Mshambuliaji wa Taifa Stars, Elius Maguri akichuana na beki wa Zimbabwe, Hadebe Teenage katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe leo. Tanzania ilifungwa mabao 3-0.
Timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeshindwa kutamba ugenini dhidi ya wenyeji Zimbabwe ‘The warriors’ baada ya kukubali kufungwa magoli 3-0 mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa uwanja wa Harare nchini Zimbabwe.
Dakika ya 7 Zimbabwe aliwapata goli la kwanza likifungwa na mshambuliaji hatari,Knowledge Musona anayecheza klabu ya KV Oostende ya Ubelgiji baada ya mpira uliopigwa na Mathew Rusike na Erasto Nyoni alishindwa kuokoa mpira huu na kumkuta mfungaji katika sehemu nzuri ya kufunga.
Baada ya kufungwa goli hilo vijana wa Mkwasa waliendelea kulisaka lango la wenyeji na katika dakika 25 Samatta alikosa goli la wazi akiwa peke yake na golikipa na dakika ya 27 Simon Msuva alioneshwa kadi ya njano baada ya kujiagusha ndani ya 18 na kujindai kuwa kaangusha hadi mapumziko wenyeji walikuwa mbele kwa goli hilo moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa wenyeji kuanza kulishambulia lango la Stars na mnomo dakika ya 54,Mathew Rusike alifunga bonge la goli kwa shuti baada ya Musona kuukosa mpira na kumkuta mfungaji akiwa na nafasi ya goli na kumchungulia Aisha Manula na kumuacha akiwa hana la kufanya.
Alikuwa Musona tena dakika ya 56 alifunga goli la tatu kwa kichwa baada ya kupokea mpira toka kwa Willard Katsande ikumbukwe kuwa Knowledge Musona anacheza Ligi moja na Samatta na katika klabu yake ya KV Oostende anaongoza kwa ufungaji akiwa na magoli sita na timu yake inashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 25 na msimamo wa wafungaji anashika nafasi ya nne.
Hadi mwamuzi anapuliza kipyenga cha mwisho Warriors wameibuka na ushindi wa jumla ya magoli 3-0 na kwa matokeo hayo yamewapa faida Wazimbabwe kuelekea katika viwango vya FIFA,kwa sasa Zimbabwe wapo nafasi ya 110 katika ubora wa viwango vya FIFA na Tanzania wamashika nafasi ya 144 na kwa kufungwa kwao kutawafanya washuke chini zaidi wakati orodha itakapotolewa na FIFA.
No comments:
Post a Comment