The Nordic countries (Sweden, Norway, Denmark, Finland and Iceland) are key donors and partners of the United Nations system globally, regionally and at country level. In order to strengthen their collaboration with the United Nations in support of the Global Goals, and strategic development priorities of the Government of Tanzania, officials representing the five Nordic countries will be in the country during 14 -18 November, 2016.
Image copyrightAFPImage captionReince Priebus alionekana na Donald Trump usiku wa siku ya uchaguzi
Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, amemteua mwenyekiti wa kamati ya taifa ya chama cha Republican, Reince Priebus, kutumika kama mkuu wa wafanyakazi.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia, Igor Konashenkov amesema kuwa, shambulio lolote la kombora au la anga litakalolenga maeneo ya jeshi la serikali ya Syria, litakuwa linahatarisha majeshi ya Russia na Syria kwa pamoja.
Konashenkov ameitaka Marekani kuzingatia kwa umakini matokeo mabaya yatakayotokana na hatua yake ya kushambulia maeneo ya jeshi la Syria.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi nchini Russia, Igor Konashenkov.
Ameingeza kuwa, baada ya hujuma ya anga iliyofanywa na ndege za kivita za Marekani tarehe 17 Septemba dhidi ya jeshi la Syria, Moscow ilichukua hatua za lazima za kuzuia kujikariri tukio kama hilo dhidi ya jeshi lake nchini Syria.
Muwania urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican, Marco Rubio
amemshambulia mwenzake Donald Trump kwa kusema kuwa Uislam unaichukia
Marekani, katika mdahalo uliorushwa kwenye televisheni huko Miami.
Mgombea
wa Democratic Hillary Clinton na mgombea wa Republican Donald Trump
wamechukua uongozi wa mapema katika mchujo wa kuteua wagombea urais
Marekani katika vyama vyao.
Huenda ukawa umezoea na kuboreka na foleni ya jiji la Dar Es Salaam ambalo wakati mwingine inaweza kukugharimu kwa zaidi ya saa moja kukaa katika foleni kutoka Tegeta hadi Posta, hususani mvua ikiwa inanyesha Dar Es Salaam sehemu huwa zinakuwa na foleni kubwa. Mtu wangu wa nguvu nimekutana na list ya mpya kutoka www.telegraph.co.ukya miji 10 inayoongoza kwa foleni Duniani, imeandikwa 04/02/2016.
Mwigizaji filamu wa Mexico Kate del Castillo anahojiwa kuhusiana na sakata inayomhusu mmoja wapo wa walanguzi wakuu wa dawa za kulevya Joaquin "El Chapo" Guzman ambaye sasa anatumikia kifungo gerezani.
Watu binafsi hawataruhusiwa tena kuweka matangazo ya kuuza bunduki katika Facebook na Instagram, kampuni ya Facebook ambayo pia inamiliki Instagram imetangaza.
Tai mkubwa aliyezuiliwa nchini Lebanon akituhumiwa kuwa jasusi wa Israel ameachiliwa huru baada ya walinda usalama wa Umoja wa Mataifa kuingilia kati, maafisa wa Israel wamesema.
Inaweza kutokea unasafiri kwenye gari hivi labda toka Dar mpaka Morogoro
kwenye basi la abiria peke yako, unaweza kujifariji kwa kuchekicheki nje
mazingira, ukachezea simu yako au ukaendelea zako na safari kwa
kusikiliza muziki au kuangalia TV kwenye basi, lakini vipi kwenye ndege
inakuwaje?
Jamaa mmoja Alex Simon mtalii kutoka Austria,
alijikuta kwenye level za kistaa hivi au mtu fulani VIP kwenye ubora
wake baada ya kujikuta akiwa ndio abiria pekeake ndani ya ndege ya
abiria zaidi ya 100… alitoka zake Manila kwenda Boracay ndani ya Ufilipino kwa ajili ya kutalii tu !!
Baada ya Simon
kuingia kwenye ndege alianza kupiga stori na marubani baadae akaungana
na wahudumu wawili wa ndege wakiendelea na stori mpaka alipotua
Cheki Video ya jamaa mwenyewe hii hapa mwanzo mpaka mwisho wa safari.
Rais wa Afrika
Kusini Jacob Zuma amemteua waziri mwingine wa fedha katika kipindi cha
siku nne, baada ya uteuzi wa awali kupingwa vikali.
Bw Zuma alikuwa amemfuta kazi Nhlanhla Nene wiki iliyopita na kumteua Desmond Van Rooyen kuwa waziri mpya. Hatua hiyo ilipingwa vikali na watu huku masoko yakidorora na thamani ya sarafu ya Rand ikishuka pakubwa. Uteuzi huo pia ulishutumiwa kupitia mitandao ya kijamii, kitambulisha mada #Zumamustfall kikivuma sana Afrika Kusini. Kutokana na hayo, Rais Zuma ameamua kubadilisha uamuzi wake na kumteua Pravin Gordon ambaye amewahi kuwa waziri wa fedha. Bw
Gordon ndiye aliyemtangulia Bw Nene katika Hazina Kuu na alisaidia
kuongoza taifa hilo kupitia msukosuko wa kudorora kwa uchumi 2009.
Mwandishi wa BBC aliyeko Johannesburg Matthew Davies
anasema sarafu ya Rand ilianza kuimarika Jumapili na bei ya hisa katika
Soko la Hisa la Johannesburg inatarajiwa kuanza kupanda tena wiki hii. Hata
hivyo, hali ya Bw Zuma kuonekana kutokuwa na msimamo itaathiri sana
chama tawala cha ANC huku taifa hilo likijiandaa kwa uchaguz wa serikali
za mitaa mwaka ujao.
Rais wa Afrika
Kusini Jacob Zuma amemteua waziri mwingine wa fedha katika kipindi cha
siku nne, baada ya uteuzi wa awali kupingwa vikali.
Bw Zuma alikuwa amemfuta kazi Nhlanhla Nene wiki iliyopita na kumteua Desmond Van Rooyen kuwa waziri mpya. Hatua hiyo ilipingwa vikali na watu huku masoko yakidorora na thamani ya sarafu ya Rand ikishuka pakubwa. Uteuzi huo pia ulishutumiwa kupitia mitandao ya kijamii, kitambulisha mada #Zumamustfall kikivuma sana Afrika Kusini. Kutokana na hayo, Rais Zuma ameamua kubadilisha uamuzi wake na kumteua Pravin Gordon ambaye amewahi kuwa waziri wa fedha. Bw
Gordon ndiye aliyemtangulia Bw Nene katika Hazina Kuu na alisaidia
kuongoza taifa hilo kupitia msukosuko wa kudorora kwa uchumi 2009.
Mwandishi wa BBC aliyeko Johannesburg Matthew Davies
anasema sarafu ya Rand ilianza kuimarika Jumapili na bei ya hisa katika
Soko la Hisa la Johannesburg inatarajiwa kuanza kupanda tena wiki hii. Hata
hivyo, hali ya Bw Zuma kuonekana kutokuwa na msimamo itaathiri sana
chama tawala cha ANC huku taifa hilo likijiandaa kwa uchaguz wa serikali
za mitaa mwaka ujao.
Mahakama ya
Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) iliyokuwa ikishughulikia
kesi za mauaji yaliyotokea miaka 20 iliyopita leo itatoa hukumu yake ya
mwisho kabla ya kufungwa kabisa.
Hukumu hiyo itakuwa dhidi ya
watuhumiwa Pauline Nyiramasu ambaye ni waziri wa zamani wa Maendeleo ya
wanawake nchini Rwanda na mtoto wake ambaye wote wamekana mashtaka
yanayowakabili. Mahakama hiyo ambayo imekuwako Kaskazini mwa
Tanzania katika mji wa Arusha ilikuwa ikisikiliza kesi za watuhumiwa wa
mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994. Mara kadhaa waendesha mashtaka wa mahakama hiyo walikabiliwa na mashahidi waliokuwa tayari kutoa ushahidi. Hata hivyo mafanikio yake yamepongezwa na watu wengi ambao wamesema si rahisi kuwatafuta na kushtaki watuhumiwa wote.
Serikali ya
Marekani imeshauri Raia wake walio nchini Burundi kuondoka nchini humo
haraka iwezekanavyo baada ya watu 87 kuuawa kwenye ghasia zilizotokea
siku ya Ijumaa.
