Watu 32 wameuawa
kwenye shambulio la bomu la kujitoa mhanga katika mji wa Yola, kaskazini
mashariki mwa Nigeria. Wengine 80 wamejeruhiwa.
Maafisa wa huduma
za dharura wanasema miili ya waliofariki imepelekwa vyumba vya
kuhifadhia maiti huku waliojeruhiwa wakipelekwa hospitalini.Baadhi ya majeruhi walikuwa wamevunjika miguu na mikono.
Walioshuhudia shambulio hilo wanasema lilikuwa kubwa kiasi kwamba mlipuko ulisikika kote jijini.
Shambulio hilo lilitokea karibu na soko la mboga majira ya jioni.
Mji wa Yola umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara, anasema mwandishi wa BBC aliye Abuja Abdullahi Kaura Abubakar.
Mji huo umeshuhudia milipuko miwili ya mabomu iliyoua watu zaidi ya hamsini mwaka huu na mojawapo wa miji iliyoathirika na mashambulio ya wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram.
No comments:
Post a Comment