Thursday, November 19

TAIFA STARS..Kichapo cha Bao 7-0 kwa Taifa Stars dhidi ya Algeria kimemvunjia rekodi hii Mkwasa …

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars November 17 ilicheza mchezo wake wa pili wa marudiano ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2018 Urusi dhidi ya Algeria Blida katika uwanja wa Mustapha Tchaker  na kukubali kipigo cha magoli 7-0,  idadi ya magoli ambayo iliifanya Tanzania kuingia katika headlines ya ya kufungwa idadi kubwa ya magoli.
November 18 kocha wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa ameongelea namna alivyokipokea kipigo hicho na kufanya kiweke historia kwake kwani kwa miaka yake 25 katika soka hakuwahi kuweka rekodi ya kupokea kipigo cha magoli mengi kiasi hicho kitu ambacho hakikuwaumiza watanzania hata yeye.
DSC_0041
“Kiukweli hata mimi ilinishangaza kidogo na tulizidiwa umeona uwezo wa mchezaji wao Yacine Brahimi uwezo wake ni mkubwa kikosi chao kilibadilika ila uwanja pia ulikuwa tatizo ulikuwa unateleza hata goli la kwanza tulilofungwa lilitokana na hivyo, kufungwa goli 7 sijawahi kiukweli katika miaka 25 yangu katika soka” >>> Boniface Mkwasa

No comments: