Saturday, April 2

WAZIRI NAPE AFANYA MKUTANO NA WASAMBAZAJI WA FILAMU NA MUZIKI NCHINI LEO

ep1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiongea na wasambazaji wa filamu na muziki nchini wakati wa mkutano kati yake na wasambazaji hao uliojadili namna gani ya kuboresha tasnia hiyo kwa manufaa ya wasanii, wasambazaji na uchumi wa Taifa.(Picha Na Benjamin Sawe- WHUSM)

WAFANYAKAZI WA DAWASCO WAFANYA USAFI HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (Dawasco ) Mhandisi Cyprian Luhemeja akishiriki zoezi la usafi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na watumishi wa Dawasco.

KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE YAKUTANA KUTATHIMINI KAZI ZA KAMATI ZA BUNGE

KM1
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akiteta jambo na Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati cha Kamati ya Uongozi ya Bunge leo tarehe 2/42016 Ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.Kamati hiyo inayojumuisha Wenyeviti wote wa Kamati za Kudumu za Bunge ilikutana ili kufanya thathmini ya shughuli za kamati za Kudumu za Bunge kabla ya Serikali kuwasilisha Mapendekezo ya Mpango na ukomo wa Bajeti ya mwaka 2016/17 wiki ijayo.

WABUNGE BARANI AFRIKA WAKUTANA NA KUJADILI JINSI YA KUPINGA BIASHARA HARAMU YA SILAHA AFRIKA

LIA1
Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwahutubia baadhi ya Wabunge kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakati wa Mkutano wa kujadili namna gani nchi za Afrika zinavyoweza kupinga biashara haramu ya silaha, leo Jijini Dar es Salaam

MKUU WA WILAYA YA SIHA AONGOZA WANANCHI KUPANDA MITI SIKU YA MAZINGIRA

Mkuu wa wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia anakaimu wilaya ya Hai,Dk Charles Mlingwa akizungumza na wananchi wakati wa maadhimisho ya mazingira kwenye chanzo cha uzalishaji umeme cha Kikuletwa kinachosimamiwa na Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),kushoto ni Makamu wa Chuo hicho(Utawala na Fedha)Mhandisi Dk Erick Mgaya.

NAIBU KATIBU MKUU CCM AENDELEA NA ZIARA MAFINGA MKOANI IRINGA LEO

IR1
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajab Luhwavi akilakaiwa na Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Elisha Mwampashi ambaye ni Katibu wa CCM wilaya ya Iringa Mjini, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Mufindi katika mji mdogo wa Mafinga leo April 2, 2016, akiwa katika ziara ya kikazi, kuzungumza na watumishi wa Chama ili kusikiliza changamoto na kero zinazowakabili. Kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama. (Picha na Bashir Nkoromo).