Kitengo cha misaada
cha umoja wa mataifa kimetoa onyo juu ya suala la wakimbizi kutoka
Syria kwamba hawapaswi kupewa uhuru mkubwa kufuatia shambulio la mjini
Paris.
Baadhi ya taarifa zinasema kwamba mmoja wa washambuliaji wa Paris,aliingia Ulaya kama mkimbizi akitokea nchini Syria.Wanasiasa kadhaa kutoka umoja wa Ulaya wametoa wito wa kusitishwa kwa zoezi la kuwapokea wahamiaji wanaofurika kuingia katika nchi za umoja wa Ulaya,ambao huvuka bahari ya Atlantic ingawa mpaka sasa majimbo takribani kumi na mawili ya Marekani wamesha sitisha zoezi la kupokea wahamiaji wanaotoka nchini Syria.
Umoja wa mataifa unaamini kwamba uchunguzi yakinifu wa wakimbizi wanapowasili katika maeneo wanayotafuta hifadhi,na haki ya kugawana mzigo wa huduma za wahamiaji na wakimbizi,kutasaidi kuwatambua ikiwa kuna shaka yoyote ya kiusalama pindi viashiria vitakapo ng'amuliwa.
No comments:
Post a Comment