Wednesday, March 9

HII NDIO KOLABO YA CHEMICAL NA FID Q PAMOJA NA CLIFF MITINDO



Mwanadada Chemical afanya collabo na Fid Q na Cliff Mitindo 
Rapper Chemical amesema baada ya kusimama mwenyewe sasa ni muda wa kufanya collabo.

Chemical Amesema kuwa tayari ameshafanya wimbo na Fid Q na Cliff Mitindo.

Makali  huyo wa Sielewi, amesema  kuwa hakupenda kuanza na kushirikisha wasanii wakubwa kwakuwa alitaka asimame mwenyewe kwanza.

“Mwanzoni nilikuwa naogopa sana kufanya collabo kwasababu watu wengi wangehisi ‘umetolewa na mtu fulani,” amesema.

“Kuna collabo nimefanya na Fid Q, you can’t imagine, Chemical featuring Fid Q. Kuna Cliff Mitindo, kwahiyo ukizisikiliza hizo ladha utajua kabisa itakuwa ni ngoma kali.”

No comments: