Naibu
waziri wa maji na umwagiliaji mhandisi Izack Kamwele akikagua chanzo
kikuu cha maji safi na salama cha mradi wa kuongeza upatikanaji wa maji
katika mji wa kigoma kilichopo eneo la katonga.
Baadhi ya vibarua katika mradi huo wakifukia mabomba ya kupitisha maji yanayotoka kwenye chanzo katika eneo la Katonga
Naibu waziri na Mhandisi Izack Kamwela akiongea na waandishi baada ya kukagua mradi wa maji Kigoma
Na, Editha Karlo,wa blog ya jamii Kigoma
NAIBU
Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwela amewabana
wakandarasi wa mradi wa maji wa kuongeza uwezo wa upatikanaji wa maji
safi na salama kwa Mkoa wa Kigoma kwa kushindwa kumaliza mradi kwa muda
muafaka uliokuwa ndani ya mkataba.
Akiongea
na wakandarasi hao katika ukumbi wa mikutano kwenye ofisi ya Mkuu wa
Mkoa kayika kwenye ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kutembelea mradi
huo alisema kuwa mradi huo ulitakiwa kuisha mwaka jana mwezi wa kumi na
mbili laki mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 46 tu.
"Huu
mradi ulitakiwa uishe ndani ya miezi 24 kwa mujibu wa mkataba lakini
sasa hivi ni miezi 34 mpo nje ya mkataba nataka kujua tatizo ni nini?
hii siyo kasi ya awamu ya tano"Alisema Mhandisi Kamwele.
Aliongeza
kwa kusema kuwa sasa hivi kila wiki mkandarasi anatakiwa kukaguliwa na
akishindwa kukamilisha kazi mkataba wake utavunjwa, na kama hawezi
kukamilisha kazi kwa wakati atafute wakandarasi wenzake wamsaidie tena
wakandarasi hao wawe daraja la kwanza.
Alisema
kuwa mradi huo unatakiwa kukamilika mwezi wa kumi na mbili mwaka huu na
usipo kamilika wahusika watawajibishwa kwani watakuwa wameipatia
serekali hasara kubwa.
Naye
Mhandisi mshauri wa mradi huo Michael Mwamkinga alisema kuwa mradi huo
ulitakiwa uwe umekamilika march 2015 lakini mpaka sasa ni asilimia 46 tu
za mradi huo ndo zimekamilika.
Alisema
sababu zilizopelekea mradi huo kushindwa kukamilila kwa wakati ni
mkandarasi aliyepewa tenda hiyo ambaye ni SPEECON alikopa fedha kutoka
Equity Bank na kushindwa kulipa mkopo huo atimaye bank imeamua
kumfirisi.
Mwamkinga
alisema kuwa mpaka sasa asilimia 98 za mradi huo upo chini ya bank
hiyo ambapo mradi huo unagharimu zaidi ya euro bilioni 16 chini ya
ufadhiri wa European union(umoja wa nchi za ulaya).
Alisema kuwa baada ya miezi miwili mradi huo utakuwa umekamilika kwa asilimia 70.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali mstaafu Issa Machibya alisema
kuwa hali ya upatikanaji wa maji safi na salama katika mji wa Kigoma
umeongezeka kutoka asilimia 56 mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 68
mpaka sasa kwasababu ya mradi wa uboreshaji wa maji safi na salama
vijijini.
Machibya
alisema kuwa changamoto ziluzopo Kigoma katika sekta ya maji ni upotevu
wa maji,ukosefu wa mitambo ya kusafirishia maji, upungufu wa wataalam
wa maji kwa Wilaya zote na ukosefu wa pesa za kuboreshea miradi ya maji
vijijini.
No comments:
Post a Comment