Thursday, November 19

Twende Paris...Ufaransa yaonya kuhusu shambulio la sumu....

Waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls ameonya kuwa Ufaransa huenda ikakabiliwa na shambulio la kemikali za sumu kutoka kwa makundi ya kigaidi,wakati ambapo wabunge wanajadili kuongeza hali ya hatari kufuatia shambulio la mjini Paris.

Maafisa wa polisi wa Ubelgiji wakati huohuo wamevamia maeneo masita ndani na nje ya mji wa Brussels,yanayohusishwa na mshambuliaji wa mji wa Paris Bilal Hadfi na Sala Abdeslam.
Haijabainika iwapo mshukiwa mkuu wa mashambulio hayo aliuwawa siku ya jumatano wakati wa uvamizi wa Paris.
Shambulio hilo la siku ya ijumaa liliwauwa watu 129.
Uvamizi uliofanywa nchini Ubelgiji unalenga mali katika maeneo ya Jette na Molenbeek inayohusishwa na Bilal Hadfi,raia wa Ufaransa anayeishi ubelgiji ambaye ni miongoni mwa walipuaji wa kujitolea muhanga aliyefariki katika mashambulio hayo mjini Paris,kulingana na chombo cha habari cha RTBF.
Ubvamizi mwengine huko Laken unahusishwa shambulio la Paris.
Bwana Valls analihutubia bunge la Ufaransa kabla ya kura hiyo ya kuongeza hali ya hatari kwa miezi mingine mitatu.

No comments: