Saturday, April 2

WAFANYAKAZI WA DAWASCO WAFANYA USAFI HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (Dawasco ) Mhandisi Cyprian Luhemeja akishiriki zoezi la usafi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na watumishi wa Dawasco.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco ,Mhandisi Cyprian Luhemeja akiweka maji katika moja ya mashine inayotumika kuzibulia miundombinu ya maji taka ijulikanayo kama Jet Machine.
Wafanyakazi wa Dawasco wakijaribu kuweka sawa mpira wa kunyunyiza maji ili kuondoa vumbi wakati wakifanya usafi katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili.
Wafanyakazi wa Dawasco  wakiendelea na usafi katika maeneo mbalimbali ya Hosptali ya Taifa ya Muhimbili.
Afisa Mtendaji Mkuu Dawasco Mhandisi Cyprin Luhemeja akimueleza jambo Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Raymond Mushi baada ya kumaliza kufanya usafi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.Wengine ni wafanyakazi wa Dawasco.
Wafanyakazi wa Dawasco wakiwa na vifaa vya kufanyia usafi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi ,Cyprian Luhemeja akitoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Mkuu wa wilaya ya Ilala ,Raymond Mushi ambaye pia alikabidhi kwa uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbi.
Baadhi ya vitu vilivyotolewa na Dawasco mara baada ya wafanyakazi wake kumaliza kufanya usafi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mkuu wa wilaya ya Ilala,Raymond Mushi akizungumza na wafanyakazi wa Dawasco mara baada ya kumaliza zoezi la usafi katika Hospitali hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco akizungumza na wanahabri mara baada ya kufanya zoezi la usafi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Meneja wa Dawasco eneo la Magomeni Mhandisi Paschal Fumbuka akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza zoezi la usafi katika Hospitai ya Taifa ya Muhimbili.
Baadhi ya vitendea kazi vya Dawasco vikiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  mara baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi.

Imeandaliwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii .
………………………………………………………………………………………………………..
Neema Mwangomo, Afisa Uhusiano, MNH.

Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam  (DAWASCO)  limefanya usafi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa lengo la kudumisha ushirikiano, lakini pia kutekeleza agizo la Rais Dk John  Magufuli la kufanya usafi katika maeneo mbalimbali nchini.
Usafi huo umeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi , Mkurugenzi wa Uuguzi na Ukunga wa Muhimbili,   Agnes Mtawa pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO  Mhandisi Cyprian Luhemeja .
Usafi huo umefanyika katika maeneo yote muhimu ya Hospitali ikiwemo utoaji wa maji taka .
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo,  Mkuu wa wilaya ya Ilala Raymond Mushi amesema zoezi la kufanya usafi lazima  halina budi kuwa endelevu ili kuhakikisha maeneo yote yanakua safi lakini pia epuka magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtawa amewashukuru DAWASCO kwa uamuzi wa kuja kufanya usafi MNH ambapo ametumia fursa hiyo  pia kuwaomba wafanyakazi wa Shirika hilo kujitolea kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa ambao wanahitaji damu.
Pamoja na mambo mengine DAWASCO wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa ambao wamelazwa Hospitalini hapo ambao wanapatiwa matibabu .

No comments: