Serikali
imesema haina mpango wa kubadili vyeti vya wanafunzi waliomaliza kidato
cha sita mwaka jana kutoka kwenye mfumo wa alama za GPA kwenda
Divisheni.
Msimamo huo wa serikali, umetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako.
Amesema
serikali haina mpango wa kubadili mfumo huo wa vyeti kwani tangu awali
wanafunzi walisoma kwa mfumo wa GPA na vyeti vilitoka kwa mfumo huo.
“Hatuwezi
kubadili vyeti hivyo, isipokuwa vimehitajika kwa ajili ya marekebisho
madogo ambayo Katibu Mkuu wa Wizara, aliyasema lakini siyo kubadili
kwenda mfumo wa divisheni,” alisema.
Februari
mwaka huu, Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), lilitangaza kusitishwa
kwa ugawaji wa vyeti vya kidato cha sita kwa wanafunzi waliohitimu mwaka
2015, huku likiagiza kuwa vile vilivyokwisha gawanywa kwa wahitimu hao
vinatakiwa kurejeshwa kwenye chombo hicho.
Hata
hivyo, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk, Charles Msonde, hakubainisha
marekebisho ambayo wanatakiwa kuyafanya kwenye vyeti hivyo na badala
yake kudai baraza linataka kujiridhisha na baadhi ya vitu.
Hatua
hiyo ya kubadili vyeti hivyo iliibua utata mkubwa, huku baadhi ya wadau
wakiwamo maofisa elimu, wakihisi Necta huenda inalenga kuvibadili vyeti
hivyo kutoka kwenye mfumo wa wastani wa alama (GPA), kwenda kwenye ule
wa jumla (division).
No comments:
Post a Comment