Bunge la Rwanda
17.11.2015 21:48
Baraza la seneti nchini Rwanda limepitisha mabadiliko mapya ya
kipengele cha katiba kitakachomruhusu Rais Paul kagame kuendelea kubaki
madarakani hadi mwaka 2034.
Uwamuzi huo ulichukuliwa kwa sauti moja siku ya Alhamis. Mabadiliko yaliyopendekezwa yatafikishwa mbele ya wananchi ili kuweza kupiga kura ya maoni ambayo inatarajiwa kupata ushindi kiurahisi.
Rais Kagame mwenye umri wa miaka 58, ameiongoza nchi ya Rwanda tangu
jeshi lake lilipomaliza mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 na kuwaondoa
madarakani wahutu wenye msimamo mkali nchini humo. Chini ya sheria
iliyopo hivi sasa, bwana Kagame anatakiwa kujiuzulu mwishoni mwa muhula
wake wa pili madarakani mwaka 2017.
Lakini kipengele kilichopendekezwa kinamruhusu bwana Kagame kuwania muhula mwingine wa miaka saba madarakani, kisha ikifuatiwa na mihula miwili ya miaka mitano madarakani.
Uwamuzi huo ulichukuliwa kwa sauti moja siku ya Alhamis. Mabadiliko yaliyopendekezwa yatafikishwa mbele ya wananchi ili kuweza kupiga kura ya maoni ambayo inatarajiwa kupata ushindi kiurahisi.
Lakini kipengele kilichopendekezwa kinamruhusu bwana Kagame kuwania muhula mwingine wa miaka saba madarakani, kisha ikifuatiwa na mihula miwili ya miaka mitano madarakani.
No comments:
Post a Comment