Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Bi. Margareth Nzuki akiwasilisha malengo ya warsha kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida kufungua warsha hiyo.
Wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam wamefanikiwa kupata nafasi ya mafunzo yanayohusu fursa mpya zinazopatikana katika kilimo cha biashara katika warsha iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF).
Elimu ambayo wajasiriamali waliipata katika warsha hiyo ni elimu ya shamba kitalu na ujasiriamali, elimu ya kilimo cha foda na mbogamboga, elimu ya kilimo na kufuga samaki katika matanki, elimu ya ufugaji samaki katika mabwawa, elimu ya ufugaji samaki katika vizimba, kutazama fursa zilizopo katika ufugaji bora wa kuku na kupata elimu kuhusu Azolla ambayo inaweza kutumika kama chakula cha mifugo na pia kama mbolea.
Akizungumza katika warsha hiyo mmoja wa wawasilishaji mada, Dominic Haule alisema kilimo kina fursa nyingi lakini watu wengi wanashindwa kufanikiwa kutokana na kuwepo mambo mbalimbali ambayo yanayakwamisha.
Alisema changamoto hizo ni pamoja na kukosa elimu ya kilimo na kushindwa kupata taarifa sahihi za kiteknolojia kuhusu kilimo cha kisasa.
“Tunahitaji kutazama fursa zilizopo, zipo nyingi lakini bado tunakabiliwa na changamoto wakulima wanakosa elimu ya kilimo kujua hata mazao bora yanakuwaje, bado kuna shida ya pembejeo na mitaji inakuwa changamoto maana ili ufanikiwe unahitaji uwekezaji mkubwa,” alisema Haule.
Awali akitoa neno la ufunguzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida alisema Tanzania ina maeneo mazuri ya kufanyia kilimo na kinachohitajika ni wakulima kutambua njia za kufanya kilimo bora ili watakapoanza kulima waweze kupata matokeo mazuri kwa aina ya kilimo wanachofanya.
“Uchumi wa nchi unategemea kilimo, nchi yetu ina eneo zuri la kilimo lakini bado kuna changamoto kama mabadiliko ya hali ya nchi ni vyema kukutana na kujua njia bora za kutumia kabla ya kuanza kufanya kilimo,” alisema Dkt. Kida.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akifungua warsha ya siku moja yenye lengo la kutambulisha na kuelimisha zaidi wananchi kuhusu fursa mpya za kibiashara ambazo zinapatikana katika sekta ya Kilimo.
Mshereheshaji katika warsha ya kutazama fursa mpya katika kilimo biashara, Abdallah Hassan.
Mwakilishi wa Wizara ya Kilimo, Mifungo na Uvuvi , John Mapunda akielezea nafasi ya serikali kuwasaidia wajasiriamali ili kufikia malengo yao katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na ESRF.
Pichani juu na chini ni umati wa washiriki kutoka mikoani na maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam waliohudhuria warsha hiyo iliyoandaliwa na ESRF.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akifurahi jambo na mwakilishi wa Wizara ya Kilimo, Mifungo na Uvuvi, John Mapunda katika warsha hiyo.
Dominic Haule kutoka chuo cha iMADS akielezea kuhusu shamba kitalu na ujasiriamali.
Bw. Abdullatif Mbulo kutoka Horti Ogranics Ltd, akielezea kuhusu kilimocha foda na mbogamboga, sambamba na ufugaji wa samaki katika matanki.
Luteni Joseph Lyakulwa, kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) akizungumzia Ufugaji wa Samaki katika Vizimba katika warsha hiyo iliyohudhuriwa na wajasiliamali mbalimbali.
Pichani juu na chini washiriki wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalamu wa Kilimo Biashara.
Pichani juu na chini washiriki wakiuliza maswali kwa wawasilishaji mada katika warsha ya siku moja ya Kilimo Biashara iliyoandaliwa na ESRF.
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida akizungumza na waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment