Showing posts with label BURUDANI. Show all posts
Showing posts with label BURUDANI. Show all posts

Monday, April 4

KAMATI YA MISS TANZANIA YAZINDUA MSIMU MPYA WA MASHINDANO YA MISS TANZANIA 2016 JIJINI ARUSHA

Hashim Lundenga
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) akimiminiwa kinywaji cha K-Vant wakati wakiingia na wadau wa tasnia ya urembo kwenye ukumbi wa Triple A jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 uliofanyika mwishoni mwa juma.

Saturday, April 2

WAZIRI NAPE AFANYA MKUTANO NA WASAMBAZAJI WA FILAMU NA MUZIKI NCHINI LEO

ep1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiongea na wasambazaji wa filamu na muziki nchini wakati wa mkutano kati yake na wasambazaji hao uliojadili namna gani ya kuboresha tasnia hiyo kwa manufaa ya wasanii, wasambazaji na uchumi wa Taifa.(Picha Na Benjamin Sawe- WHUSM)

Wednesday, March 9

HII NDIO KOLABO YA CHEMICAL NA FID Q PAMOJA NA CLIFF MITINDO



Mwanadada Chemical afanya collabo na Fid Q na Cliff Mitindo 
Rapper Chemical amesema baada ya kusimama mwenyewe sasa ni muda wa kufanya collabo.

Thursday, March 3

HAYA NDIO MAJIBU YA BELLE 9 KWA DIAMOND NA WATANZANIA BAADA YA MATUSI MTANDAONI

 
Ni masaa machachetu tangu kusambaa kwa ujumbe ulioandikwa kupitia Instagram account ya staa wa bongo fleva Belle 9 ikionyesha kumdiss staa mwenzake bongoflevani Diamond Platnumz, 

Tuesday, March 1

DUDUBAYA AWAITA KENGE AWA JAMAA......


dudu-baya
Dudubaya amewajia juu baadhi ya majirani zake na Watu wengine waliosema amefulia na amekuwa akishinda maskani muda wote kuvuta bangi.

Tuesday, February 16

MSAADA...BONDIA MANNY PACQUIAO AKABIDHI NYUMBA KWA FAMILIA MASIKINI..


 Mwana masumbwi maarufu Duniani toka nchini Phillipines Emmanuel Dapidran Pacquiao (37) maarufu kama "Manny Pacquiao" amekabidhi nyumba kwa wananchi wa jimbo lake kwa ajlili ya makazi ya familia masikini zipatazo 1,000...

Akieleza wakati wa makabidhiano ya nyumba hizo kwa wananchi hao Pacquiao alisema, amejenga nyumba hizo kwa fedha ambazo amekuwa akizipata kutokana na malipo ya Ubunge na mchezo ya ngumi ambao unamuingizia pesa kibao.

Nyumba zenyewe ni hizo kama zinavyoonekana kwenye picha..

Thursday, December 17

Hawa Ndo Top 5........Wajue wasanii watano wenye ushawishi mkubwa Africa kwa mwaka 2015… Mtanzania yupo mmoja tu!...


Nimekutana na jarida la New African Magazine toleo ya December 2015 na ndani ya jarida hilo nikakutana na list ya watu waliotajwa kama watu wenye ushawishi mkubwa zaidi Africa kwa mwaka huu wa 2015… kwa upande wa burudani nimekutana na mastaa watano huku Mtanzania akiwemo mmoja tu!
AAAAA
Hawa ndio Africa Most Influencial Africans in Media, Arts & Culture waliotajwa na jarida la New African Magazine:
Lupita Nyong’o – Kenya.
Baada ya kushinda tuzo yake ya kwanza ya Oscars ya Best Supporting Role kwenye filamu yake ya kwanza kubwa, Two Years A Slave, staa wa movie Lupita Nyong’o kutoka Kenya amezidi kuonyesha uwezo wake kwenye industry ya filamu Marekani kwa kuzidi kupokea nafasi nyingi kubwa za kuigiza pamoja na kushinda tuzo kadhaa kwenye majukwa mbalimbali Marekani. Licha ya hayo Lupita pia ni Balozi wa Wild Elephants na Mwanaharakati wa haki za Wanyama.
African1
Lupita Nyong’o.
Trevor Noah – South Africa.
Mchekeshaji kutoka South Africa, Trevor Noah aliiteka  dunia baada ya Marekani kumtangaza kuwa mtangazaji mpya atakayerithi kiti cha show ya comedy, The Daily Show nchini Marekani. Toka ujio wa Trevor Noah kwenye kipindi hicho watazamaji wa show hiyo kutoka Marekani wametokea kuvutiwa na mchekeshaji huyo ambaye material yake kubwa ya comedy inaongelea sehemu kubwa ya maisha ya Kiafrika. Kwa mujibu wa ripoti kadhaa zilizotolewa na mitandao tofauti Marekani, ujio wa Trevor Noah kwenye kipindi hicho kumeongeza watazamaji milion 1.5 kwenye show hiyo.
African2
Trevor Noah.
Diamond Platnumz – Tanzania.
Staa wa muziki wa Bongo Fleva na mshindi wa tuzo ya MTV Africa Music Awards 2015: Best Live Act pamoja na MTV EMA 2015: Best African Act, Diamond Platnumz kwa mwaka huu ametajwa kama mmoja wa wasanii wa kubwa wa Africa kwa mwaka 2015 akiwa na ushawishi mkubwa ndani na nje ya Africa, akiwa pia na mashabiki wakubwa na wanaomuongelea zaidi kwenye mitandao ya kijamii kitendo kinachomfanya Diamond kuwa msanii kijana mwenye ushawishi mkubwa kwa mwaka huu wa 2015.
african3
Diamond Platnumz.
Yemi Alade – Nigeria
Baada ya hit song yake ya ‘Johnny’ kuweka headlines sehemu mbalimbali Africa staa wa muziki kutoka Nigeria, Yemi Alade alijipatia umaarufu mkubwa sana kupitia video hiyo ambayo ushawishi wake umegusa watazamaji zaidi ya milion 30 kweye mtandao wa YouTUBE. Ukiachia hayo style yake ya muziki pamoja na mavazi yake imetokea kuvutia wasichana wengi wanaofuatilia muziki wake.
African4
Yemi Alade.
Koffi Olomide – DRC Congo.
Mkongwe wa muziki kutoka Congo, Koffi Olomide amekuwa akijulikana kwenye industry ya muziki kuanzia miaka ya 1970 na bado umaarufu wake unagusa watu wengi wa rika zote duniani. Mwezi October mwaka huu 2015, Koffi aliachia album yake ya 13 na ya mwisho ikiwa na nyimbo 39. Licha ya kuachia Album yake ya mwisho Koffi anahesabika kama miongoni ya watu waliobadilisha sura ya muziki nchini Congo.
Africa5
Koffi Olomide.

ETI NAYEE NI MUUZA UNGA....Kesi ya kukutwa na dawa za kulevya ya Nelly yafutwa...


nelly
Kesi ya kukutwa na dawa za kulevya iliyomkabili rapa Nelly imefutwa. Nelly ametoa tamko juu ya swala hili na kusema
“Namshukuru wakili wangu Scott Rosenblum na watu wa mji wa Tennessee kwa kuwa na haki juu yangu”
Nelly alikamatwa Tennessee mwezi wa nne na polisi wa usalama barabarani na kukutwa na aina ya paraphernalia,marijuana na mfuko mwingine wenye methamphetamine ambao baada ya vipimo iligundulika kuwa haikuwa dawa ya methamphetamine.
Nelly alifikishwa mahakamani na kukubali kosa la kukutwa na dawa hizo na alipewa adhabu ya kifungo cha nje cha mwaka mzima.

Tuesday, December 8

AHADI NI DENI......Duu!! mwanamitindo katimiza ahadi yake ya kuvua nguo baada ya Palmeiras kutwaa Ubingwa …


Stori za Brazil kufanya vizuri katika soka zimekuwa kawaida sana ila siku hizi hii ni mpya kutoka kwa mashabiki wao, inashangaza kidogo, tumewahi kusikia Mrisho Ngassa akiahidi kama atashindwa kufunga goli katika mechi Yanga dhidi ya Simba atachoma moto nyumba zake tano ahadi ambayo alifanikiwa kuitimiza kwa kufunga goli.
mg_4491
Cintia Vallentim
Ila kwa mashabiki wa kike wa Brazil wameingia katika headlines hii mtu wangu, wiki iliyopita mwigizaji wa Brazil Maite Proenca mwenye miaka 57 aliahidi kama timu yake ya Botafogo itashinda na kufuzu kucheza Ligi daraja la kwanza Brazil atavua nguo, December 8 ni headlines za mwanamitindo wa kibrazil Cintia Vallentim mbaye nae aliahidi ahadi kama hiyo kama timu yake ya Palmeiras itatwaa Ubingwa wa Brazil.
mg_4341
Cintia Vallentim ametimiza ahadi hiyo ya kupiga picha akiwa mtupu baada ya timu yake ya Palmeiras kuifunga Santos kwa mikwaju ya penati na kushinda Kombe la Brazil. Tukio hili linakuja ikiwa ni wiki moja imepita toka muigizaji Maite Proenca kufanya kama hivyo ila yeye ni baada ya Botafogo kushinda na kupanda daraja la kwanza.
maite_1
Maite Proenca

Sunday, December 6

KIDUME NDANI.... Kim Kardashian na Kanye West waongeza furaha ndani ya familia yao…

Ni habari njema kwa familia ya Rapper wa Marekani Kanye West na mke wake Kim Kardashian!!.
Baada ya safari ndefu ya ujauzito wa staa huyo wa kipindi cha televisheni cha ‘Keeping Up with the Kardashians’ ambayo ilichukua headlines katika vyombo mbalimbali vya habari duniani hatimaye familia ya mastaa hao imejaliwa mtoto wa pili wa kiume jana Desemba 5.
Mtoto huyo ambaye mpaka sasa hajapewa jina anakuwa ni mdogo wa mtoto wao wa kwanza aitwaye North West.

Tuesday, November 24

USINDI SURA MBAYA...SHINDANO LA SURA MBAYA ZIMBABWE LAMALIZIKA KWA GHASIA.....

Ghasia zimeibuka baada ya mwanaume mwenye umri wa miaka 42 kutangazwa kuwa mshindi katika shindano la mtu mwenye sura mbaya Jijini Harare nchini Zimbabwe, huku mashabiki wakiwatuhumu majaji kwa upendeleo.

Majaji hao walimchagua, Mison Sere, kuwa mshindi kutokana na kutokuwa na meno mengi na kuwa na uwezo wa kuibadilisha sura yake kwa kuikunja kunja, na kumshinda bingwa mtetezi William Masvinu, ambaye amekuwa bingwa tangu mwaka 2012.

Mshindi wa shindano la mwanaume mwenye sura mbaya nchini Zimbabwe, huibuka na zawadi ya dola 500, ambayo ni fedha nyingi ukizingatia wengi wa washiriki wa shindano hilo huwa hawana ajira maalum.
                                      Washiriki wa sura mbaya wakiwa katika mapozi tofauti 
                    Mshindi wa shindano la sura mbaya Mison Sere akiwa amebebwa juu

Mfaham Huyu Hapa...Msanii wa bongofleva aliethibitisha kupata Zero kwenye mtihani wa Form IV...


MziwandaNATIONHuwa ni mara chache sana utasikia staa au mtu maarufu kajitokeza au kakubali kuweka wazi kuhusu sehemu aliyowahi kuharibu au kufeli kwenye maisha.
Kwenye muziki wa bongofleva tunae Nuh Mziwanda ambaye pia ni boyfriend wa msanii Shilole…… Nuh ameongea ukweli wa moyoni kwenye exclusive interview na millardayo.com na kusema >>> ‘Kwenye maisha yangu ninachojutia ni nilivyofeli mtihani wangu wa form IV nilipata Zero kabisa na sikufanya mitihani kama mitatu, yote hiyo ilitokea sababu ya muziki’
‘Nilikua mtoto mwenye akili sana na Mama yangu alikua anategemea nitakuja kuwa mtu flani mwenye elimu yake kwenye familia yetu na sio Mwanamuziki, nyumbani kwetu tuko watano na mimi ndio wa mwisho na nilikua nina akili sana kuliko wote na kuanzia la kwanza mpaka la saba nilikua sishuki kwenye Wanafunzi kumi bora‘ – Nuh
mziwandanation4Kwenye sentensi nyingine Nuh anamalizia >>> ‘Kupata Zero Form IV ni jambo ambalo linanifanya nijute sana mpaka sasa, ningekaza ningekua nafanya muziki huku nikisoma lakini nilivyojua maswala ya muziki tu nikaachana na Masomo, najutia…. nilikuja nikarudia tena mitihani na nikafeli, inaniuma sana… kama ninavyokosea kiingereza sio kwamba napenda, ni shule hamna’
Nuh amesema kuna uwezekano wa kurudi shule >>> ‘shule ni kitu muhimu haikataliwi, ni kitu poa unakuwa Mwanamuziki alafu una elimu yako… na muziki naudai sana ndio maana naukazania sababu ulinifanya nifeli shule’

Friday, November 20

Akon+Mshindi wa Airtel Trace...Mayunga Kawasili Universal Studios Marekani tayari kurekodi wimbo na Akon...


Mayungaa Narimi ambaye ni mshindi wa shindano kubwa la vipaji la Airtel Trace Music Staramefika kwa mara ya kwanza kwenye Ofici za lebel kubwa ya muziki ya Universal Studios mjini HollyWood nchini Marekani.
Hizi ni baadhi ya picha alizotuonyesha Mayunga na ujumbe huu
“There we are 😉💃💃💃💃 for the first time in UNIVERSAL STUDIOS. …. HOLLYWOOD oow 🙏 thank you ALLAH,thanks @Airtel Trace music star, thanks beautiful people……( you know what! Dont let anyone stop yo dreams because i had a dream that one day i would love to be in UNIVERSAL STUDIOS. ..HOLLYWOOD oow can’t even explain it more because it’s more than happiness , what i can say is just join me on this trip so that we can share somethings i love u guys☺. (Kwa mara ya kwanza ndani ya UNIVERSAL STUDIOS… HOLLYWOOD OOW asante sana mungu sante sana @Airtel Trace music star pia asante sans watu wangu wa zuri.Unajuwa nini usiache mtu yeyote akusimamishie ndoto zako kwa sababu nilikuwa na ndoto kwamba sikumoja ningependa kuwa UNIVERSAL STUDIOS. .HOLLYWOOD OOW siwezi hata kuelezea sana kwani ni zaidi ya furaha, ninachoweza sema ni kwamba ungana nami katika hii safari ili tu weze ku shea baadhi ya vitu nawapenda sana sante.😊. ”
mayunga 2
mayunga 2 (2)

Je Unataka Kujua?!!>>>Kuna chochote kati ya Future na Blac Chyna? Majibu yote yapo kwenye ‘Rich $ex’ – (Video)!....


Ni FurahiDay na rapper kutoka Freebandz, Future anaziandika headlines za leo kwenye kurasa za burudani kwa kuisogeza single nyingine kutoka kwenye mixtape yake ya Dirty Sprite 2 (DS2).
Wimbo unaitwa ”Rich $ex” na video yake ipo hewani tayari lakini video queen kwenye hii ngoma mpya ni model na dancer, Blac Chyna staa ambaye wiki chache zilizopita aliweka headlines nyingi kwenye social media baada ya kuchora tattoo ya jina la rapper huyo mkonini mwake… ikasemekana ni wapenzi lakini Future akakanusha taarifa hizo!
chynafut2
Je ni kweli kuwa Future na Blac Chyna sio wapenzi? majibu yote yanaweza kupatikana kwenye video hiyo...

MKALI WA ACTION MOVIE....Pichaz 8 za mkali wa movie kutoka Hollywood Van Damme alivyotembelea mazoezi ya Man City.....


Staa wa movie kutoka Hollywood Jean-Claude Van Damme mkali ambaye amewahi kutamba na movie kadhaa November 19 alipata nafasi ya kutembelea mazoezi ya klabu ya Manchester City. Staa huyo wa Hollywood yupo jijini Manchester kwa ajili ya shughuli ya ‘black-tie dinner’ ambapo atapata nafasi ya kuoneshwa kwa movie zake.
2E9B924D00000578-3325905-image-a-23_1447960227983
Jean-Claude Van Damme na Vincent Kompany
Jean-Claude Van Damme ambaye ana umri wa miaka 55 alivyotembelea mazoezi ya Man City mastaa wa klabu hiyo hawakuacha kuchukua kumbukumbu zao kwa kupiga picha na staa huyo, wachezaji wa Man City kama Yaya Toure, Vincent Kompany, Kevin De Bruyne, Sergio Aguero pamoja na kocha wao Manuel Pellegrini hawakusita kupiga picha na Van Damme.
2E9B927C00000578-3325905-The_80s_action_movie_hero_poses_for_a_picture_with_Belgian_compa-m-11_1447959922108
Jean-Claude Van Damme na Vincent Kompany
Mkali huyo wa movie duniani ambaye kwa miaka ya karibuni ametamba katika tangazo la bia, amewahi kutamba katika movie za mapigano zikiwemo Bloodsport, Hard Target na Universal Soldier. Hizi ni baadhi ya pichaz zake alivyotembelea Man City.
2E9B970600000578-3325905-image-a-21_1447960121031
2E9B945600000578-3325905-image-a-20_1447960070642
Jean-Claude Van Damme na golikipa wa Man City Joe Hart
2E9B971E00000578-3325905-image-a-5_1447959538287
Sergio Aguero na Jean-Claude Van Damme
2E9B934600000578-3325905-image-a-8_1447959792555
Jean-Claude Van Damme Kevin De Bruyne
2E9B977000000578-3325905-image-a-10_1447959881627
Kocha wa Man City Manuel Pellegrini akiwa na Jean-Claude Van Damme
0064DDFD00000258-3325905-image-a-17_1447960042452
Universal Soldier hii ni movie aliyotamba nayo miaka ya 1990 aliyoicheza Jean-Claude Van Damme alicheza pamoja na Dolph Lundgren

Wednesday, November 18

Rapa Mkali Toka Kitambo..Snoop Dogg aponda vikali orodha ya Billboard ya rappers wakali wa muda wote....

Snoop-Dog-Main
Rapa mkongwe duniani Snoop Dog ameponda vikali orodha ya rapa wakali zaidi wa muda wote iliyotolewa na tovuti ya Billboard wiki iliyopita.
Majina kwenye orodha hii yalikuwa pamoja na Biggie, Jay Z, Eminem, Rakim, Nas, Andre 3000, Lauryn Hill, Ghostface Killah, Kendrick Lamar na Lil Wayne.
Snoop Dogg amekasirishwa kuwa Tupac hakutajwa kwenye orodha hii. Haya ndio maneno yake kwenye instagram >>“This is so disrespectful. !!“Whoever did this list need a swift kick in the Ass. No. Tupac. Come on cuz ?. Jus my opinion.“
billboard

Je Ni Sawa kusikiliza muziki wa R Kelly baada ya kujua alikuwa na mahusiano na binti mwenye miaka chini ya 18 ?.....



r kelly
Kuelekea kutoka kwa album yake ya 13 ‘The Buffet’ rnb staa R Kelly amefanyiwa mahojiano hivi karibuni na jarida la New York  kuhusu tabia na skendo yake ya zamani ya kuwa na mahusiano na mabinti wenye umri chini ya miaka 18.
Swali kubwa lilikuwa Je Ni Sawa kusikiliza muziki wa R Kelly baada ya kujua au kudhani anatabia hii ?
“Kila siku ni takuwa ni zawadi kwa watu ila hilo litabaki kuwa laana kwangu, watu milioni moja wananiongelea vibaya ila milioni nane wananipenda,so nina watu milioni tisa wanaoniongelea,hio inanifanya nizidi kubaki kwenye muziki “.
Mwandishi wa habari za burudani mjini Chicago alifanyiwa mahojiano na jarida hili pia na kusema ” Sio sahihi kuhusisha maisha binafsi ya msanii na Muziki au sanaa yake, kama unapenda sanaa yake baki kuwa shabiki “.
R Kelly pia ameulizwa kama bado anatamani kuwa na mabinti wenye umri chini ya miaka 18 ?
Kelly alijibu kwa kusema ” huo ni uzushi kama uvumi mwingine tu duniani, ndio maana siongelea mambo hayo, ningekuwa mtu wa kawaida haya mambo yasingeongelewa kuhusu mimi  “.