Wednesday, November 18

URUSI: Marekani inafanya mchezo mchafu Syria....


Russia: Marekani inafanya mchezo mchafu Syria
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesema Marekani inaendeleza mchezo mchafu na hatari nchini Syria, hatua inayofanya kuwa vigumu kubainisha nia ya Washington kuhusu mzozo wa nchi hiyo ya Kiarabu. Sergey Lavrov amesema Marekani ipo kwenye kinamasi kwa kutoa misimamo ya kukinzana kuhusu mgogoro wa Syria.
 Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesema kwa upande mmoja Marekani inaunga mkono kundi la kitakfiri la Daesh ili liangushe serikali halali ya Rais Bashar al-Assad, huku upande mwingine ikipinga mpango wa kundi hilo la kigaidi kutwaa madaraka iwapo litafanikiwa kuuangusha utawala wa Assad. Lavrov amekariri kuwa, mashambulizi ya anga ya jeshi la Marekani nchini Syria hayajazaa matunda kufikia sasa huku akipuuzilia mbali madai ya Washington kwamba vikosi vya Russia vinashambulia makazi ya raia nchini Syria.
 Hii ni katika hali ambayo, Uungaji mkono wa hali na mali wa Marekani na baadhi ya nchi za eneo ikiwemo Saudi Arabia, Qatar na Uturuki kwa wapinzani wa Syria tangu mwaka 2011 hadi sasa, umesababisha magaidi kutenda jinai za kutisha katika nchi za eneo hususan Syria na Iraq.


No comments: