Thursday, April 14

BARCELONA NI KAMA SIMBA YA BONGO, YATUPWA NJE UEFA NA MAJIRANI WA MAHASIMU WAO JIJINI MADRID


Hivi majuzi timu y asoka y aSimba SC ya hapa nyumbani iling'olewa katika hatua y arobo fainali katika kombe la FA licha ya mashabiki wengi kuipa nafasi y akushinda kutokana na mwenendo mzuri iliyonayo katika ligi, lakini mbele ya Vijana wa Tanga, {Coastal Union} wakalala mbili moja mwele ya mashaiki wao jijini Dar es salaam.

vivyo hivyo hapo jana usiku Klabu ya soka ya Barcelona Jumatano ilivuliwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Atletico Madrid huku Mabao yote ya Altletico Madrid yakifungwa na Antoine Griez-mann na bao la pili likifungwa kwa mara nyingine na Antoine kwa njia ya penalti .

Kwa matokeo hayo Atletico Madrid wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 3 -2 baada ya awali kufungwa 2-1 na Barcelona katika Uwanja wa Camp Nou.

Katika mchezo mwingine Bayern Munich imefakiwa kutinga nusu fainali baada ya kuitoa Benfica kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya sare ya 2-2 katika mchezo wa jana .

Mabao ya Benfica yamefungwa na Raul Alonso Rodriguez na Anderson Souza Conceicao , na magoli ya Bayern Munich yakifungwa na Arturo Vidal na Thomas Muller .

Hivyo Atletico Madrid na Bayern Munich zinaungana na Real Madrid ya Hispania pamoja na Manchester City katika nusu fainali ambayo droo yake itapangwa siku ya Ijumaa.

No comments: