Lugha ya watu wa kabila hili inafanana sana na ile ya jamii ya wanyankole wa nchi jirani ya Uganda.
Tanaduni zao na hata mazao wanayolima (ndizi) vinafanana sana.
Zamani hakukuwa na kiberiti kwa hivyo jamii hii ilitumia vipande viwili vya mti uitwao Mrinzi.
Vipande hivyo vilivyokauka vikipekechwa hadi moto unapowaka.
Wakati wamishenari wa Ulaya walipowasili, eneo hilo lilikuwa maarufu kwa kuwa na Kadinali wa kwanza wa kikatoliki marehemu Laurian Rugambwa.
Aidha watu wa Jamii hii walizingatia sana elimu ikilinganishwa na makabila mengine nchini humo.
Mwaka wa 1978 eneo la Kagera lilivamiwa na jeshi la Uganda wakati huo chini ya uongozi wa Rais Idi Amin Dada lakini jeshi hilo lilishindwa kwa jeshi la Tanzania.
Kufikia mwaka wa 2006 idadi ya jamii ya wahaya ilikuwa zaidi ya watu milioni moja laki tatu.
hii ndio ndizi Bukoba |
Kabla ya kuwa na serikali ya taifa watemi ndio walitambuliwa kama wakuu wa jamii ya Wahaya.
Ndoa ni swala linaloheshimiwa katika kila jamii, na ni jambo linaloenziwa sana na jamii ya Wahaya.
Mahari ya Ng'ombe ama mbuzi ilitolewa kwa baba wa msichana kulingana na makubaliano ya pande zote mbili.
Wahaya wana koo 8 ambazo ni Bumbira, Edangabo, Ganda-Kiaka, Hamba, Hangiro, Mwani, Nyakisisa, Ekiziba na Yoza.
Katika jamii ya wahaya kuna mambo ambayo ni mwiko kuyafanya yaani yamekatazwa kwa mfano kukata mti aina ya Mjuju na Mjunangoma.
Mti huo wa Mjunangoma uliheshimiwa sana kwani hapo ndipo mteni alipofanya tabiko, kwa hivyo unachukuliwa kama mti mtakatifu.
Aidha wanawake hawaruhusiwi kula wadudu aina ya senene ambao ni maarufu sana kwenye jamii hii,
Iwapo mtemi angehitaji kutembea kwenda kijijini sokoni ama popote pale kwenye eneo lake basi alibebwa juu na watu wake akiwa ameketi juu ya machela maalum.
Watu walilibeba machela hiyo kwa zamu kutoka eneo moja hadi lingine. Na walifurahia sana kumbeba mtemi walichukulia fursa hiyo kama ni baraka.
Mtemi Emanuel aliyefiriki alirithiwa na mwanawe wa kiume wa kwanza Innocent Rukamba.
Nyumba ya jadi ya Wahaya iitwayo nyaruju ilijengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi kwenye paa na hata kuta zake.
nyumba aina ya Nyaruju |
Yaani hii ni nyumba ya nyasi kwa jumla hakuna udongo.
Sakafuni kumetandazwa nyasi maalum inayotumika kama zulia.
kwa kawaida walio wengi Kwenye nyumba moja wanaishi watu pamoja na mbuzi wao ikiwa wanafuga mbuzi.
Utamaduni wa Wahaya una historia ndefu
Inaaminika kwamba wao ni kati ya watu wa kwanza kuanzisha shughuli za utengenezaji wa bidhaa za chuma cha pua.
jumba la makumbusho la Kagera mjini Bukoba.
Hili ni jumba maridadi la makumbusho ambako kuna baadhi ya vitu vilivyotumiwa na jamii ya Wahaya kama vile vibuyu vya kuhifadhia pombe ya kienyeji.
Aidha kuna kifaa kilichotumiwa kuchemsha mawe ya Chuma aina ya iron.
Ukutani kuna picha za wanyama miti, ndege, samaki na nyoka wanaopatikana kwenye eneo la jamii ya Wahaya.
wahaya wana vyakula vya aina nyingi lakini chakula chao kikuu ni ndizi ambapo chakula hiki hupikwa kwa njia mbali mbali na moja ya aina yenye mvuto zaidi ni hii hapa katika picha ambayo yenyewe ndizi,uchanganywa na maharagwe,na nyama au samaki humo humo.
pia ugali huliwa japo kwa kiasi kidogo sana,ambapo huliwa na mboga yoyote ile lakini hujiskia raha kama watakula ugali na Senene.
Mlo wa ugali na Senene |
katika aina nyingine za ndizi kuna hii inaitwa enkonjwa, huliwa baada ya kuchomwa misli ya mihogo,na mara chache sana huchemshwa.
ndizi aina ya Enkonj |
No comments:
Post a Comment