Mkuu wa Baraza la Mpito la Jamhuri ya Afrika ya Kati,
Ferdinand Alexandre Nguendet ameitaka jamii ya kimataifa kuisaidia nchi
yake kuimarisha uwezo wa jeshi ili kukabiliana na hali mbaya ya
kiusalama katika nchi hiyo.
Nguendet amefafanua kuwa, serikali ina
mpango wa kuwachukua vijana 1000 kutoka kila jimbo na kuwapa mafunzo ya
kijeshi na kwa njia hiyo taifa litaweza kupata jeshi jipya na imara.
Jamhuri ya Afrika ya Kati ina majimbo 77 na endapo mpango huo wa
serikali utatekelezwa, jeshi jipya la nchi hiyo litakuwa na wanajeshi
elfu 77.
Ferdinand Alexandre Nguendet amesema njia pekee ya kurejesha
amani na utulivu Jamhuri ya Afrika ya Kati ni kuwa na jeshi imara na
lenye uwezo wa kulinda mipaka ya nchi lakini pia kudhibiti hali ya mambo
ndani ya nchi.
No comments:
Post a Comment