Showing posts with label SPORTS. Show all posts
Showing posts with label SPORTS. Show all posts

Monday, November 14

AZAM FC YASAKA NA KUANDAA VIPAJI VIPYA


TanzaniaImage copyrightGOOGLE
Image captionVijana wakipepetana kuwania nafasi ya malezi ya vipaji maalum

Vijana saba wenye umri chini ya miaka 17, wamepenya kwenye majaribio ya wazi ya mwisho katika mkoa wa Dar es Salaam, yaliyoendeshwa na Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC mwishoni mwa juma.

TAIFA STARS YABAMIZWA 3-0 NA WARRIORS YA ZIMBABWE ,NYOTA WA KV OOSTENDE YA UBELGIJI AMUONESHA SAMATTA MAVITU

samata1
Mshambuliaji wa Taifa Stars, Elius Maguri akichuana na beki wa Zimbabwe, Hadebe Teenage katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe leo. Tanzania ilifungwa mabao 3-0.

Friday, October 7

LIGI YA WANAWAKE KUANZA KUTIMUA VUMBI NOVEMBA MOSI, TIMU 12 KUSHIRIKI


Timu 12 zinatarajiwa kushiriki Ligi ya Taifa ya Wanawake inayotarajiwa kuanza Novemba mosi, mwaka huu kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Maendeleo ya Soka la Wanawake na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), zilizoridhia tarehe hiyo.

Sunday, May 22

YANGA SC YAMKUNA RAIS WA FIFA GIANNI INFANTINO


Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, ameipongeza timu ya soka Young Africans ya Dar es Salaam, kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2015/16.

Thursday, April 14

BARCELONA NI KAMA SIMBA YA BONGO, YATUPWA NJE UEFA NA MAJIRANI WA MAHASIMU WAO JIJINI MADRID


Hivi majuzi timu y asoka y aSimba SC ya hapa nyumbani iling'olewa katika hatua y arobo fainali katika kombe la FA licha ya mashabiki wengi kuipa nafasi y akushinda kutokana na mwenendo mzuri iliyonayo katika ligi, lakini mbele ya Vijana wa Tanga, {Coastal Union} wakalala mbili moja mwele ya mashaiki wao jijini Dar es salaam.

vivyo hivyo hapo jana usiku Klabu ya soka ya Barcelona Jumatano ilivuliwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Atletico Madrid huku Mabao yote ya Altletico Madrid yakifungwa na Antoine Griez-mann na bao la pili likifungwa kwa mara nyingine na Antoine kwa njia ya penalti .

Kwa matokeo hayo Atletico Madrid wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 3 -2 baada ya awali kufungwa 2-1 na Barcelona katika Uwanja wa Camp Nou.

Katika mchezo mwingine Bayern Munich imefakiwa kutinga nusu fainali baada ya kuitoa Benfica kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya sare ya 2-2 katika mchezo wa jana .

Mabao ya Benfica yamefungwa na Raul Alonso Rodriguez na Anderson Souza Conceicao , na magoli ya Bayern Munich yakifungwa na Arturo Vidal na Thomas Muller .

Hivyo Atletico Madrid na Bayern Munich zinaungana na Real Madrid ya Hispania pamoja na Manchester City katika nusu fainali ambayo droo yake itapangwa siku ya Ijumaa.