Wednesday, November 18

MAKUBALIANO...IAEA yapongeza makubaliano ya nyuklia ya Iran....


IAEA yapongeza makubaliano ya nyuklia ya Iran
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA amepongeza kile alichokitaja kuwa ‘maendeleo mazuri’ kuhusu makubaliano ya nyuklia ya Iran katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. 
Akihutubia kongamano la 17 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapo jana mjini New York nchini Marekani, Yukiya Amano amesema makubaliano hayo yanadhihirisha kuwa masuala mazito ya kimataifa yanaweza kutatuliwa kwa njia za kidiplomasia. 
Amesema shirika hilo linajiandaa kuwasilisha ripoti ya mwisho ya uchunguzi wake kuhusu miradi ya nyukia ya Iran kufikia Disemba 15.
 Mkurugenzi Mkuu wa IAEA amepongeza juhudi za pande zote katika mazungumzo ya kufikiwa makubaliano ya nyuklia ya Iran, ikiwemo Tehran, kundi la 5+1 na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Itakumbukwa kuwa Iran na kundi la 5+1 zilifikia mapatano ya nyuklia huko Vienna, Austria mnamo Julai 14.


No comments: