Jeshi la Cameroon limetangaza kuwa limewatia nguvuni wanachama kadhaa wa kundi la kigaidi la Boko Haram.
Jeshi hilo limesema wanachama hao 19 wa kundi la Boko Haram wametiwa
nguvuni katika kitongoji cha Ketta karibu na mpaka wa nchi hiyo na
Nigeria katika operesheni iliyofanywa na jeshi la anga na la nchi kavu
la nchi hiyo.
Vyombo vya jeshi la Cameroon vimesema kuwa idadi nyingine ya
wapiganaji wa kundi la kigaidi la Boko Haram imeangamizwa katika
mashambulizi yaliyoendelea kwa kipindi cha masaa mawili.
Jeshi la Cameroon lilianzisha operesheni kali ya kuwasaka na
kuwaangamiza wanachama wa kundi la kiwahabi na kigaidi la Boko Haram
baada ya wanachama wake kuvamia eneo la kaskazini mwa nchi hiyo na kuua
idadi kubwa ya raia wa eneo hilo.
No comments:
Post a Comment