Wednesday, November 18

UN: Watoto laki 5 wakabiliwa na utapia mlo Yemen.......

UN: Watoto laki 5 wakabiliwa na utapia mlo YemenMfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF umesema watoto zaidi ya laki 5 nchini Yemen wanakabiliwa na hatari ya kupoteza maisha kutokana na utapia mlo.
Mkuu wa mfuko huo Anthony Lake ameeleza hofu yake ya kuongezeka idadi hiyo na kwamba hatua za dharura zisipochukuliwa, huenda tatizo hilo likageuka na kuwa mzigo kwa jamii ya kimataifa.
 Hii ni kati hali ambayo, Saudi Arabia inaendelea kuua raia wasio na hatia nchini Yemen huku ikipuuza miito ya kusitisha hujuma zake za kinyama dhidi ya nchi hiyo masikini ya Kiarabu.
Hivi karibuni Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu lililaani kuendelea mashambulio ya Saudi Arabia dhidi ya hospitali na vituo vya afya huko Yemen. 
Saudi Arabia na waitifaki wake tarehe 26 Machi mwaka huu walianzisha mashambulizi dhidi ya wananchi wa Yemen kwa kisingizio cha kuirejesha madarakani serikali iliyojiuzulu.
 Raia zaidi ya 7,200 wameuawa na wengine wengi kulazimika kuwa wakimbizi kutokana na mashambulizi hayo huku miundo mbinu ya nchi hiyo ikiharibiwa vibaya.

No comments: