Usiku wa November 17 watanzania wengi na
wapenzi wa soka walikuwa wakisubiri kuona mchezo wa pili wa marudiano
wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 Urusi kati ya timu ya taifa ya Algeria dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, mchezo ambao ulichezwa Blida Algeria katika uwanja wa Mustapha Tchaker.
Taifa Stars ambayo ilionesha kiwango kizuri katika uwanja wa nyumbani Dar Es Salaam
licha ya kulazimishwa sare ya goli 2-2, wameshindwa kutamba katika
mchezo wa pili na kukubali kipigo cha goli 7-0, ilichukua dakika 45 za
kwanza Taifa Stars kuanza kuruhusu magoli matatu ya mwanzo, magoli ambayo yalianza kukatisha tamaa wa Tanzania.
Wakati Taifa Stars wanatafakari namna ambavyo watasawazisha magoli Mudathir Yahaya alioneshwa kadi nyekundu dakika ya 41, kipindi cha pili kocha wa Tanzania Boniface Mkwasa alifanya mabadiliko ya kumuingiza Aishi Manula na kumtoa golikipa Aly Mustapha na Farid Mussa nafasi yake ikachuliwa na Salum Telela, mabadiliko ambayo hayakuzaa matunda.
Magoli ya Algeria yalifungwa na Yacine Brahimi dakika ya 1, Faouzi Ghoulam dakika ya 23 na dakika ya 59 akapachika goli jingine kwa mkwaju wa penati, Riyad Mahrez dakika ya 43 na Islam Slimani kafunga kwa mkwaju wa penati dakika ya 49 na 75, Carl Medjani dakika ya 72 . Kwa matokeo hayo Taifa Stars imetolewa kwa jumla ya magoli 9-2 baada ya mchezo wa awali kumalizika kwa sare ya goli 2-2.
No comments:
Post a Comment