika mbuga ya wanyama pori ya Maswa Kaskazini mwa Tanzania.

Ugiriki:Wasusia mechi kupinga vifo vya wahamiaji



Image copyright

Wachezaji wa timu mbili hasimu nchini Ugiriki wamesusia mechi wakipinga ongezeko la vifo vya wahamiaji wanaozama wakijaribu kuingia nchioni humo kukwepa vita Syria na Iraq.

BARCA WAINGIA NUSU FAINALI KOMBE LA MFALME



Mabingwa watetezi wa kombe la Mfalme Barcelona wamesonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Barcelona waliwachapa Athletic Bilbao kwa mabao 3-1 kwa mabao ya Luis Suarez, Gerrard Pique na Neymer na hiyo barca kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-2.

Nao Celta de vigo wakawaondoa katika michuano hiyo vijana wa Diego Simione Atletico Madrid kwa kuwachapa kwa mabao 3-2.

Robo fainali ya pili itapigwa leo usiku kwa Las Palmas kushuka dimbani kuwakabili Valencia, huku Mirandés wakiwa na kibarua pevu dhidi ya Sevilla.

Thursday, December 17

YAMEMKUTA..haya Baada ya Vichapo Vingi......Jose Mourinho afutwa kazi Chelsea....

Meneja wa klabu ya Chelsea ya Uingereza amefutwa kazi baada ya klabu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo mabaya.

The Blues walishinda Ligi ya Premia msimu uliopita lakini msimu huu mambo yamekuwa kinyume, na wamo alama moja tu juu ya eneo la kushushwa daraja ligini.
Bodi ya klabu hiyo ilikutana jana kujadili hatima ya Mourinho chini ya mmiliki wa klabu hiyo, Mrusi Roman Abramovich.
Klabu hiyo kupitia taarifa imesema mkataba kati ya klabu na meneja hiyo umekatishwa kwa maelewano kati ya pande zote mbili na ikamtakia kila la kheri Mourinho.
“Sifa zake Stamfrod Bridge na Uingereza zinajieleza na daima anakaribishwa kurejea Stamford Bridge,” klabu hiyo imesema kupitia taarifa.
“Sasa tutaangazia kuhakikisha kikosi chetu kilichojaa wachezaji wenye vipaji kinafikia uwezo wake. Hakutakuwa na taarifa zozote zaidi kutoka kwa klabu hadi kocha mpya ateuliwe.”
Mreno huyo mwenye umri wa miaka 52 amekuwa Chelsea kwa kipindi cha pili, kilichoanza Juni 2013.
Chelsea walimaliza alama nane mbele kileleni msimu uliopita na kutwaa taji pamoja na Kombe la Ligi lakini mwaka huu wameanza vibaya, wakishindwa mechi tisa kati ya 16 ligini kufikia sasa.
Mechi ya mwisho kwa Mourinho kwenye usukani ilikuwa Jumatatu walipochapwa na viongozi wa ligi Leicester City 2-1.
Mourinho alitia saini mkataba mpya wa miaka minne tarehe 7 Agosti mwaka huu na ndiye meneja aliyefanikiwa zaidi akiwa na Chelsea.
Alishinda mataji matatu ya Ligi ya Premia kipindi chake cha kwanza katika klabu hiyo kati ya 2004 na 2007.
Pep Guardiola, Guus Hiddink, Brendan Rodgers na Juande Ramos na miongoni mwa wanaopigiwa upatu kumrithi.

Monday, December 14

TP Mazembe yachapwa 3 - 0 Klabu Bingwa Duniani....


Wawakilishi wa Afrika katika michuano ya kombe la dunia la vilabu timu ya Tp Mazembe imechapwa na wenyeji wa michuano hiyo timu ya Sanfrecce Hiroshima 3-0.
Wenyeji Hiroshima walipata mabao yao kupitia Tsukasa Shiotani, Dakika ya 44, Kazuhiko Chiba, 56, na Takuma Asano, akifunga bao la mwisho.
kipigo hicho kinainyima nafasi timu ya Tp Mazembe kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo hivyo watachuana na Klabu America, ya Mexico, ambayo nayo ilichapwa kwa mabao 2-1 Guangzhou Evergrande.
Kwenye nusu fainali Sanfrecce Hiroshima, watawachuana na River Plate, huku Barcelona wakikipiga na Guangzhou Evergrande.

Tuesday, December 8

Tinga Tinga...Baada ya TRA kuifungia account ya shirikisho la soka Tanzania (TFF), imenifikia kauli ya TFF hapa …


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema tayari limeshaanza kufanya mazunguzo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kufikia hatma ya akaunti yake kufungiwa. Kupitia kwa Afisa Habari wa Shirikisho hilo, Baraka Kizuguto, amesema wao kama TFF hawahusiki na kufungiwa kwa akaunti yao, bali serikali ndio chombo pekee kinachopaswa kuhojiwa kwanini TFF haijalipa kodi.
Kizuguto ameweka wazi kuwa kodi ambayo TFF wanadaiwa imetokana na mishahara waliyokuwa wanalipwa Makocha wa kigeni, tokea ujio wa Marcio Maximo pamoja na deni la kodi ya mchezo wa Brazil na Tanzania, uliofanyika mwaka 2010. Mishahara hiyo ilikuwa ikilipwa na serikali pia Kamati maalum ya serikali ndiyo ilihusika na mechi ya Taifa Stars na Brazil maana mapato yake hayakuingia kwenye akaunti ya TFF.
jengo-la-TFF
“ TRA wamezuia akaunti kwa madai kwamba kuna malimbikizo ya kodi ambayo yanafakia zaidi ya Bilioni 1.6 na deni hilo limetokana na malipo ya mishahara kwa makocha walioondoka, mapato yaliyopatikana kwenye mechi kati ya Taifa Stars na Brazil, kwa maana hiyo mapato na mishahara ya makocha hao ilikuwa haipitii TFF” >>>Kizuguto.
Shirikisho limesema kufungwa kwa akaunti hiyo kumesababisha timu ya Taifa ya Vijana Chini ya umri wa miaka 15 (U15) kushindwa kuendelea na ziara yake ya kutembelea Kigoma, Burundi, Rwanda, Uganda na mwisho Nairobi Kenya kutokana shirikisho kushindwa kugharamia.
TRA inaidai TFF  zaidi ya bilioni 1.6 za kitanzania, ikiwa ni malimbikizo ya kodi kwa kipindi cha mwaka 2010 – 2013 huku akaunti iliyofungiwa ina jumla ya kiasi cha Shilingi milioni 300.

Monday, November 30

WAMETUAGA HAWAAA....KWAHERI KOBE BRYANT, KWAHERI BLACK MAMBA,KWAHERI ROLE MODEL WA VIJANA WENGI WAPENDA BASKET, KWAHERI MTU WA KIKAPU... NI MUDA ULIFIKA SASA, NA SISI WOTE TUPO NYUMA YAKO. AHSANTE KWA YOTE ULIYOTUFANYA TUNAYAONE NDANI NA NJE YA UWANJA.....

kobbKobe Bryant , ambaye alisaidia Lakers kushinda mataji  matano ya NBA baada ya kuwa katika NBA kwa zaidi ya miaka  20 ambayo yote ameichezea timu aloipenda daima ya Los Angeles Lakers.
Kobe alitangaza Jumapili kwenye tovuti ya Wachezaji ‘kwamba ameamua kustaafu baada ya msimu huu , huku akiandika kwamba ” msimu huu ndio pekee uliobakia kwangu wa kuwapa nilichonacho. ”
Kobe aliandika kwa mtindo wa shairi huku akiliita “Dear Basketball” na ndani yake kukiwa na maneno kadhaa ya kugusa moyo wa kila mpenda michezo.
kobe
Mojawapo ni kauli ya “huu ndio mchezo uliompa   na kumtizimia ndoto mtoto aliyekuwa na umri wa mika 6 (akimaanisha mtotoyeye) tu ya kuchezea Lakers na nitaupenda kwa hilo siku zote.”
” Lakini siwezi kukupenda kwa dhati ile kwa muda mrefu, ” Bryant aliandika. ” Msimu huu ndicho ambacho mimi nimebakiwa nacho ambacho naweza kutoa. Moyo wangu unaweza kabisa kukabiliana na vurugu .
Mawazo yangu yanaweza vyema kushughulikia misuguano  lakini mwili wangu unajua ni wakati wa kusema kwaheri. “Na hiyo ni sawa . Mimi niko tayari ili uondoke uende zako mmpenzi basketball . ”
barua ya Kobe kuhusu kustaafu waliyokuwa wanagawiwa mashabiki mlangoni katika mchezo dhidi ya Pacers
barua ya Kobe kuhusu kustaafu waliyokuwa wanagawiwa mashabiki mlangoni katika mchezo dhidi ya Pacers
Kocha wa Lakers Bryon Scott alisisitiza kuwa Kobe Bryant atacheza mchezo wa Jumapili ambayo itakuwa jumatatu alfajiri kwa Afrika Mashariki. Katika taarifa yake Scott alisema ni kweli kuwa Bryant atastaafu lakini sio kwamba hatocheza maana amesema kuwa ni msimu wake wa mwisho na ataucheza kwa nguvu zote ikiwezekana.
“Nadhani yeye bado anaupenda sana mchezo huu ,” Scott aliwaambia waandishi wa habari . “Kiukweli  bado ana shauku kubwa kwa ajili yake na kikubwa  bado ni kijana mwenye ushindani wa hali a juu.
kobe
” Scott alisema alikuwa ” alistushwa ” wakati Bryant anampa taarifa yake Jumamosi usiku kwamba alikuwa anaenda kutangaza kustaafu kwake siku inayofuata.
kobee
“Alinistua aliponiletea taarifa hiyo kiasi fulani,” Scott alisema. Pengine nitakuwa mtu ninayesikitika kwa hili kuliko mtu yoyote mwingine au kitu chochote kile. Mtu ambaye nina mapenzi makubwa sana kwake na mtu ambaye nimekuwa nikiheshimu sana uwezo wake.
Siku zote huwa ni vigumu sana mtu wa kariba ya Kobe katika mchezo akiamua kutundika kila kitu” Hata hivyo mara kadhaa Kobe alikuwa akinukuliwa kwa kuelezea kuwa alifikiri huu ungeweza kuwa msimu wake wa mwisho.
Na kwa kuzingatia namna alivyoanza msimu kwa kiwango kibovu sio jambo geni sana lakini kwa rekodi, uwezo na jina alilojijengea katika NBA ni wazi kuwa ni taarifa kubwa sana.
Kobe Bryant ameshinda kila kitu katika NBA. Akicheza kwa miongo miwili yaani miaka 20, ameshinda tuzo ya MVP, kashinda mmedali zadhahabu za Olympic, kashiriki NBA All Star mara 17, ameshinda ubingwa wa NBA mara sita, kashinda tuzo za MVP za All star.
Hakuna alichobakisha au pointi zake 81 alizofunga katika mchezo mmoja. Pia ni mchezaji wa tatu aliyefunga pointi nyingi zaidi katika NBA.
koben
Kamishna wa Ligi kuu  ya kikapuMarekani, Adam Silver naye alitoa maoni yake kwa kusema awe anagombea ubingwa wa NBA, au akiwa katika uwanja tupu wa mazoezi akijaribu kurusha mitupo yake, Kobe Bryant anabaki kuwa mchezaji na mtu mwenye Upendo mkubwa kwa mchezo huu.

PATA HII...BALE, RONALDO KILA MMOJA ATUPIA MADRID IKIITANDIKA EIBAR 2-0 NYUMBAN......


Eibar: Riesgo, Capa, Pantic, Dos Santos, Junca, Escalante, Dani Garcia, Adrian (Verdi 69 mins), Saul Berjon, Inui, Enrich (Arruabarrena 86)
Subs not used: Irureta, Ramis, Silvestre, Harjovic, Luna
Booked: Dos Santos, Escalante

Real Madrid: Navas, Carvajal (Benzema 85), Nacho, Pepe, Danilo, Kroos, Modric, Kovacic (Casemiro 79), Rodriguez (Lucas Vazquez 65), Bale, Ronaldo
Subs not used: Casilla, Arbeloa, Cheryshev, Lazo
Goal: Bale 43, Ronaldo pen 82











MTAZAMO WA SALEH ALLY....KUHUSU JEZI ZA KILIMANJARO STARS..........

KILA siku binadamu anajifunza jambo jipya, huenda jana halikuwepo au kusikika. Lakini leo mambo yanabadilika na linakuwa gumzo au linalotakiwa kufanyiwa kazi.

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ndiyo ulizaa Tanzania yenye Bara na Visiwani. Hili ni jambo ambalo Watanzania wengi wamekuwa wakilipigania kuhakikisha linadumu.
Lakini kuna kitu ambacho nilikifikiria, lakini pia nikapata changamoto kutoka kwa mdau mmoja wa soka. Linahusu jezi ambazo timu zetu tatu kubwa za taifa zimekuwa zikitumia.
Tuna Taifa Stars ambayo inajumuisha Tanzania Bara na Visiwani na hii ndiyo inayobeba picha ya muungano hasa.
Taifa Stars inatuwakilisha kila tunapokwenda kushiriki mashindano yoyote chini ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) na lile la Afrika (Caf).
Lakini tuna timu nyingine mbili ambazo zinakuwa wawakilishi wa Watanzania wakati wa michuano ua Ukanda wa Afrika Mashariki. Hiyo ni michuano ya Chalenji ambayo Bara wanawakilishwa na Kilimanjaro Stars huku Visiwani wakiwakilishwa na Zanzibar Heroes.
Hizi timu zinakuwa zinajitegemea kwa maana ya ukanda na Tanzania inakuwa na wawakilishi kutoka pande mbili. Jambo ambalo ni zuri kwa kuwa linatanua wigo zaidi.
Sitaki kuingia kwenye ile vita ya Zanzibar nao wamekuwa wakitaka uwakilishi upande wa Caf na Fifa. Mimi zaidi nitalenga kwa upande wa jezi, bora zikiwa za aina tatu tofauti na sasa ni aina mbili.
Wachezaji wa Zanzibar wanapokuwa pamoja wale wa Tanzania Bara, wanaunda Taifa Stars na kutumia jezi moja. Wakienda kwenye michuano ya Chalenji, Zanzibar Heroes wanakuwa na jezi zao lakini Kilimanjaro Stars wanabaki na jezi za Taifa Stars.
Hii kidogo ndiyo inanipa mkanganyiko, ndiyo maana nikaamua kuifikisha hapa kama sehemu ya mjadala. Simlaumu mtu, badala yake natamani nanyi mlifikirie hili ana kuona nini kifanyike.

Binafsi ninaona itakuwa sahihi kama kutakuwa na jezi za aina tatu tofauti. Kwa kuwa tayari zipo za Taifa Stars na Zanzibar Heroes, basi Kilimanjaro Stars ingekuwa na jezi zake zinazojitegemea kabisa.

Kwangu naona hii, kwanza italeta usawa sahihi na maana sahihi ya kuwa Tanzania ina timu tatu tofauti zenye hadhi ya kuitwa timu ya taifa. Lakini itatengeneza taswira inayoeleweka kwa kila kikosi kati ya hivyo vitatu.
Kwa sasa taswira ya kikosi cha Kilimanjaro Stars, imejificha ndani ya kivuli cha Taifa Stars, jambo ambalo ninaona si sahihi hata kidogo, kwa nia nzuri tu.

Tuaiacha Taifa Stars iendelee kujitegemea kuliko kuifanya Kilimanjaro Stars ni sawa na Taifa Stars wakati inakuwa haina wachezaji kutoka Zanzibar.

Tuwafanye wachezaji wapate hisia ya tofauti kati ya Taifa Stars na Kilimanjaro Stars kama ambavyo wanavyoipata wale wanaokwenda Zanzibar Heroes, kwa kuwa jezi pekee zinaweza kuwapa hisia hiyo, sasa wako upande upi.
Hili si kosa, huenda watu hawakuwahi kuliona kama ni muhimu sana lakini kwangu naona lina umuhimu mkubwa kuanzia kwa maana, kwenda kwa wachezaji wenyewe kwa hisia lakini pia hata thamani pia hisia za mashabiki.
Ninaamini bado wachezaji wanapaswa kujua heshima ya jezi hizo tatu. Pia bado wana kila sababu ya kujua, kufanya vizuri katika klabu, kufanya vizuri zaidi katika Zanzibar Heroes na Kilimanjaro Stars ni uhakika wa kuitumikia Taifa Stars ambayo inatubeba Watanzania wote.
Jezi haliwezi kuwa jambo gumu sana kama TFF itaamua kulifanyia kazi mara moja na kulimaliza hilo. Baada ya hapo, utambuzi na tofauti zitakuwa wazi.
Hakuna haja ya kuepuka au kuona si sahihi kwani hata majina tu ya timu zenyewe, yanaonyesha jezi zinatakiwa kuwa tatu tofauti.

Kila la kheri Kilimanjaro Stars katika michuano ya Chalenji dhidi ya Ethiopia, leo.

Sunday, November 22

Algeria kumshitaki kocha wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa...Hizi sababu zao....

November 17 timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilicheza mchezo wake wa pili wa kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi dhidi ya timu ya taifa ya Algeria mjini Blida katika uwanja wa Mustapha Tchaker, ikiwa ni siku tatu tu zimepita toka wacheze mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu michuano hiyo uwanja wa Taifa Dar Es Salaam na kumalizika kwa sare ya goli 2-2.
Mchezo wa pili uliyochezwa mjini Blida ulimalizika kwa Algeria kuibuka na ushindi wa goli 7-0 ila kabla ya mchezo huo kuanza waalgeria wana mtuhumu Mkwasa kutoa kauli za kibaguzi, hivyo wamepanga kumshitaki kwa shirikisho la mpira wa miguu ulimwenguni FIFA kwa kusema wao ni wabaguzi wa rangi.

Full Kilichotokea....Burundi Vs Zanzibar Heroes CECAFA Challenge 2015 …

Michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika Mashariki na kati maarufu kama CECAFA Senior Challenge Cup yameanza leo November 21 mjini Addis Ababa Ethiopia, ikiwa ni michezo miwili ilikuwa inatarajia kuchezwa leo November 21, timu ya Zanzibar Heroes dhidi ya timu ya taifa ya Burundi ndio zilikuwa timu za kwanza kufungua dimba kabla ya wenyeji Ethiopia watakaocheza dhidi ya Rwanda.
????????????????????????????????????
Burundi ambao walikuwa na nyota wao kadhaa akiwemo Didier Kavumbagu anayekipiga katika klabu ya Azam FC ya Tanzania walikuwa wakiutawala mchezo kwa wastani kumiliki mpira kwa asilimia 56 katika kipindi cha kwanza wakati Zanzibar walikuwa na asilimia 44 za umiliki wa mpira kwa dakika zote 45 za kwanza.
Ethiopia-cecafa-e1448110702168
Mchezo huo ambao Burundi walikuwa wakifika sana langoni kwa Zanzibar Heroes hadi wanaenda mapumziko walikuwa wanaongoza kwa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Didier Kavumbagu dakika ya 38. Licha ya kipindi cha pili Zanzibar kutafuta nafasi ya kusawazisha goli hilo haikuwezekana.

Wednesday, November 18

AGEUKA KIVUTIO ALGERIA...ANGALIA HUYU MWARABU ALIVYOKUWA AKIMUANGALIA SAMATTA....

WAKATI WACHEZAJI WA TAIFA STARS WAKITEMBEA KATIKA MITAA YA BILDA, MBWANA SAMATTA ALIENDELEA KUWA KIVUTIO NA MASHABIKI WALIKUWA WAKITAMANI ANGALAU KUPIGA NAYE PICHA. ANGALIA SHABIKI HUYO ALIVYOKUWA AKIZUBAA UTAFIKIRI KAMUONA SAMUEL ETO'O.




HATIMAYE AIBUKIA KINONDONI....KMC FC YAANZA MAZUNGUMZO NA SELEMANI MATOLA....


Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola, amethibitisha kuwa kwenye mazungumzo na Klabu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC FC) inayoshiriki Ligi Darala la Kwanza, lakini hofu imetanda klabuni hapo, kwani imebainika haziivi na kocha wa timu hiyo, Amri Said ‘Jap Stam’ ambaye pia aliwahi kuwa kwenye benchi la Simba msimu wa 2010.

Matola ambaye aliachana na Simba wiki iliyopita kwa kile alichobainisha ni kutokuwa na maelewano mazuri na kocha mkuu, Dylan Kerr, amesema amefanya mazungumzo na uongozi wa klabu ya KMC FC, lakini bado hawajafikia muafaka.

“Wao walinifuata tukazungumza kiutendaji lakini hakukuwa na muafaka katika mazungumzo yetu. Kama tutamalizana vizuri taarifa zitatolewa tu na siyo jambo la kuficha,” alisema Matola.
Hata hivyo, kuonyesha kuwa uhusiano wake na Matola siyo mzuri, Stam alipoulizwa kuhusu Matola kukaribia kujiunga na timu hiyo, alisema:

“Sijaambiwa chochote kuhusu kumtaka Matola ingawa taarifa hizo ninazo, kuwa wanataka tusaidiane kuhakikisha tunaipandisha timu ligi kuu. Nafikiri hilo siyo jukumu lao ni jukumu la kocha mkuu, hivyo walikuwa na kila sababu ya kunifuata kuniuliza kuhusu mtu sahihi katika kusaidiana katika harakati hizi.

“Timu inafanya vema na dhamira yangu kuu ni kuipandisha ligi kuu, hivyo kama ni masuala haya, wanataka kutibua hali ya mambo. Mimi ndiye ninatakiwa kumtafuta msaidizi wangu na siyo mtu yeyote, maana mimi ndiye kocha mkuu,” alifunguka kocha huyo aliyewahi pia kuzifundisha Mwadui na Ndanda.

SIKIA KAULI YA NAHODHA HUYU...ZLATAN KIBURI, JEURI! ATANGAZA KULISTAAFISHA SOKA TAIFA LOTE LA DENMARK......


Nahodha wa Sweden, Zlatan Ibrahimovich amefunga moja kati ya mabao mawili yaliyoiwezesha Sweden kusonga mbele katika kuwania kucheza Kombe la Dunia baada ya kuing'oa Denmark.

Awali, Denmark walitamba kumstaafisha soka Zlatan, lakini baada ya sare ya 2-2, Sweden imesonga kwa jumla ya mabao 4-3 na Zlatan amesema: "Sasa taifa lao lote, nimelistaafisha soka."

Denmark na Sweden ni majirani ambao wana ushindani wa hali ya juu.

Denmark (4-2-3-1): Schmeichel 6.5; Jocobsen 6, Kjaer 5, Agger 6, Durmisi 5.5 (Vestergaard 83); Hojbjerg 6, Delaney 6.5 (Krohn-Dehli 45, 6); Poulsen 6.5, Eriksen 6, Jorgensen 6; Bendtner 5
Subs not used: Andersen, Wass, Kvist Jorgensen, Braithwaite, Christensen, Falk Jensen, Simon Poulsen, Jakob Poulsen, Rasmussen, Lossl.
Booked: Durmisi, Poulsen, Hojbjerg 
Sweden (4-4-2): Isaksson 6.5; Lustig 6.5, Johansson 6, Granqvist 5.5, Bengtsson 5 (Olsson 86); Larsson 6.5 (Hiljemark 81), Lewicki 6.5, Kallstrom 6 (Svensson 69), Forsberg 6; Berg 6, Ibrahimovic 8.5
Subs not used: Olsen, Helander, Guidetti, Kujovic, Milosevic, Toivonen, Durmaz, Zengin, Carlgren.
Booked: Bengtsson, Larsson 
Referee: Martin Atkinson (England) 6.5







KOCHA WA YANGA..PLUIJM ALIA CHALENJI KUHARIBU PROGRAMU NA KAMBI NZIMA.....


Yanga imeshindwa kuingia kambini kujiandaa na Ligi Kuu Bara kutokana na michuano ya Kombe la Chalenji iliyopangwa kuanza Novemba 20 jijini Addis Ababa, Ethiopia.


Yanga hivi sasa inaendelea na maandalizi ya ligi kuu chini ya Kocha Mkuu, Mholanzi, Hans van Der Pluijm na Juma Mwambusi wakati ligi hiyo ikisimama.

Pluijm amesema ni ngumu kuifuata programu aliyoipanga wakati ligi kuu ikisimama kutokana na nusu ya wachezaji kuwepo vikosi vya timu zao za taifa.

Pluijm alisema, katika ripoti yake aliomba mechi tano za kirafiki za kimataifa pamoja na kambi ya pamoja ya kujiandaa na ligi hiyo katika kuhakikisha wanautetea ubingwa wao.

“Timu inaendelea na mazoezi yake ya pamoja ikiwa na mchanganyiko wa wachezaji wa U20 baada ya nusu ya wachezaji wa timu kubwa kuwepo kwenye timu zao za taifa.

“Hivyo hivi sasa siwezi nikafanya chochote ikiwemo kucheza mechi za kirafiki za kimataifa, pamoja na kambi ya kujiandaa na ligi kuu iliyosimama hadi pale wachezaji wote watakaporejea kujiunga na wenzao,” alisema Pluijm.

Matokeo ya Mtanange kati ya Algeria Vs Taifa Stars November 17 2015........


Ronaldo anamuiba binti wa wakala wake …….

Cristiano Ronaldo kuingia katika headlines imekuwa kawaida sana kwake ukilinganisha na Lionel Messi ambaye amekuwa akitajwa kama mshindani wake mkubwa licha ya kuwa maisha binafsi wako tofauti sana kitabia za nje ya uwanja. Ronaldo amekuwa akihusishwa sana kuwa katika mahusiano na wapenzi wengi kwa nyakati tofauti tofauti.
2E89F8EC00000578-3322398-image-a-44_1447782766649
Ronaldo katika picha ya pamoja akiwa na wakala wake Jorges Mendes pamoja na Marisa Mendes wakati wa uzinduzi wa movie ya Ronaldo
Amewahi kuripotiwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi ya muda mfupi na Kim Kardashian lakini Paris Hilton amewahi kutoka na staa huyo, mrembo kutoka katika mchezo wa tennis Maria Sharapova na baadae Iryna Shayk ila headlines za November 17 zinazo muhusu staa huyo anatajwa kutoka kimapenzi na Marisa Mendes ambaye ni binti wa wakala wake Jorges Mendes.