Ghasia zilizojitokeza kwenye mitaa ya mji mkuu wa
nchi hiyo, Bujumbura ni mbaya zaidi tangu kuanza kwa vurugu mwezi Aprili
baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuamua kuwania tena urais kwa muhula wa
tatu. Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch (HRW) limeitisha uchunguzi kuhusu mauaji hayo ya Ijumaa. Mwezi
uliopita, Ubelgiji pia iliwashauri raia wake kuondoka Burundi, huku
Muungano wa Ulaya (EU) nao ukipunguza wahudumu wake, kwa kuondoa
wafanyakazi ambao ni wa muda, "familia na wafanyakazi ambao si muhimu
sana." "Kufuatia machafuko ambayo yanaendelea kuongezeka, Wizara
ya Kigeni meagiza kuondoka kwa jamaa za maafisa wa Marekani na maafisa
ambao si wa kushughulikia dharura nchini Burundi," taarifa ya Marekani
ilisema. "Ubalozi wa Marekani unaweza kutoa huduma za dharura kwa kiwango cha chini tu kwa raia wake nchini Burundi." Jijini
Nairobi, wanaharakati Jumapili jioni waliwakusanya vijana kutoka
Burundi, Kenya na nchi nyingine za Afrika Mashariki jijini Nairobi kwa
ajili ya mkesha na kuwasha mishumaa kuwakumbuka Raia wa Burundi
walioathirika kutokana na mzozo wa kisiasa nchini mwao. Aidha, walitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati.
Mazungumzo kuhusu
Mabadiliko ya tabia nchi yanaanza rasmi asubuhi ya leo huko jijini Paris
nchini ufaransa, wakuu wa nchi zaidi ya mia na hamsini wanatarajiwa
kuhudhuria mkutano huo uliondaliwa na umoja wa mataifa.
Maandamano
yamefanayika duniani kote kushinikiza kuchukuliwa hatua kupambana na
ongezeko la joto duniani, jijini Paris Polisi walilazimika kutumia gesi
ya kutoa machozi kuwasambaratisha waandamanaji huku watu mia moja
wakishikiliwa kwa kosa la kukiuka amri ya kutofanya maandamano
iliyotolewa baada ya mashambulizi jijini humo. Akifungua mkutano
huo, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius, alisema ana
uhakika kuwa mazungumzo hayo yatawafikisha kwenye hatua ya makubaliano
chanya. Wakati huo huo rais Obama amezuru kituo cha burudani cha
Bataclan mjini Paris kutoa heshima zake kwa waathiriwa na shambulio la
kigaidi wiki mbili zilizopita. Obama na rais wa nchi hiyo, Francois
Hollande waliweka shada la maua kwenye ukumbi huo, ambako watu tisini
waliuawa na wanamgambo wa Kiislamu waliokuwa wamejihami kwa bunduki.
Wakati vikao vya siri vya kutafuta suluhu ya mzozo wa kisiasa visiwani
Zanzibar vikiwa vimeripotiwa, juhudi za kuupatia ufumbuzi mzozo huo
zimehamia kutoka Ikulu ya Zanzibar na kufika Ikulu ya Marekani (White
House).
Wanachama wa ZADIA kutoka majimbo tafauti Nchini Marekani wakionyesha mabango yao.
Mnamo tarehe 21 mwezi huu, Wazanzibari waishio nchini Marekani
waliandamana hadi kwenye Ikulu ya nchi hiyo katika juhudi za kutafuta
uingiliaji kati wa kimataifa ili kuupatia suluhisho mzozo huo.
Akizungumza na waandishi wa habari mbele ya Ikulu hiyo, Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) iliyoandaa
maandamano hayo Bwana Omar Haji Ali, alisema kuwa maandamano hayo
yanakuja katika juhudi za Jumuiya hiyo za kutafuta uingiliaji kati wa
kimataifa katika kuukwamua mgando wa kisisas visiwani Zanzibar.
Aliendelea kusema kwamba maandamno hayo pia yana lengo la kumkumbusha
rais Barack Obama wa Marekani kutekeleza ahadi yake ya kuilinda
demokrasia Barani Afrika.
"Katika
hotuba yake aliyoitoa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika mapema
mwaka huu, rais Obama alisema '.. pale ambapo raia hawawezi kutekeleza
haki zao, basi ulimwengu una jukumu la kukemea. Na Marekani itafanya
hivyo, hata kama wakati mwengine itakuwa inauma'..", alikumbusha Bwana
Ali.
Aliongeza kuwa "Wananchi wa Zanzibar wameshindwa
kutekeleza haki yao kwa zaidi ya nusu karne sasa. Wakati umefika sasa
kwa ulimwengu kuchukua jukumu lake. Wakati umefika sasa kwa Marekani
siyo tu kukemea, lakini pia kuchukua hatua za kivitendo ili kuhakikisha
kuwa sauti za Wazanzibari zinasikilizwa na kuheshimiwa"
Alipoulizwa ni hatua gani watakazochukuwa iwapo Serikali ya Marekani
haikuchukua hatua yoyote kusaidia kumaliza mgando wa kisiasa Zanzibar,
Bwana Ali alisema "Tuna imani na rais Obama, na tumemfikishia barua ya
malalamiko yetu, na tunasubiri jibu lake, na imani yetu ni kuwa
atachukua hatua madhubuti khususan ikizingatiwa kuwa Ubalozi wa Marekani
nchini Tanzania ulikuwa wa mwanzo kutoa taarifa kuelezea kuwa uchaguzi
wa Zanzibar ulikuwa wa haki na huru" Alidokeza kuwa, iwapo hali
itaendelea kubakia kama ilivyo, basi ZADIA itaelekea kwnye Umoja wa
Mataifa.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) Bwana Omar Haji, akiongea na moja waandishi wa habari.
Katika maandamano hayo yaliyowashirikisha pia wapenda amani na
demokrasia kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni, waandamanaji walibeba
mabango yaliyokuwa na maneno kama vile "Mshindi wa uchaguzi atangazwe",
"maamuzi ya Wazanzibari yaheshimiwe", "bila haki hakuna amani' na
mengineyo.
Akizungumza na Swahilivilla, raia mmoja wa Marekani aliyeshiriki kwenye
maandamano hayo alisema "Nilimpeleka mwanangu kwenda kusoma kule, bado
ana mapenzi na Zanzibar, na amenisimulia habari nzuri za amani, utulivu
na ukarimu wa watu wake. Amekuwa akifuatilia hali ilivyo, na kwa hamasa
kubwa alipopata habari za maandamano haya, akaniomba tuje kuwaunga mkono
Wazanzibari katika kudai haki yao"
Itakumbukwa kuwa,
wananchi wa Zanzibar walipiga kura mnamo tarehe 25 Oktoba mwaka huu,
lakini Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Bwana Jecha Salum
Jecha akatangaza kufutwa kwa uchaguzi huo Mkuu visiwani humo, kitendo
ambacho wataalamu wa Sheria wamesema kuwa kinakwenda kinyume na Katiba
ya Zanzibar.
Wachambuzi wanaona kuwa hatua hiyo ya Bwana Jecha
ilikuja wakati asilimia kubwa ya matokeo yaliyokuwa yametangazwa
yalikuwa yanampa ushindi mgombea wa urais wa Zanzibar kutoka chama cha
upinzani cha Wananchi (CUF) Maliim Seif Shariff Hamad.
Kitendo
cha kufutwa kwa uchaguzi huo ambao wachunguzi wa nje na ndani
waliulezea kuwa ulikuwa wa haki na huru, kimezua mtafaruku wa kisiasa
visiwani Zanzibar, na juhudi za ndani na nje zimekuwa zikifanyika ili
kumaliza mgogoro wa kisiasa visiwani humo.
Maandamano ya ZADIA ni katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kimataifa za kusaka suluhu za mgogoro huo kwa njia za amani.
Mpenda amani na Demokrasia Lodi Mohamed akiongea na muandishi wa habari Njee ya Ikulu ya Marekani (White House)
Waziri
mwenye ushawishi mkubwa katika serikali ya Rais Uhuru Kenyatta
amejiuzulu wadhifa wake baada ya shinikizo kutolewa ajiuzulu kutokana na
tuhuma za ufisadi.
Bi Anne Waiguru, ambaye amekuwa Waziri wa Mipango na Ugatuzi,
amewaambia wanahabari Nairobi kwamba ameshauriwa na daktari wake
“achukue muda kupumzika”. Amewaambia wanahabari kwamba amemwandikia Rais Kenyatta akimtaka amuondolee majukumu yake. Wakenya wapigania waziri kwenye Twitter Hata hivyo amesisitiza kwamba hana hatia.
“Ninafuata ushauri wa daktari na nimemuomba Rais aniondolee majukumu
yangu kama waziri ... na akiona inafaa, anipe majukumu ambayo si
mazito,” Bi Waiguru amesema.