Monday, April 4

SHINIKIZO LA KIMATAIFA KUHUSU ZANZIBAR BADO LINAINYEMELEA TANZANIA


Siku chache baada ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), kufuta Tanzania kwenye nchi wanachama wake na hivyo kuikosesha serikali msaada wa zaidi ya Sh. trilioni moja kutokana na uchaguzi wa Zanzibar, Umoja wa Ulaya (EU), upo hatarini kutotoa Sh. trilioni 1.56 kwa sababu ya suala hilo huku mmoja wa Waziri wa Uingereza, akiitaka serikali yake isitoe Sh. bilioni 622 za msaada kwa Tanzania.

KAMATI YA MISS TANZANIA YAZINDUA MSIMU MPYA WA MASHINDANO YA MISS TANZANIA 2016 JIJINI ARUSHA

Hashim Lundenga
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) akimiminiwa kinywaji cha K-Vant wakati wakiingia na wadau wa tasnia ya urembo kwenye ukumbi wa Triple A jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 uliofanyika mwishoni mwa juma.

ANASWA AKISAFIRISHA SMG NDANI YA BASI LA ABIRIA MOROGORO


Polisi  mkoani Morogoro inamshikilia Juma George (29) mkazi wa Shinyanga, kwa kukutwa na silaha ya kivita aina ya SMG iliyofutwa namba zake za usajili, magazini mbili, risasi 21 pamoja na panga vikiwa vimehifadhiwa ndani ya begi lake la nguo.

CUF KUTOA MSIMAMO WAO LEO KUHUSU HALI YA ZANZIBAR

Chama kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar leo kinatarajiwa kutangaza mikakati yake na msimamo kuhusiana na mzozo wa kisiasa wa Zanzibar.
Hata hivyo msimamo huo unatarajiwa kuzungumzia mufaka katika ya chama cha CUF na CCM ambao ulileta uundwaji wa serikali kati ya vyama hivyo viwili.
Chama cha CUF visiwani Zanzibar bado kinaendeleza msimamo wake kususia kutambua matokeo na serikali iliyoundwa kufuatia uchaguzi wa marudio.
Hivi karibuni shirika la misaada la Marekani MCC lilisitisha msaada wa dola 487 kwa madai ya kutoridhishwa na hali ya kisiasa visiwani Zanzibar.

DKT. KIGWANGALLA AFUNGUA OFISI MPYA ZA SHIRIKA LA T-MARC TANZANIA.

1T
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla Charles Singili Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la T. Marc Tanzania pamoja na Diana Kisaka Mkurugenzi wa Shirika la T.Marc Tanzania wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa ofisi za shirika hilo zilizoko Kunduchi jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki , Shirika hilo linajihusisha na shughuli mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu katika masuala ya ukimwi, Malaria na Elimu ya Uzazi.

WAJASIRIAMALI DAR WAJAZWA MADINI KUHUSU FURSA MPYA KATIKA KILIMO BIASHARA

Margareth Nzuki - ESRF
Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Bi. Margareth Nzuki akiwasilisha malengo ya warsha kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida kufungua warsha hiyo.