Wednesday, November 18

Marufuku Kuvaa....Senegal yapiga marufuku vazi la burqa.....

Senegal yapiga marufuku vazi la burqaSerikali ya Senegal imetoa taarifa rasmi ya kupiga marufuku vazi la stara la burqa, linalovaliwa na wanawake wa Kiislamu. Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo ya Kiafrika imesema kuwa, ni marufuku kuanzia sasa kuvaa burqa nchini humo, kutokana na sababu zilizotajwa kuwa za kiusalama. 
Gazeti la L’Observanteur la nchi hiyo limesema kuwa Rais Macky Sall ametia saini sheria hiyo, kufuatia mashinikizo kutoka kwa taasisi za kiusalama na kiulinzi za nchi hiyo.
 Hii ni katika hali ambayo, katika mkutano wa usalama na amani wa bara Afrika uliofanyika Jumatatu iliyopita mjini Dakar, Rais Sall alidokeza kuwa vazi hilo linafanya vita dhidi ya ugaidi kuwa vigumu. 
Miezi michache iliyopita, Cameroon nayo ilipiga marufuku vazi hilo la heshima la Kiislamu.
 Viongozi wa Cameroon walichukua uamuzi huo baada ya kujiri mlipuko uliouwa watu 13 na kujeruhi wengine 31 mwezi Julai mwaka huu.


No comments: